Kuanzia sasa Oman Air itaanza safari
zake mfululizo kati ya miji ya muscat na Dar-es-salaam.
Safari hizo Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muscat kila siku ya jumamosi, Jumatatu na Jumatano kwa wiki, Ndege Zitakazo geuza kurudi Muscat Zitaanzia safari katika kiwanja cha kimataifa cha Julius Nyerere, Dar-es-salaam na kupitia vituo vingine kuelekea Muscat.
Oman Air inaruka katika vituo 38 Duniani.
Mkurugenzi mtendaji wa Oman Air, Peter Hill Anasema: “Oman Air imedhamiria kupanua zaidi wigo wake wa kibiashara kwa kuiongezea Dar es Salaam kwenye safari zake na tumelifanyia kazi hili kwa bidii bila kuchoka ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu.
Mkurugenzi huyo anasema ‘‘ Tukiwa na historia nzuri ya siku nyingi ya kibiashara baina ya Tanzania na Oman tuna uhakika mkubwa sana wa kuendelea kujenga na kuendeleza uhusiano huu wa nchi hizi mbili kupitia huduma zetu za oman Air.
Anasema ikijulikana kwa vivutio vyake vya asili, Dar-es-salaam inatazamiwa kuwa na umaarufu wasafari za kitalii zaidi kutoka duniani kote kulingana na thamani yake, Pia kama sehemu maalum ya kufurahia mapumziko ya likizo kubwa za mwaka.
Huduma zetu katika nchi yenye mvuto wa kipekee zitaambatana na wasafiri wenye kutambua vitu vizuri na wenye uchaguzi mzuri wan chi nzuri za kitalii kama Tanzania.
Dar es salaam ndio mji mkubwa zaidi wa kibiashara katika Tanzania ndiyo maana tunaiunganisha Dar es salaam na Dunia.
Anafafanua kwamba ukiwekwa kama mji wa kitalii na njia kuu ya watalii wanaopitia kwenda kupata mapumziko katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Zanzibar tunaamini kwamba tutakua sehemu ya kukuza utalii katika Tanzania.
Kaka michuzi.
ReplyDeletehabari za kuamka hapo bongo!
michuzi hizi huduma zinazotolewa na waomani zilikuwepo hapa kwetu ZANZIBAR kwa miaka mingi tu.
wazanzibari tulikuwa tukifaidi huduma hizi za ndege kutoka oman na kuja direct zanzibar.lakini ilipoonekama midege inajazana kuingia zanzibari na wazanzibari wananufaika basi hapo panga la moto la kuzikata hizi safari lilipita.kwa kisingizio kuwa uwanja wa ndege wa zanzibari ni mbovu!
Binafsi naiona hii hatuwa iliyochukuliwa na tanga-nyika ni ya kiufisadi tu(ujanja) maana wanajuwa kuwa zenji uwanja unajengwa na utakapokamilika midoge kutoka omani haitosita kutinga visiwani.
binafsi naungana na wazanzibari wenzangu wanaoamua kuchukuwa ndege kokote kule duniani hadi kenya na kutoka kenya kutinga zenj.no! no! bara
hapo kambalage nyelele katu hawatopata hela yangu ya ushuru.
msemo niOMAN-KENYA-ZANZIBAR
TEHETEHETEHETEHE!
Sedouf, mtoa maoni wa kwanza acha ubinafsi na ubaguzi. Nchi yetu haina dini, rangi wala kabila na sijui wewe umeyatoa wapi hayo malalamiko ya kipuuzi, nyambafffff!!!!!!
ReplyDeleteSedouf,
ReplyDeleteWacha jazba. Toa hoja zenye tija. Vinginevyo tafuta vitu vya maana zaidi vya kufanya katika kuutumia muda wako.
Binasfi kwangu wewe ni kero tu. Maongezi yako yote ni jazba jazba tu.
Watu wanalenga mambo ya umoja na maendeleo, na sio kuzidisha mifarakano na migawanyiko katika jamii.
Kuna ile mtu kuongea kijazba kwa utani, sawa? Ile rukhsa. Ila wewe nimekusoma kuwa upo serious na hizo jazba zako.
Ukimeza, ukitema, shauri yako, ila kwa manufaa yako, ningekushauri umeze; hata kama utasema havinihusu kukwambia kitu.
Habari ndio hiyo.
Sedouf maneno yako hayafanani na jina lako. Shame on you! Wewe unafanya maamuzi kutokana na umbeya tu na sio ukweli na facts findings. Lione vile...
ReplyDeleteDaima unapojaribu kuongelea kuminywa kwa ZANZIBAR HAKI ZAKE ZA MSINGI watanga-nyika hukujia juu ili kukunyamazisha.
ReplyDeleteJamani huu ni ulimwengu wa uwazi ,watanga-nyika msiogope ukweli.na kumbukeni hiyo kutofautiana kimawazo ni ishara ya kukuwa demokrasia.
ZANZIBAR ya leo sio ile iliyochukuliwa kimabavu na nyelele.wazanzibari sasa wana upeo mkubwa sana katika kufahamu haki zao.
WAZANZIBARI tusisite kuupinga udhalimu dhidi ya nchi yetu kiuchumi,kisiasa na kijamii unaofanywa na jirani zetu wa tanga-nyika.
vijana wa kizanzibari njia ni hiyo hiyo tu NCHI ZA NJE ---KENYA---ZENJ.