Mama Dora Kaseko Mpangile
Kwa wana blogu ya jamii salaam.

Naitwa Dora Kaseko Mpangile, nagombea udiwani Kata ya Kiwanja cha Ndege Morogoro CCM viti maalum. Lengo langu ni kushirikiana, elimishana, wezeshana, na kusaidiana katika kuhamasisha kinamama/dada kujikwamua toka katika hali duni na kujiendeleza kufikia viwango vinavyokubalika duniani.

Tunaweza kusema haya ni malengo makubwa sana, la hasha, kama watu wawili kati ya kumi wakifikia malengo haya basi hao wawili hawanabudi kuwawezesha wengine wanne na mwishowe taratibu tunafikia lengo letu.

Basi, kwanza nawashukuru na ninaomba maoni yenu na michango yenu ya hali na mali katika kutimiza lengo hili.

Unaweza kuwasiliana nami kwa e-mail ifuatayo dorampangile@yahoo.com na pia niko kwenye facebook - Dora Mpangile- hapo tutaweza kuwasiliana vema.

Asanteni sana wanablogu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mkata IssueJune 21, 2010

    Photoshop au?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2010

    Mama, mimi niko NYUMA yako. Lakini niahidi MSHIKO!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2010

    Ok.......what is your VISION?

    Mbije,A

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2010

    kwa nini usijiamini ukagombee kwenye kata. Why viti maalum bibi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2010

    Safi sana mama Mpangile, ila ungegombea viti halisi, sio hivi vya kupewa (maalum).
    Ila hata hivyo naomba nikupe sapoti ya nguvu.
    Nitakuchapishia fulana za kampeni.

    Mdau wa Mwenge - Dar

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2010

    Mdau Mbije,

    "VISION" nenda kwenye facebook Dora Mpangile hapo utapata jibu la swali lako natumaini kwa kufupi hapo juu pia nimeandika.

    Asante.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2010

    Nashukuru kwa mchango wenu wanangu wote na wanablogu ya jamii mmoja wetu akishinda wote tumeshinda na huu ndio msimamo wetu.

    Taratibu ndio mwendo tunaanza na huku mbali na kujifunza na taratibu kwa msaada wenu tutajikuta kukiendelea mbele hatua moja kwa kila muda.

    Asanteni.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2010

    Mimi nakufagilia sana Mama Mpangile, isipokuwa kitu kidogo samahani kama nitakuudhi.
    Make up yako ni almost caking na haiba yako japo nzuri overmake up inaharibu kidogo.
    Ukiondoa hayo yote mimi nakupa kura ya ndiyo!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 21, 2010

    BONGE LA SMILLING FACE

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 21, 2010

    michuzi acha kubana niachie haki yangu ya kuongea mi nasema sorry bibi kura yangu kwa vijana !!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2010

    Duh!, haya kila la kheri. Ila ange.. aaakh basi najua 90% ya ninayotaka kuyaandika yatafanya mtu flani animinye

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 22, 2010

    Nashukuru wanablogu wa jamii kwa pale tunapo kubaliana na kupishana, hii ndio demokrasia tuna uhuru wa kutoa maoni yetu hata yakiwa yanapingana.

    Kuwajibika ni kuwajibika iwe kwa kuchaguliwa,kuteuliwa, au kujiari, binafsi naamini matunda ya kazi yatapimika tu kwa kila tendo/jambo kuna matokeo.

    Naamini demokrasia ni kwa wakubwa na wadogo. Katika majukwaa ya siasa kuna umri unaohitajika basi kwa maoni yangu vijana na wazee tujiunge pamoja kufikia viwango vya demokrasia na maendeleo yanayokubalika katika uwanja wa kimataifa.

    Asanteni.

    Dora Mpangile

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...