
Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,inaripoti kuwa msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini,Joseph Mbilinyi a.k.a mr II amekamatwa leo mapema asubuhi na watu wanaodaiwa kuwa ni wanausalama wakati anakwenda kwenye kikao cha press talk kinachofanyika kila siku ya jumatatu katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),sababu ya kukamatwa kwake bado haijajulikana na haijulikani wamekwenda nae wapi.
Globu ya Jamii inafuatilia kutaka kujua mustakabali mzima wa kukamatwa kwake na italeta taarifa kamili hapo baadae.hivyo tuvute subira.
Mtu akitangaza kujiunga na chama cha upinzani anaandamwa namna hii kwa nini jamani? itafika siku kila mwananchi mzalendo ataingia msituni kudai haki yake.
ReplyDeleterecording yake ya kuwataja virusi wanaoharibu tasnia ya muziki wa Tanzania ndo imemponza
ReplyDelete"wanachotaka wewe upate taabu shida kibao bila sababu.."..na mama hizo nitazikabili...Dawa ya jeuli uwe kiburi...Go go sugu mwana sana hapa Tampere Finland..tupo pamoja mpaka tone la damu la mwisho...
ReplyDeletePigania usawa....wakikutoa roho bado itikadi zako zitabaki...
Wanamwita sugu ..sugu sugu sugu.,..
WAMESHAANZA HAO,HIVI MAMBO HAYA MPAKA LINI SIASA ZA BONGO,YAANI MTU AKITAKA KUINGIA KWENYE BONGO POLITIKI NI LAZIMA AWE KWENYE HICHO CHAMA CHENU?EBOO HEBU ACHENI UOGA MNA KILA KITU LAKINI HAMJIAMINI SASA MTU KAMA MR 2 NYIE ATAWAATHIRI NINI ZAIDI YA KUMPANDISHA CHART TU MWANASIASA HUYO UNDERGROUND KATIKA SIASA ZA BONGO,MH.HALIMA MDEE WEWE MWANASHERIA HEBU JARIBU KUFUATILIA SUALA LA MWANACHADEMA HUYU MPYA UJUE LIMEKAAJE,
ReplyDeleteAsije akawa kajiingiza kwenye mihadarati!!! dRU
ReplyDeleteChadema nini ? michuzi usibanie Coment za watu zikianza Kudondoka Michuzi jnr tunajuwa anabania sababu ya Clouds. Mwacheni Kijana msimsingizie jamani.
ReplyDeletewasije wakamnanii kijana wa watu. haki yake wametafuna, bado wanamtafuta? Haya, Chadema .. kijana wenu anaanza kuonja joto ya jiwe!
ReplyDeletehaya ndo matokeo tuliyokua tunayasubili,sugu si umejifanya kujiunga na chadema!bado mkoloni na g-solo nao kutiwa baloni!!habari ndo hiyo ccm ina wenyewe ndugu zangu!!
ReplyDeletewenzako wanavyo chukua kadi za ccm siyo kwamba wanapenda tu au ni kama ccm ndo chama kizuri !!! pole kaka ndo siyasa za bongo system ndo hiyo kweli haki akuna bongo! mumu niebushe nisirudi bongo mimi sitaki sitaki kabisa kuja uko !!
ReplyDeleteSerikali vijana wenye hasira za ku fail maisha tunayaona haya, siku tukiamua watoto wenu wa Oysterbay hawawezi kutuzidi nguvu. Tanzania ni kubwa kuliko Dar es Salaam. Ni hayo tuu!!!
ReplyDeleteSiasa za kizamani sana hizi.
ReplyDeleteBwana mdogo mr 2 mbona unaingia mkenge kichwa kichwa?
ReplyDeleteLabda CCM imemkamata kwa sababu SUGU ameamua kujiunga na Chadema ili kupiga vita ufisadi wa CCM.
ReplyDeleteHawan lolote la kumfanya...Tanzania inaongozwa na Sheria. Kama wana kesi wampeleke mahakamani tusikie makosa yake.
ReplyDeleteMr Two wewe kichwa cha panzi kabisa. Nilipoona unajiunga na Chadema nikajuwa unajua matatizo uliyonayo na unatafuta namna ya kuyaondoka.
ReplyDeleteTZ waachie wenyewe, muulize Mtikila, Seif sharif Hamad, na Jumbe. kumbuka ule msemo unaosema Ukishindwa, jiunge nao.
Huoni jinsi huyo kabwe, Cheyo na Mbowe wanavyokula nao hao jamaa na kupuliza. Utaishia kuwekwa ndani na kama una ka-green kako ka US, basi ujue jamaa wausalama bongo wanakampango ka kukuharibia. Kubali wamekushinda, jiunge nayo then nyamaza huku ukila asilimia 20 badala ya ile 80 unayotaka wewe. jaribu kukua au kwenda na umri Mbilinyi, unakaribia 40, waza kiforty na sio ki20 sugu.
pole lakini kw yote yaliyokukuta.
Kiranga Haliliwi wala halaliwi Tanga..
ReplyDeletehii yote ni kwa sababu ya kuchukua kadi ya Chadema nini?
ReplyDeleteNahis jamaa kakamatwa sababu ya wimbo mpya unaitwa Anti-Virus ambapo amewaponda clouds live live.Sikiliza maneno yake.Linki hii hapa:
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=hiMGe2HYq2o
Nchi hii haina uhuru binafsi, demokrasia wala utawala wa sheria.
ReplyDeleteKwa nini mtu akamatwe kwa kujiunga na chama halali cha siasa?
Nchi hii haitaendelea kama haya hayaishi!!!!!!!!!!!!!!!!
Mmh, huu wimbo umemnyanyapaa mtu, its not right kunyanyapaa mtu mwenye ugonjwa.Tukana utakalo kama mtu kakutukana au kakukwaza, ila unyanyapaaji noo, its too much
ReplyDeleteWe michuzi mbona unabania points za maana ambazo hazina hata matusi?
ReplyDeleteMr II nimeangalia youtube yako (mwangaliaji namba 777).. aisee sema bwana. Bila kusema watu huwa hawasikiagi.
Nice song by the way.
Polisi ilipaswa wawakamate watu waliotamkwa kuwapa mimba watoto wa Tanzania House of Talents, na sio kumkamata MR II. Huu ni ujinga.
ReplyDeletenadhani kakamatwa kwa sababu amejiunga na chadema!
ReplyDeleteduh siasa za bongo noma.