Boti ya Seagull ifanyayo safari zake kati ya Dar na Zanzibar ikiwa Jahazi iliyokuwa ikitokea ng'ambo ya pili kwa upande wa kigamboni. Chanzo cha ajali hii inasemekana ni kubadilika kwa muelekeo wa upepo kulikoipelekea Jahazi hiyo kwenda kujipiga katika boti hiyo iliyokuwa safarini kuelekea Zanzibar. Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha katika ajali hiyo kwani walivyoona mambo yamekwenda kombo wote waliokuwemo ndani ya Jahazi hiyo waliruka ambapo wengine walidandia kwenye hilo boti na wengine waliokolewa na mashua za uvuvi.
Jahazi ikizama mara baada ya kugongwa na boti ya Seagull baada ya kupoteza muelekeo na kwenga kujipigiza katika boti hiyo ambayo ilikuwa safarini kwenda Zanzibar. Ajali hii imetokea leo hii majira ya saa 5 asubuhi jijini Dar.
Jahazi likizidi kuzama
waokoaji waliwahi kufika eneo la tukio na kuokoa waliokuwepo ndani ya Jahazi

HABARI ZIMETUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA KUNA AJALI YA MAJINI IMETOKEA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM KARIBU NA FERI AMBAPO INASEMEKANA BOTI YA ABIRIA IENDAYO KASI IMEGONGA JAHAZI NA KUISABABISHA IZAME. JUHUDI ZA KUOKOA WALIOKUWA KWENYE JAHAZI ZINAENDELEA. TIMU YA GLOBU YA JAMII IKO ENEO LA TUKIO NA HABARI ZAIDI BAADAYE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2010

    Jahazi??...Ngalawa??...Boti??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2010

    ".. nakusababisha izame." Boti ilizama au jahazi lilizama? Nimeani kiswahili ni kigumu.

    ReplyDelete
  3. Regular Yacht SkipperJune 28, 2010


    Huyo Captain wa Seagull inaonyesha hazifahamu sheria za majini wala haelewi kwamba Jahazi zinapelekwa kwa upepo. Sheria na majini zinazipa boti ambazo zinatumia upepo "advatage" kwa vile mwendo na muelekeo wake unategemea upepo na sio injini ambayo inaweza kwenda mbele nyuma au kushoto/kulia.
    Mimi naomba tu hao wenye Seagull wamlipe mmyonge fidia yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...