Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein kulia na Waziri Mkuu wa Mheshimiwa Mizengo Pinda kulia, wakizungumza jambo katika kikao cha Kamati ya pamoja kinachojadili mambo mbalimbali ya kero za Muungano, kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Salama Hall Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk Ali Mohamed Shein katikati, Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda kulia na Waziri kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha kushoto, wakipitia ajenda mbalimbali kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati ya pamoja kinachojadili mambo mbaliom,bali ya kero za Muungano, kilichofanyika leo kwenye ukumbni wa Salama Hall ukumbi wa Bwawani mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya kikao kinachojadili mambo mbalimbali ya kero za Muungano, kulia Naibu Waziri wa Miundombinu Mhe.Maua Daftari, Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Mhe. Philip Marmo, Waziri wa Ulinzi Mhe. Hussein Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe. Mohamed Seif Hatib, wakipitia Agenda mbalimbali kabla ya kuanza kwa kikao hicho leo katika ukumbi wa Salama Hall ukumbi wa Bwawani mjini Zanziabar.
(picha na Amour Nassor wa VPO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2010

    Tusipoangalia huu Muungano unaweza ukawa ni mzigo....Vikao kama hivi, mimi ninavyojua ni gharama kubwa sana (gharama halisi, gharama hewa etc) kama kila siku kunakuwa na vikao kujadili kero za muungano maana yake ni kwamba muundo au muungano wenyewe ni kero na kwa nini usivunjwe!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2010

    haya tena wazanzibari kama wanaume kweli semeni matatizo yenu,sio mnakaa mnalia kwenye majukwaa,kazi kwenu sasa

    ReplyDelete
  3. tume kuweni makini mno katika kutatua hizo kero .maana yawafaa mufahamu kuwa wazanzibari hawataki muungano wenu feki!

    so tambuweni kuwa hapa hakuna ujanja wa kiini macho.wazanzibari wako macho.

    kama watanganyika mnataka muungano basi mufanye mambo kitaalamu ,kwa misingi ya haki na uwazi la sivyo BAI BAI MUUNGANO FEKI maana kiboko ya muungano feki ni serikali ya mseto zanzibari ambayo tayari imeshawadia.

    kazi kwenu kina pinda sasa maana wazanibari wapo tayari kwa mbivu ama mbichi.

    uamuzi wa watanganyika kuja ZANZIBAR kwa viza kama waendapo Dubai ni wako pinda na wenzio.


    hahahahahahahahah!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2010

    Mdau unaitaji kufanya spelling check kwenye bahazi ya aticles zako.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2010

    Wewe mpumbavu unayejiita Seedof nanai huku bara kakwambia anataka hilo limungangano ? Kwa taalifa yenu sisi hata leo ukivunjika hatutapata shida, shida mtapata nyie huko. Chakula chenyewe mnashindwa kujitosheleza. Halo Mhando wa Tanesco hebu wakatie umeme kwanza haao majuha.

    ReplyDelete
  6. Yani wazanzibari kweli bado, yani kikao kikubwa kama hicho mnawapa waheshimiwa maji ya drop yasiyokuwa na kiwango hata kidogo, no wonder wengi wameyasusia maana glass zimepinduliwa!! waziri mkuu kayakacha ameamua kuagiza kilimanjaro. halafu eti hamtaki muungano? wakati hata maji ya kunywa yenye ubora mnashindwa kutengeneza, mna-import!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2010

    KWANI TATIZO LA KUNGANGANIA NINI WAZANZIBARI WASHAJUA WATAPATA TABU UKIVUNJWA SASA SI MUWAACHIE TU NA TABU ZAO? AU KUNA SIRI GANI? KAMA MAFUTA HATA BARA YASHAGUNDULIWA,MADINI KIBAO SASA TATIZO NININI? AU MAREKANI ANA WASI WASI KUTAKUWA NA UJAHIDINA VISIWANI WAKIJITEGEMEA? HEBU TUWACHIENI JAMANI TUPATE ANGALAU VISA FREE EUROPEEE

    ReplyDelete
  8. siku zote ukiongelea matatizo ya muungano,watanganyika wanakuja juu na kijisababu chao eti muungano ukivunjika wazanzibari watapata tabu!!! pumbavu nyinyi.

    dunia inafahamu jinsi muungano huu unavyoendeshwa kimabavu na majirani zetu wa tanga-nyika.

    zanzibar na wazanzibar hawautaki huu muuitao muungano.

    tunaanza na kura ya maoni kwa serikali ya mseto then tunamalizia kura ya maoni juu ya muungano.
    watanga-nyika wasio na pasi za kusafiria wafanye hivyo haraka maana utakubidini muingie zanzibar (dubai ya africa) kwa viza.

    dunia inafahamu juu ya ujuha wa watanganyika.nchi yao ina kila aina ya utajiri wa kuifanya nchi na wananchi wake wawe matajiri lakini wapiiii?
    mahahabu.maalmasi,urenium,bahari,misitu,ardhi bora kwa kilimo,lakini hakuna lolote mlonalo!
    leo hii tanga-nyika inaendeshwa kwa misaada(pumbavu)

    ni kweli zanzibar maisha magumu,lakini muungano unazidisha ugumu wa maisha hapa visiwani.
    hatuna madini,gesi wala mafuta lakini tukiwa huru tutaendesha maisha yetu kama kawa vileeee.
    nimefurahi majuzi nilipomuona mengi akisisitiza tanzania isipunguziwe misaada!!

    pengine nchi ina laana hii tujitizame tulikotokaa.......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...