Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EML Francis Anthony Ciza Majey akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa Club maisha mapema leo
asubuhi,shoto ni meneja wa club hiyo Allan Ngugi
Moja ya sehemu mbili za Ma DJ
Kila sehemu kumetakata
Mlango wa kuingilia New Maisha Club iliyoko Oysterbay jijini Dar umewekwa 'ChwiChwiChwi' (metal detector) kujihami na uingiaji na silaha ama chuma
New Maisha Club kwa nje. Bwawa la kuogelea halipo tena hapo mbele
sehemu ya juu ndani ya New Maisha Club



Sehemu ya ndani



ukumbi wa kusakatia libeneke. New Maisha Club iliyokuwa Maisha Club kabla ya kuteketea kwa moto mnamo Novemba 8 mwaka jana inafungua milango kwa wadau kuanzia kesho ambapo sherehe ya uzinduzi kukata na shoka inaandaliwa. Kwa wale ambao hawakuona habari ya awali ya kuungua kwa Maisha club ama wanaotaka kujikumbushia:


UKUMBI maarufu wa starehe wa Club Maisha unatarajiwa kufunguliwa upya Juni 24 mwaka huu, baada ya kufanyiwa ujenzi mkubwa kutokana na kuungua moto mwaka jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey), alisema klabu hiyo imefanyiwa ubunifu mkubwa ili kukonga nyoyo kwa kutoa burudani murua na ya uhakika kwa wateja wake.

“Club Maisha inakuja katika mtazamo mpya kwa kutoa burudani za usiku Dar es Salaam iliyopambwa vizuri, sauti ya kutosha na inaipeleka Tanzania mbele katika kutoa burudani za usiku.

“Baada ya miezi kadhaa wateja wetu kukosa burudani, klabu yao sasa inarudi ikiwa ni ya kisasa zaidi yenye televisheni 32 zitakazokuwa zikionesha fainali za Kombe la Dunia na video za muziki, sehemu mbili za kuchezea, vyumba viwili maalumu vya VIP, hii yote ni katika kuuweka kuwa ya kisasa,” alisema Majey.

Vitu vingine vilivyopo katika Club Maisha ni pamoja na sehemu za kuvutia sigara, varanda ya juu, sehemu saba (7) za baa, jiko na TV kubwa inayoonesha fainali za Kombe la Dunia na michezo mingine kwa nje.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema siku itakayofunguliwa Club Maisha itakolezwa na kusisimuliwa na baadhi ya wachezeshaji muziki (ma-DJ) kutoka Afrika Mashariki na Marekani ambao watapiga nyimbo kali zinazotesa kwa sasa duniani.

“Klabu tayari imekaguliwa na mainjinia kutoka Idara ya Zimamoto pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha hakuna ajali ya moto inayoweza kutokea tena, na milango ya dharura imeongezwa ili kuhakikisha usalama mkubwa unakuwepo,” alisema Majey.

“Tumewekeza vya kutosha ili kuirejesha Club Maisha katika nafasi yake ya ubora kwa klabu za usiku Tanzani, tumeweka staili za kisasa kwa lengo la kutoa burudani iliyotakata kwa wapenda burudani za usiku,” alisema.

Viingilio vitabaki kuwa vya kawaida ambavyo
ni sh. 10,000 sehemu ya kawaida na sh. 20,000 kwa VIP.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2010

    Du Tsh. 10,000/= Kiingilio cha kwenye starehe tu ya disco wakati mshahara wangu ni 300,000 kwa mwezi.

    Ebu mfikirie tena vyema.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2010

    Swadakta! Maelezo yamenitosheleza sina swali, hivyo hiyo tarehe 24 nitaingia viwanja.

    Mdau
    Tantin

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2010

    Club inaonekana imejengwa upya na ni nzuri sana lakini baada ya huo umo je walivyoijenga upya wameijenga kwa utaalamu mpya wa kutumia vifaa mbalimbali vya kukinga, kuzuia ama kupunguza madhara ya moto na tungeomba tuonyeshwe hizo emergency doors...na kama wameweka fire alarms, fire sprinkler protection systems etc etc

    Hapo juu ningekua so excited kama ungenionyesha mambo hayo ya kujiepusha na moto kuliko kunionyesha metal detecting doors..Huo mlango moto ukitokea tena sidhani kama utaniokoa maisha yangu...

    Tulikua na rafiki yangu kwenye club moja [jina nalihifadhi] hapo Dar mwezi wa 12 mwaka jana alikua anashangaa sana tumilango tulivyo tudogo, hakuna alama za kuonyesha milango ya kutoka wakati wa hatari na air ventilation ilikua ndogo sana usiku huo kulingana na watu tuliokua humo ndani. Yaani unasikia harufu za kila aina sigara, perfumes, vikwapa etc etc...

    Tunatakiwa tujifunze sana kutoka kwa wenzetu ambao siku hizi wana night club builing codes sidhani kuwa nchi yetu inayo hii ukizingatia night clubs kila siku zinafunguliwa hata kwenye residential areas

    Wenye clubs wangejitahidi kuzingatia haya na sio kusubiri mpaka Govt ilazimishe au watu wapoteze maisha yao wakati watu walichofuata kwenye hizo clubs is just to have funny and not to sell their lives...

    Au na sisi mpaka tuingie kwenye hii record? ..

    Quezon City night club fire killed 162 people in 1996

    Rhode island night club fire killed 100 people in 2003

    Buenos Aires night club fire killed 194 people in 2004

    Shenzhen night club fire killed 43 people in 2008

    Thailand night club fire killed 66 people in 2009

    Moscow night club fire killed 109 people in 2009

    I can go on and on and on.....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2010

    Club Maisha,

    Mtakuwa mnapiga nyimbo za aina gani? Lingala au ndio yatakuwa mambo ya ma-hip hop?

    Au ukumbi mmoja Lingala na mwingine Hip Hop?

    Na huko VIP zinapigwa nyimbo za aina gani?

    Maana Bongo hamna sehemu ya maana inayopiga nyimbo za 'watu wazima' (Lingala, Zouk, nyimbo za hapa home za bendi n.k)ambao wengi wao (watu wazima)ndio wenye pesa zao. Kumbi karibia zote za maana zime-base kwa madenti tu.

    Hizo kumbi ni 'Sound Proof'?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2010

    HII MAISHA CLUB IPO WAPI JAMANI? INAONEKANA NI CLUB NZURI.

    MDAU HAPO JUU UNASEMA UKWELI HATA WAZEE WANAPENDA BURUDANI KWA HIYO
    MMILIKI FANYA UTARATIBU WA KUWAPA KITU WANAPENDA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2010

    Kiingilio 20,000 VIP, na vinywaji bei gani??

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2010

    ukilipa twenty vinywaji bure

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2010

    Endeleeeni ku-MAISHIKA,mi na make money tu hapa.
    Mdau Mbije,A

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 24, 2010

    maisha club iko oysterbay, karibu hotel

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...