pichani baadhi ya warembo hao wakitambulishwa mbele ya waandishi wa habari, dada aliyekaa ni mratibu wa shindano hilo Cathelini John.


Kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Dar City Centre 2010, kinatalajia kufanyika Juni 5 kwenye Hotel ya Moven pick jijini Dar es Salaam, huku mrembo wa kwanza wa shindano hilo akinyakua kiasi cha shilingi Milioni moja(1000000) na wapili laki saba(700000) na wa tatu akinyakua kiasi cha laki tano(500000)

Mbali na zawdi hizo kwa washindi hao, pia zawadi kwa mshindi waliobaki wataondoka na kifuta jasho cha shilingi 100000(laki moja moja0.

Katika shindano hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Millennium promoters, kundi la Machozi Band, sambamba na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ pamoja na Chege anayetamba na nyimbo ya ‘Mkono mmoja weka juu” watapagawisha mashabiki watajkaojitokeza kuangalia warembo hao.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Fortunatus Faustine, akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwatambulisha warembo hao mbele ya waandishi wa habari, ilipofanyika katika Ukumbi wa Savanna Lounge uliopo katika Hotel hiyo Paradise City Centre.(Posta Mpya).

Katika shindano hilo ambalo linatalajia kuanza majira ya jioni saa mbili usiku.Walitaja viingilio vya shindano hilo kuwa ni kiasi cha shilingi 25,000, kwa muda wa kawaida na getini itakuwa ni shilingi 30,000.mbali na hilo pia kwa upande wa VIP ambapo itakuwa pamoja na chakula cha usiku, ni shilingi 50,000.

Kwa Upande wake mratibu wa kituo hicho cha Dar City Centre, Cathelini John, alisema kuwa tiketi za shimndano hilo zimeanza kuuzwa katika sehemu za; Best Bite-Namanga, Savannah Lounge, Movenpick- Gift Shop, Chiken Hut-MIlimani City, Rose Garden -Pub, Best Bite -Namanga.

Pia Cathelini alisema kuwa warembo hao ammbao mpaka sasa wanajifua katika hotel ya Lamada chini ya aliyekuwa miss Tabata pia alishiriki shindano la Miss Tanzania , Flora Florence(22).

Aliwataja baadhi ya warembo hao kuwa ni pamoja na Glory Mosha (20), Agness Francice (20), Bahati Chande (20), Kiren Mohammed (20), Sara Nasoro (20), Suraina Merwiro (23), Neena Jackob (2o), Neema Alen (18), Mariam Hassan (19), Sara Said (20), Nance Mane (20) na Anabela Isaya(21).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2010

    haya nayo hayaeshi jamani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2010

    Kaka Michu naomba kuuliza. Hivi hawa warembo hawana kazi nyingine? Kila siku kuna Miss huyu, miss yule! Kha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...