Na Woinde Shizza, Arusha
Mtu mmoja ambaye hakuweza kutambulika jina kwa haraka anayesadikiwa kuwa jambazi Mkoani Arusha amepigwa risasi ubavuni mara baada ya kutaka kuvamia katika kituo cha mafuta cha ToTal kilichopo katika eneo la Kimandolu nje kidogo ya mji
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Basilio Matei alisema kuwa tukiohilo lilitokea eneo la Kimandolu majira ya saa 5 asubahi ambapo majambazi hao walikuwa wakitaka kuvamia katika kituo cha mafuta cha Total kilichopo nje kidogo ya mji.
Alisema kuwa polisi walipewa taarifa na raiya mwema ambaye hakuweza kumtaja jina na kusema kuwa kuna majambazi walikuwa wamepanga kuvamia kituo hicho cha mafuta kilichopo kimandolu wakiwa na nia ya kuchukuwa fedha zote za mauzo za wiki nzima.
Alisema kuwa baada ya polisi kupata taarifa hizo waliamua kufuatilia na katika kituo hicho cha mafuta na kuongeza kuwa mara baada ya kufika katika kituo hicho cha mafuta muda kidogo waliona gari aina ya Toyota Korola ambayo ilikuwa haina namba.
Amebainisha kuwa mara baada ya gari hiyo kufika gari hilo ambalo lilikuwa limewabeba majambazi wanne ndipo majambazi wawili walishuka na kuelekea katika kituo hicho cha mafuta na kusema kuwa wakati walipokuwa wakielekea katika kituo hicho ndipo askari mmoja aliyekuwa na pikipiki akapita katika kituo hicho cha mafuta .
"sasa walipoona askari yule amepita walishutuka na kuanza kurusha risasi hewani huku wakimbia kimbia kuelekea katika lile gari ambalo walikuwa wamekuja nalo sasa katika zile kurukushani ndipo polisi wetu alimuwahi mmoja wapo na kumpiga risasi ya mbavuni"alisema Matei.
Kamanda alibainisha kuwa wakati kurukushani zikiendelea ndipo jambazi moja ambalo lilishuka likakimbilia katika vimitaa vilivyopo katika maeneo hayo huku majambazi wengine waliokuwa kwenye gari wakiwa wamekimbilia pasipo julikana.
Aidha alisema jambazi huyo aliyepigwa risasi alikutwa akiwa na bastola aina ya BROWNING cz83 yenye no A27411 ambayo inasemekana imetengenezwa czeck na alisema kuwa jambazi huyo alifariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
Matei alimalizia kwa kusema kuwa nia ya jeshi lake la polisi ni kuwamalizi majambazi wote ambao wanawasumbua wananchi na wanaitaji wananchi wao kuishi na amani bila ya kuwa na wasiwasi wowote ule na amewataka raia wema kuendelea kutoa ushirikianao kwa polisi ili kuweza kumaliza tatizo hili kabasa.

Polisi wetu wanamatatizo sana, hivi ni nini? Mmepewa taarifa ya ujambazi, mnaenda katika tukio na mnafanikiwa kumuua jambazi mmoja watatu wanatoroka? Sasa usalama wa mtoa habari uko wapi ikiwa majambazi hamjafanikiwa kuwakamata?
ReplyDeleteTusiwalaumu sana polisi, wamejitahidi ila wakati ujao wajizatiti zaidi na kupena taarifa ili wajikusanye wengi na kuweza kuwakabili wote kabisa. Hii itasaidia sana maana hawa majambazi wakikuwahi wewe wanakuua pia. Hivyo ni vema tu wanapokamatwa wakiwa katika ujambazi na silaha zao wawadhibiti ipasavyo hata kama ni kwa kuwavunja vunja viungo tu ili walemae na wasiweze kufaya ujambazi wao na unyama kila kukicha.
ReplyDelete