Mama Dora Kaseko Mpangile
Kwa wana blogu ya jamii salaam.
Naitwa Dora Kaseko Mpangile, nagombea udiwani Kata ya Kiwanja cha Ndege Morogoro CCM viti maalum. Lengo langu ni kushirikiana, elimishana, wezeshana, na kusaidiana katika kuhamasisha kinamama/dada kujikwamua toka katika hali duni na kujiendeleza kufikia viwango vinavyokubalika duniani.
Tunaweza kusema haya ni malengo makubwa sana, la hasha, kama watu wawili kati ya kumi wakifikia malengo haya basi hao wawili hawanabudi kuwawezesha wengine wanne na mwishowe taratibu tunafikia lengo letu.
Basi, kwanza nawashukuru na ninaomba maoni yenu na michango yenu ya hali na mali katika kutimiza lengo hili.
Unaweza kuwasiliana nami kwa e-mail ifuatayo dorampangile@yahoo.com na pia niko kwenye facebook - Dora Mpangile- hapo tutaweza kuwasiliana vema.
Asanteni sana wanablogu ya jamii

Photoshop au?
ReplyDeleteMama, mimi niko NYUMA yako. Lakini niahidi MSHIKO!!!
ReplyDeleteOk.......what is your VISION?
ReplyDeleteMbije,A
kwa nini usijiamini ukagombee kwenye kata. Why viti maalum bibi?
ReplyDeleteSafi sana mama Mpangile, ila ungegombea viti halisi, sio hivi vya kupewa (maalum).
ReplyDeleteIla hata hivyo naomba nikupe sapoti ya nguvu.
Nitakuchapishia fulana za kampeni.
Mdau wa Mwenge - Dar
Mdau Mbije,
ReplyDelete"VISION" nenda kwenye facebook Dora Mpangile hapo utapata jibu la swali lako natumaini kwa kufupi hapo juu pia nimeandika.
Asante.
Nashukuru kwa mchango wenu wanangu wote na wanablogu ya jamii mmoja wetu akishinda wote tumeshinda na huu ndio msimamo wetu.
ReplyDeleteTaratibu ndio mwendo tunaanza na huku mbali na kujifunza na taratibu kwa msaada wenu tutajikuta kukiendelea mbele hatua moja kwa kila muda.
Asanteni.
Mimi nakufagilia sana Mama Mpangile, isipokuwa kitu kidogo samahani kama nitakuudhi.
ReplyDeleteMake up yako ni almost caking na haiba yako japo nzuri overmake up inaharibu kidogo.
Ukiondoa hayo yote mimi nakupa kura ya ndiyo!!!
BONGE LA SMILLING FACE
ReplyDeletemichuzi acha kubana niachie haki yangu ya kuongea mi nasema sorry bibi kura yangu kwa vijana !!!
ReplyDeleteDuh!, haya kila la kheri. Ila ange.. aaakh basi najua 90% ya ninayotaka kuyaandika yatafanya mtu flani animinye
ReplyDeleteNashukuru wanablogu wa jamii kwa pale tunapo kubaliana na kupishana, hii ndio demokrasia tuna uhuru wa kutoa maoni yetu hata yakiwa yanapingana.
ReplyDeleteKuwajibika ni kuwajibika iwe kwa kuchaguliwa,kuteuliwa, au kujiari, binafsi naamini matunda ya kazi yatapimika tu kwa kila tendo/jambo kuna matokeo.
Naamini demokrasia ni kwa wakubwa na wadogo. Katika majukwaa ya siasa kuna umri unaohitajika basi kwa maoni yangu vijana na wazee tujiunge pamoja kufikia viwango vya demokrasia na maendeleo yanayokubalika katika uwanja wa kimataifa.
Asanteni.
Dora Mpangile