Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mhashamu Elisa Buberwa akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya kanisa la Kashura mjini Bukoba Jumapili kushiriki katika maadhimisho ya jubilii ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo. Katikati ni Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini Askofu Dr.Alex Malasusa. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa kanisa la KKKT nchini Tanzania Askofu Dk. Alex Malasusa wakati wa maadhimisho ya jubilei ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo iliyofanyika katika kanisa la KKKT la Kashura, wilayani Bukoba. mkoa wa Kagera.
Baadhi ya waumini wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi wakihudhuria sherehe za kuadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hili huko Kashura Bukoba mjini Jumapili mchana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2010

    Jana tulitangaziwa kwamba KKKT imeanzishwa mwaka 1963. Hii post inasema miaka 100 ya KKKT. Who is right?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2010

    mdau wa kwanza si uingie google kukata mzizi wa fitna?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2010

    Mdau wa 10.45 we acha tuu!!
    Watu wengine wavivu wa kufikiri.

    ReplyDelete
  4. Lumuli LwikunuloJune 21, 2010

    Muuliza swali ameuliza swali ambalo watu wengi linawachanganya. Aki-google kutafuta jibu anaweza kupata maelezo au hata inaweza pia ikamchanganya zaidi. Hali halisi ni kwamba 'KKKT' na 'Kanisa la KKKT- Kashura Bukoba' ni vitu viwili tofauti lakini vina uhusiano wa karibu sana. KKKT ni muungano wa Dayosisi mbalimbali za makanisa ya Kilutheri nchini Tanzania. Dayosisi (makanisa) hayo ikiwemo Kashura-Bukoba, Konde-Tukuyu,n.k. yalianza zamani wakati wa ukoloni.Dayosisi (Kanisa)ya Konde Tukuyu kwa mfano walisherehekea Jubilee ya miaka 100 miaka ishirini hivi iliyopita. Wakati wa ukoloni hakukua na muungano wa pamoja unaoitwa KKKT. Kila Dayosisi (Kanisa) ilikuwa inajitegemea.Baada ya uhuru yaani 1963 wakaamua kuunda umoja huo ambao Askofu Gerhaz Malasusa ambae pia ni askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ndiye Mkuu wake.Kumbuka pia kuwa kila Dayosisi ina askofu wake.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2010

    Nawewe Lumuli umechapia Gerhaz mwalasusa ni baba yake Alex mwalasusa ambaye ndio askofu Gerhaz alikuwa mchungaji tu, hakuwahi kuwa askofu, wewe ndio unaongezea mkorogo kabisa!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2010

    mdau uliyesema kaongezea mkorogo umeniua kwi kwi kwiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...