Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiagana na Mama Maria Nyerere muda mfupi baada ya kumalizika kwa misa Maalumu ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili atangazwe kuwa Mwenye Heri iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mashahidi wa Uganda huko Namugongo, nje kidogo ya mji wa Kampala leo asubuhi.Misa hiyo iliyohudhuriwa pia na baadhi ya waumini kutoka Tanzania ni sehemu ya mchakato ilioanzishwa na kanisa Katoliki Tanzania wenye nia ya kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu kulingana na vigezo na kanuni zilizowekwa na Kanisa hilo.
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya ibada maalumu kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa la Mashahidi wafia dini wa Uganda huko eneo la Namugongo, nje kidogo ya jiji la Kampala leo asubuhi.Wa kwanza kushoto ni Askofu Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba na wapili kushoto ni Dr.Cyprian Lwanga Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Kanisa Katoliki Kampala.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiasalimiana na baadhi ya Watanzania waliohudhuria ibada maalumu ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kanisa Katoliki ya Mashahidi wafia dini wa Uganda huko eneo la Namugongo, nje kidogo ya jiji la Kampala
(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2010

    It is all non-sense; the guy is dead, it's up to his soul and his God according to what he did before his death. Praying for him may be wastage of time. Declaring him a Saint won't make him one, if he never was, and vice versa. The best we can do is to learn from all good things he did while ignoring the bad things.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2010

    m7 baba shavu limeng'aa,
    hongera mama mpendwa mama Maria, looking good always.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2010

    Mi naona kama sio haki vile, kwa wema gani aloufanya nyerere wa kuwa mtakatifu, umaskini huu tulokuwa nao ndo sababu yake yeye, nchi ilikwisha mshinda ndo akambwagia mzigo mwinyi... Aliifanya Tanzania kuwa kama ni yake, watu wangapi wametaifishwa mali zao kwa kisiningizio cha Azimio la Arusha? kaacha nchi yenye elimu duni ukilinganisha na majirani zetu, nadhani hii sio sahihi, mambo mengine hayaelekei.. Jamani kweli Binaadamu anapewa utukufu na Binaadamu wezake... Utukufu upo kwa Mungu tu pekeyake achana siasa zenu hizo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2010

    Kwenye hiyo picha ya chini hapo naona kama sijaelewa meno ya juu ya JK...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2010

    MIE SISEMI KITU KATIKA HILI,NI VIZURI WAMEAMUA KUMTANGAZA NYERERE KUWA MTAKATIFU,HII ITAKIFANYA KIZAZI CHA LEO AMBACHO KIMEZALIWA NA KUKUTA MAJINA MENGIIII YA WATAKATIFU .WATU WAMEKUWA WAKIOMBA KUPITIA HAO WANAOITWA WATAKATIFU,SASA WATAJUA HAO WATAKATIFU WALIISHIJE NA WALIPATIKANA JE.MENGI ATAONGEA MTIKIRA MAANA ANAJUA KUONGEA ZAIDI YANGU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...