Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano wa Shirika la Ndege la Oman Air, Philippe Georgious, akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini jana juu ya kuanza upya kwa safari za ndege za shirika la Oman Air, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa shirika hilo,Mohammed Mubarak Al- Shikely,kulia ni Ejaz Khan Meneja wa Ukanda wa Afrika na Uarabuni.

Kuanzia sasa Oman Air itaanza safari
zake mfululizo kati ya miji ya muscat na Dar-es-salaam.

Safari hizo Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muscat kila siku ya jumamosi, Jumatatu na Jumatano kwa wiki, Ndege Zitakazo geuza kurudi Muscat Zitaanzia safari katika kiwanja cha kimataifa cha Julius Nyerere, Dar-es-salaam na kupitia vituo vingine kuelekea Muscat.
Oman Air inaruka katika vituo 38 Duniani.

Mkurugenzi mtendaji wa Oman Air, Peter Hill Anasema: “Oman Air imedhamiria kupanua zaidi wigo wake wa kibiashara kwa kuiongezea Dar es Salaam kwenye safari zake na tumelifanyia kazi hili kwa bidii bila kuchoka ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu.

Mkurugenzi huyo anasema ‘‘ Tukiwa na historia nzuri ya siku nyingi ya kibiashara baina ya Tanzania na Oman tuna uhakika mkubwa sana wa kuendelea kujenga na kuendeleza uhusiano huu wa nchi hizi mbili kupitia huduma zetu za oman Air.

Anasema ikijulikana kwa vivutio vyake vya asili, Dar-es-salaam inatazamiwa kuwa na umaarufu wasafari za kitalii zaidi kutoka duniani kote kulingana na thamani yake, Pia kama sehemu maalum ya kufurahia mapumziko ya likizo kubwa za mwaka.

Huduma zetu katika nchi yenye mvuto wa kipekee zitaambatana na wasafiri wenye kutambua vitu vizuri na wenye uchaguzi mzuri wan chi nzuri za kitalii kama Tanzania.

Dar es salaam ndio mji mkubwa zaidi wa kibiashara katika Tanzania ndiyo maana tunaiunganisha Dar es salaam na Dunia.

Anafafanua kwamba ukiwekwa kama mji wa kitalii na njia kuu ya watalii wanaopitia kwenda kupata mapumziko katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Zanzibar tunaamini kwamba tutakua sehemu ya kukuza utalii katika Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kaka michuzi.
    habari za kuamka hapo bongo!

    michuzi hizi huduma zinazotolewa na waomani zilikuwepo hapa kwetu ZANZIBAR kwa miaka mingi tu.

    wazanzibari tulikuwa tukifaidi huduma hizi za ndege kutoka oman na kuja direct zanzibar.lakini ilipoonekama midege inajazana kuingia zanzibari na wazanzibari wananufaika basi hapo panga la moto la kuzikata hizi safari lilipita.kwa kisingizio kuwa uwanja wa ndege wa zanzibari ni mbovu!

    Binafsi naiona hii hatuwa iliyochukuliwa na tanga-nyika ni ya kiufisadi tu(ujanja) maana wanajuwa kuwa zenji uwanja unajengwa na utakapokamilika midoge kutoka omani haitosita kutinga visiwani.

    binafsi naungana na wazanzibari wenzangu wanaoamua kuchukuwa ndege kokote kule duniani hadi kenya na kutoka kenya kutinga zenj.no! no! bara

    hapo kambalage nyelele katu hawatopata hela yangu ya ushuru.

    msemo niOMAN-KENYA-ZANZIBAR

    TEHETEHETEHETEHE!

    ReplyDelete
  2. Mume Wangu, safarini canadaJune 04, 2010

    Sedouf, mtoa maoni wa kwanza acha ubinafsi na ubaguzi. Nchi yetu haina dini, rangi wala kabila na sijui wewe umeyatoa wapi hayo malalamiko ya kipuuzi, nyambafffff!!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2010

    Sedouf,

    Wacha jazba. Toa hoja zenye tija. Vinginevyo tafuta vitu vya maana zaidi vya kufanya katika kuutumia muda wako.

    Binasfi kwangu wewe ni kero tu. Maongezi yako yote ni jazba jazba tu.

    Watu wanalenga mambo ya umoja na maendeleo, na sio kuzidisha mifarakano na migawanyiko katika jamii.

    Kuna ile mtu kuongea kijazba kwa utani, sawa? Ile rukhsa. Ila wewe nimekusoma kuwa upo serious na hizo jazba zako.

    Ukimeza, ukitema, shauri yako, ila kwa manufaa yako, ningekushauri umeze; hata kama utasema havinihusu kukwambia kitu.

    Habari ndio hiyo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2010

    Sedouf maneno yako hayafanani na jina lako. Shame on you! Wewe unafanya maamuzi kutokana na umbeya tu na sio ukweli na facts findings. Lione vile...

    ReplyDelete
  5. Daima unapojaribu kuongelea kuminywa kwa ZANZIBAR HAKI ZAKE ZA MSINGI watanga-nyika hukujia juu ili kukunyamazisha.

    Jamani huu ni ulimwengu wa uwazi ,watanga-nyika msiogope ukweli.na kumbukeni hiyo kutofautiana kimawazo ni ishara ya kukuwa demokrasia.

    ZANZIBAR ya leo sio ile iliyochukuliwa kimabavu na nyelele.wazanzibari sasa wana upeo mkubwa sana katika kufahamu haki zao.

    WAZANZIBARI tusisite kuupinga udhalimu dhidi ya nchi yetu kiuchumi,kisiasa na kijamii unaofanywa na jirani zetu wa tanga-nyika.

    vijana wa kizanzibari njia ni hiyo hiyo tu NCHI ZA NJE ---KENYA---ZENJ.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...