Meza kuu ikijiandaa kutoa kombe kwa timu ya Foo
Nahodha wa timu ya Foo akipokea kombe la ubingwa

Mashabiki na wachezaji wa Foo wakisherehekea ubingwa
Na Woinde Shizza
wa
Globu ya Jamii, Kilimanjaro

Timu ya Foo ya mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kutwaa taji la kombe la ligi ya Fuya Kimbita Cup lililokuwa likiendelea katika wilaya ya Hai iliyoko mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarif ailiyotolewa na mratibu wa mashindano hayo Norman Sigalla alisema kuwa mashindano hayo yalianza mapema May na yamemalizika June 6 mwaka huu katika viwanja vya CCM vilivyopo wilayani ya Hai mjini.

Alisema kuwa mashindano haya yameshirikisha jumla ya timu zipatazo 76 zilizopo katika vijiji na kata za wilaya hiyo na mashindano haya yaliendeshwa kwa mfumo wa ligi hadi yalipo fikia tamati.

Aliongeza kuwa mashindano haya yalianza ramsi kwa kushindanisha timu zilizopo katika vijiji na hata kupata timu moja na kila timu ilicheza katika mashindano ya kata kwa njia ya mtoano awamu ya kwanza ilimalizika kwa kupatikana timu mbili za kila kata ambazo zilienda katika kucheza katika tarafa na kuchagua bigwa wawili katika tarafa zote za wilaya ya hai.

Aliongeza kuwa bigwa aliyepatikana hapa ndiye aliyeshiriki mashindano haya katika ngazi ya fainali ambayo walicheza katika mfumo wa ligi wa kujikusanyia pointi.

Aliwataja timu ambazo zilifanikiwa kufika hatua ya mwisho kuwa ni timu ya Kia ,Mbwera ,Bomani,Foo,Uroki pamoja na tasakero alisema timu hizi zilishindanishwa kwa mfumo wa ligi wa kucheza ndani na nje kwa kujikusanyia pointi.

Alisema kuwa hitimisho la mashindano haya ni kupata mshindi wa kwanza wapili ,watatu na hata wane alizitaja timu ambazo zimeshinda kuwa ni Foo ambao waliondoka na kitita cha shilingi laki tano pamoja na kombe lenye thamani ya shilingi laki tano na nusu uku mshindi wa pili Bomani ambao waliondoka na kitita cha shilingi laki tatu na mshindi wa tatu ambaye ni Kia aliondoka na kitita cha shilingi laki mbili na mshindi wa nne akiwa ni Mbwera aliyeondoka na kitita cha shilingi laki moja aliongeza kuwa pia katika mashindano haya kulikuwa na timu yenye nithamu ambayo ni Roo ya machame ambayo yenyewe iliondoka na kitita cha shilingi laki moja

Alisema kuwa mashindo haya yameandaliwa na mbunge wa jimbo la hai mjini Fuya Kimbita ambayo ndiyo ambao jina lake limebeba jina la mashindano na pia alimuomba mbunge huyo kufanya mashindano hayo kuwa endelevu.

Kwa upande wa mbunge huyo ambaye pia ndie aliyekuwa mgeni rasmi alisema kuwa amefurahi kuona kuwa wananchi na vijana wa moshi wanapenda michezo kwani wamejitokeza kwa wingi na alihaidi kuwasaidia kwa mambo mbalimbali hasw aya kimichezo.

Alisema kuwa anafurahi kuona vija wengi ndio ambao wamejitokeza katika mashindao haya na wameamua kuacha kazi zao na kuja katika mashindano na aliwasihii wasihishie hapa kwani mchezo ni afya michezo ni ajira na michezo pia ni burudani na alisema kua iwapo wakiendelea kushiriki michezo hii basi ata muda wa kukaa katika makundi maovu hawata kuwa nayo..




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...