Mkurugenzi wa Mauzo wa TBL,Nik Broks (kulia) akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja wakitoa uchafu uliopo katika mtaro uliopo kando kando ya Kampuni hiyo ya Bia ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mazingira dunia iliyoadhimishwa leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia TBL,Robin Goetzsche akijumuika pamoja na wafanyakazi wake katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani.Mkurugenzi huyo alishiriki bega kwa bega na wafanyakazi wake pamoja na wakazi wa eneo hilo kuhakikisha eneo lote la jengo hilo na maeneo ya jirani yanakuwa safi.
Mkuu wa Maswala ya utawala wa TBL,Phocus Lasway (kushoto) akiwa pamoja na Meneja wa Safari Lager,Fimbo Butallah (pili kulia) pamoja na wafanyakazi wengine wa TBL wakishirikiana kufanya usafi leo ikiwa ni siku wa Mazingira Duniani.
Da' Lilian Erasmus wa TBL akikabidhi baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wa mazingira kwa Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Richard Mfugale ikiwa ni siku ya Mazingira Duniani iliyoadhimishwa leo Duniani kote.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiendelea na usafi leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2010

    Kwa kweli hali ya uchafu Dar imeshamiri mno. Sielewi imekuwaje hadi wa-Tanzania tukakumbatia kwa nguvu tabia hii.
    Inahitajika usafi ufanywe na wote siku zote na sio siku maalum tu kama hii ya mazingira duniani. Why not emulate Kagame and have at least every second weekend dedicated to usafi mtaani. Bars should be closed on those days everybody MUST be involved, with penalty to those ignoring the by-law..... au mnasemaje wadau?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2010

    This sickens me to puke, I bet it would cost them less to put a sewer system for less than what they are giving away in some other unnecessary donations. I understand the photo app they are having here for their publicity, however, they can do better than that.
    think about it!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2010

    Mfano wa kuigwa. Ila isiwe mara moja kwa mwaka.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2010

    Uongozi wa TBL unahistahili pongezi! sidhani km ishawahi kutokea Tanzania! au kwa kuwa uongozi wa juu ni wageni? wao hawaoni ajabu kujishughulisha kwa kazi za usafi, hivi ingekuwa uongozi wa juu ni wazawa! Mkurugenzi angekubali kuacha ofisi na kwenda kufanya Usafi? achia mbali Mkurugenzi! Meneja je, angekubali kwenda kufanya usafi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2010

    Mh..!! Publicity.com - Nagira A Tawn.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2010

    mnaona haya halafu mnasema mambo ya ughaibuni ya kuiga hayana maana. Hii yote ya wenzetu volunteer muhimu sana kwa taifa letu..na pia ukiona mtu akatupa uchafu okota weka mahali panapotakiwa. Sio kungojea watu waje wasafishe tu..Kila mtu akiwajibika tutafika tu..

    1. mambo ya kutema mate hovyo mwiko
    2. kutupa bazoka kila mahali mwiko
    3. kutupa takataka tu hovyo hovyo mwiko. If you see someone is doing that say something

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2010

    TBL WAMEPEWA ADHABU NDOGO SANA KWA KOSA LA KUHUJUMU SBL.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 03, 2010

    HIS MASTERS VOICE, MICHUZI STOP BEING COWERED YOU MUST RESPECT ALL PEOPLES OPINIONS NOT PRO ONLY, IT HURTS TO SEE THAT YOU ARE TRYING TO HIDE THE TRUTH TO SAVE THE MASTER. ARE THEY GIVING YOU A CUT????????

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 03, 2010

    JAMANI DAR CHAFU......!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 03, 2010

    Hii sio mazingira bali ni usafi. Tusichanganye mambo hapa. Kwanza nawaonea huruma na mabuti yao ya mvua na jua kali la bongo maana hiyo ngoma mpira kaka hiyo..
    Halafu si kazi yao na wala haisaidii chochote.

    Wapo wahusika wa kazi hii na ambao hawaifanyi wanaitwa Serikali. Ila wahangaikaji wakiweka vikapu vyao vya vitumbua Serikali hiyo ipo kuja kuwanyang'anya mali zao...wizi mtupu.

    Kama wanataka kusaidia mazingira wasitafute kupigwa picha wanaungua jua na mabuti ya mvua bali wakae na wataalam wabuni project za mazingira ambayo wataitolea hela ..mfano kuboresha bustani za mapumziko, kuboresha bonde la jangwani liwe na mvuto, livute viumbe mbalimbali na pengine kulifanya liwe green belt.
    Kwa kifupi hii ni PR tu hamna lolote!!
    Mzawa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 03, 2010

    kudadadadeki si mchezo usafi kwanza. sipati picha wakikutana na mavi ya wahindi kwenye hiyo mitaro au kwenye hizo lambo (flying toilets) zinazotumiwa na wahindi kwenye majumba ya NHC ... tehe tehe tehe!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 03, 2010

    kidumu chama cha mafukara.... Watanzania usafi kwetu ni kama donda ndugu kwani laiti kama tungelikuwa tuna AIBU japo 1/10 basi mambo kama haya yangelitoweka enzi zile za ujima....... kweli RAIS na Wenzi wake tunao na wadanganyika sie tusivyoweza kujiuliza maendeleo ni nini kweli hii ni AIBU KWA KILA MTANZANIA.... Kama mnakumbuka ile hadithi ya ...'afadhali yangu sijasema ....' basi nami nasema "afadhali niliwahi kukumbia hiyo nchi" kwani kuanzia Viongozi hadi wananchi wanaowachagua kila siku ni vichwa vya wendawazimu kwani mpaka kesho sielewi kwanini hawawaulizi viongozi wao ni niniwameifanyia nchi yao tokea miaka 35 iliyopita ikiwa bado mji mashuhuri kama DAR kuna nyumba za udongo na uchafu unaozidi umri baadhi ya wanablog hii....AIBU AIBU
    Mdau, Cleveland,oh

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2010

    Uchafu kando kando ya TBL???? Si ni wajibu wenu kuhakikisha kuwa ni pasafi kila leo???? Mnasubiri pachafuke weee ndio mjipachike katika siku ya mazingira???? Mfano mliopaswa kuuonesha ni kwamba siku ya mazingira imewakuta mkiwa wasafi, na sio siku ya kusafisha. Hivyo mlipaswa kwenda kusafisha sehemu nyingine ambayo ni public (zaidi), kama vile kufyeka nyasi Muhimbili, kurekebisha mazingira ya mashuleni n.k. Mnisamehe, ila kwa kweli naona mmejidhalilisha tu i.e. siku ya mazingira imewa-expose badala ya nyie kui-expose kwa jamii na kuchochea tabia ya usafi mara kwa mara. Hiyo ingewapa PR ya nguvu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...