
asubuhi,shoto ni meneja wa club hiyo Allan Ngugi


UKUMBI maarufu wa starehe wa Club Maisha unatarajiwa kufunguliwa upya Juni 24 mwaka huu, baada ya kufanyiwa ujenzi mkubwa kutokana na kuungua moto mwaka jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey), alisema klabu hiyo imefanyiwa ubunifu mkubwa ili kukonga nyoyo kwa kutoa burudani murua na ya uhakika kwa wateja wake.
“Club Maisha inakuja katika mtazamo mpya kwa kutoa burudani za usiku Dar es Salaam iliyopambwa vizuri, sauti ya kutosha na inaipeleka Tanzania mbele katika kutoa burudani za usiku.
“Baada ya miezi kadhaa wateja wetu kukosa burudani, klabu yao sasa inarudi ikiwa ni ya kisasa zaidi yenye televisheni 32 zitakazokuwa zikionesha fainali za Kombe la Dunia na video za muziki, sehemu mbili za kuchezea, vyumba viwili maalumu vya VIP, hii yote ni katika kuuweka kuwa ya kisasa,” alisema Majey.
Vitu vingine vilivyopo katika Club Maisha ni pamoja na sehemu za kuvutia sigara, varanda ya juu, sehemu saba (7) za baa, jiko na TV kubwa inayoonesha fainali za Kombe la Dunia na michezo mingine kwa nje.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema siku itakayofunguliwa Club Maisha itakolezwa na kusisimuliwa na baadhi ya wachezeshaji muziki (ma-DJ) kutoka Afrika Mashariki na Marekani ambao watapiga nyimbo kali zinazotesa kwa sasa duniani.
“Klabu tayari imekaguliwa na mainjinia kutoka Idara ya Zimamoto pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha hakuna ajali ya moto inayoweza kutokea tena, na milango ya dharura imeongezwa ili kuhakikisha usalama mkubwa unakuwepo,” alisema Majey.
“Tumewekeza vya kutosha ili kuirejesha Club Maisha katika nafasi yake ya ubora kwa klabu za usiku Tanzani, tumeweka staili za kisasa kwa lengo la kutoa burudani iliyotakata kwa wapenda burudani za usiku,” alisema.
Viingilio vitabaki kuwa vya kawaida ambavyo
ni sh. 10,000 sehemu ya kawaida na sh. 20,000 kwa VIP.
Du Tsh. 10,000/= Kiingilio cha kwenye starehe tu ya disco wakati mshahara wangu ni 300,000 kwa mwezi.
ReplyDeleteEbu mfikirie tena vyema.
Swadakta! Maelezo yamenitosheleza sina swali, hivyo hiyo tarehe 24 nitaingia viwanja.
ReplyDeleteMdau
Tantin
Club inaonekana imejengwa upya na ni nzuri sana lakini baada ya huo umo je walivyoijenga upya wameijenga kwa utaalamu mpya wa kutumia vifaa mbalimbali vya kukinga, kuzuia ama kupunguza madhara ya moto na tungeomba tuonyeshwe hizo emergency doors...na kama wameweka fire alarms, fire sprinkler protection systems etc etc
ReplyDeleteHapo juu ningekua so excited kama ungenionyesha mambo hayo ya kujiepusha na moto kuliko kunionyesha metal detecting doors..Huo mlango moto ukitokea tena sidhani kama utaniokoa maisha yangu...
Tulikua na rafiki yangu kwenye club moja [jina nalihifadhi] hapo Dar mwezi wa 12 mwaka jana alikua anashangaa sana tumilango tulivyo tudogo, hakuna alama za kuonyesha milango ya kutoka wakati wa hatari na air ventilation ilikua ndogo sana usiku huo kulingana na watu tuliokua humo ndani. Yaani unasikia harufu za kila aina sigara, perfumes, vikwapa etc etc...
Tunatakiwa tujifunze sana kutoka kwa wenzetu ambao siku hizi wana night club builing codes sidhani kuwa nchi yetu inayo hii ukizingatia night clubs kila siku zinafunguliwa hata kwenye residential areas
Wenye clubs wangejitahidi kuzingatia haya na sio kusubiri mpaka Govt ilazimishe au watu wapoteze maisha yao wakati watu walichofuata kwenye hizo clubs is just to have funny and not to sell their lives...
Au na sisi mpaka tuingie kwenye hii record? ..
Quezon City night club fire killed 162 people in 1996
Rhode island night club fire killed 100 people in 2003
Buenos Aires night club fire killed 194 people in 2004
Shenzhen night club fire killed 43 people in 2008
Thailand night club fire killed 66 people in 2009
Moscow night club fire killed 109 people in 2009
I can go on and on and on.....
Club Maisha,
ReplyDeleteMtakuwa mnapiga nyimbo za aina gani? Lingala au ndio yatakuwa mambo ya ma-hip hop?
Au ukumbi mmoja Lingala na mwingine Hip Hop?
Na huko VIP zinapigwa nyimbo za aina gani?
Maana Bongo hamna sehemu ya maana inayopiga nyimbo za 'watu wazima' (Lingala, Zouk, nyimbo za hapa home za bendi n.k)ambao wengi wao (watu wazima)ndio wenye pesa zao. Kumbi karibia zote za maana zime-base kwa madenti tu.
Hizo kumbi ni 'Sound Proof'?
HII MAISHA CLUB IPO WAPI JAMANI? INAONEKANA NI CLUB NZURI.
ReplyDeleteMDAU HAPO JUU UNASEMA UKWELI HATA WAZEE WANAPENDA BURUDANI KWA HIYO
MMILIKI FANYA UTARATIBU WA KUWAPA KITU WANAPENDA.
Kiingilio 20,000 VIP, na vinywaji bei gani??
ReplyDeleteukilipa twenty vinywaji bure
ReplyDeleteEndeleeeni ku-MAISHIKA,mi na make money tu hapa.
ReplyDeleteMdau Mbije,A
maisha club iko oysterbay, karibu hotel
ReplyDelete