( wa pili kulia) akiwa na wenzie wa bodi ya Sauti za Busara
HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE TOKA ZENJI ZIKISEMA KWAMBA MSANII MAARUFU WA HUKO VISIWANI YUSUF AHMED ALLEY MAARUFU KAMA BWAN'CHUCHU HATUNAYE TENA. HABARI HIZO ZINASEMA BWAN'CHUCHU AMEFIA JIJINI NAIROBI, KENYA, ALIKOKUWA AMEKWENDA KIKAZI. CHANZO CHA MAUTI YAKE HATUJAAMBIWA ILA IMETHIBITISHWA KWAMBA MWILI WAKE UMESHAREJESHWA ZENJI NA MSIBA UKO KWAO SEHEMU ZA KISIMA MAJONGOO NA MAZIKO YATAFANYIKA LEO SAA 10 KWENYE MAKABURI YA MWANAKWEREKWE.
BWAN'CHUCHU ATAKUMBUKWA KWA UHODARI WAKE KATIKA MUZIKI HASA ALIPOUNDA BENDI YA CHUCHU SOUND ILIYOTAMBA SANA KWA VIBAO VYAKE VIKALI NA CHAPUO ZA MAONGEZI KATI YAKE NA OMARI MKALI YALIYOKUWA YAKIHITIMISHWA NA NENO LA 'EE! KWAHERI'.
MAREHEMU CHUCHU PIA ALIKUWA MMOJA WA WAJUMBE WA BODI YA TAMASHA LA KILA MWAKA LA SAUTI ZA BUSARA NA PIA ALIKUWA ANAMILIKI STUDIO YA KUREKODIA MUZIKI PAMOJA NA STESHENI YA REDIO.
MOLA AIWEKE MAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU
-AMIN
Kusikia kimoja ya vibao vya Chuchu Sound BOFYA HAPA
Its a big loss...Chuchu..daima utakumbukwa na ndugu zako, marafiki zako, majirani zako na wapenzi wako wote...Nenda salama kaka..upumzike pema
ReplyDeleteInna lillahy wainna ilayhi iraji3un.
Du, tumempoteza msanii na kiongozi mzuri ktk tasnia ya burudani, tupo pamoja wafiwa na wapenzi wote wa Chuchu sound.
ReplyDeletePia sijui hiki kitu kikali cha 'Tenda Mtende Nyie' kama kilitolewa angalau DVD/Video, maana kama bado, basi Omari Mkali jaribu kuvuta majeshi mkirekodi ktk DVD/Video kumuenzi mwenzetu Bwan'Chuchu.
Mdau
Muscat. Omanni
OMG. May He Rest in Peace.
ReplyDeleteDuh, ama kweli hapa duniani tunapita tu. Yaani katutoka ghafla ghafla namna hiyo! Jamani, tuwe tayari wakati wote maana hatujui siku wala saa.
ReplyDeleteMungu akujalie pumziko jema Bwa'Chuhu! Poleni sana wana familia na wengine wote ambao mmeguswa sana na huu msiba wa ghafla!
Poleni wafiwa , mungu ailaze roho ya maremu peponi .. tumepoteza hazina kubwa katika maswala ya sanaa na habari
ReplyDeleteSisi watu wa hapa Washington state seattle tunakumiss tayari.Chuchu Mpenzi wetu,mwanetu,rafiki yetu, na kaka yetu Mungu akulaze mahala pema peponi.
ReplyDeleteWatu wengi wa zanzibar wameondokewa jana na kiumbe,alikuwa mtu wa kufurahisha watu pia ni mcheshi.Tunatoa Pole kwa Familia yake yote kuanzia Mkewe Bi Laila na wengine wote.Kutasomwa Hitma hapa Bellevue siku ya jumatatu tarehe saba juni saa kumi jioni kwenye hall la wakina shaaban Moyo nyote mnakaribishwa mliopo hapa WA.
R.I.P. CHUCHU. Tunatoa mkono wa Pole kwa familia ya Chuchu yote Hasa mkewe Bi Laila.
ReplyDeleteHapa Bellevue WA state kutasomwa Hitima jumatatu tarehe saba june,ukumbi wa Moyo saa kumi jioni Watanzania na jumuiya yote kizanzibari mnalikwa kwenye kisomo.
Tutamkumbuka chuchu kwa ucheshi wake na wema wake Mungu amlaze mahala pema.Amin.
Doh Michuzi Nuksi yaani bado unatuwekea muziki wake badala ya kumtakia maghfira.Mungu amlaze mahali pema peponi,safari yetu ni sote.Poleni sana wafiwa na mtakieni maghfira kwa sana,kama namuona vile tokea enzi hizo hadi leo
ReplyDelete