UKIJANI WA JIJI LA DAR ES SALAAM


Wakati tukiwa ktk jitiahada za kupendezesha jiji letu inabidi vilevile tuwe wabunifu,ufahamu wa mambo mbalimbali tunayoyafanya.Mfano ni hili suala la kupanda miti aina ya Palms pembezoni na katikati ya barabara zetu !

Pamoja na maua,vichaka .Palms ziko za aina mbalimbali na pia zina nafasi yake kwa matumizi yake tokana na sehemu itakayopandwa,zina ukubwa tofati na pia zina tabia tofauti ,zingine zina weza stawi kwenye jua kali na upepo,zingine kwenye kivuli na pasipo na upepo. Hali kadhalika miti ya kivuli,vichaka,maua.

Tujaribu angalia sehemu kama barabara ya Sam Nujoma kuna Palms zinazoitwa Roystenea Oleracea. (Royal palm)hizi zafaa kupandwa barabarani tokana na uhalisi wake zaweza vumilia upepo na vilevile size yake na haswa unene wa shina na urefu wake zinakubalika kukaa barabarani

Sasa kuna Palms zimepandwa pale eneo la barabara ya Ally Hassan Mwinyi maeneo ya Mbuyuni na njia panda ya Kaunda Drive zinaitwa Ptychosperma macarthurii(Fish Tail !) kwa kweli hizi si Palms za kupanda barabarani kabisa tokana na uhalisi wake kwanza hazitaweza kuhimili upepo mkali wa barabarani na zinaitaji matunzo ya karibu mno ! Kweli zinapendeza na watu wamejitahidi kuziweka pale lkn si muafaka kukaa pale.

Kuna Palms zingine zimepandwa pale Barabara ya Ally Hassan Mwinyi maeneo ya Morroco na Oysterbay Police station zinaitwa Washingtonia Robusta/Filifera nazo ni muafaka kuwa katikati na pembezoni mwa barabara kwanza size yake ni kubwa na hata nchi za wenzetu kama Marekani kwenye miji ya California utaweza ziona zipo kati na pembezoni mwa barabara.

Vilevile kuna aina zingine za Palms ambazo zinaitwa Phoenix Dactilifera (Date Palm/Mtende) hizi zinafaa sana nazo kukaa barabarani na tokana na uhalisi wake kwanza zaweza sana kustahimili ukame,size yake vile vile ni kubwa.

Vilevile kuna Shrub (kichaka) ambacho kimepandwa katikati ya barabara ya Sam Nujoma na sehemu zingine pia inaitwa Oleander huu mmea ni mzuri na unatowa maua muda wote ! na pia unastahimili ukame pia upo kwenye parking za magari pale ubalozi wa Marekani.Huu mmea upo ktk makundi kadhaa na na waweza kuutumia kama uzio,kivuli na mapambo pia.

Kwa hiyo basi tunaomba wale ambao watapata nafasi na fursa ya kushiriki ktk kupendezesha miji yetu wajaribu kuzingatia haya ili jitihada zao ziweze kuwa na manufaa mazuri.

Mdau Mzushi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2010

    Kwa kweli Ndugu Mdau Mzushi amenifurahisha saana na mada hii kuhusu hii miti. Yaelekea huyu ndugu ni mtaalam aliyebobea katika masuala ya mimea...nimeipenda sana makala hii kwani ni yenye kuelimisha na yenye manufaa kwa jamii!! Hizi ndizo makala zinazotakiwa haswaaa.....Wazee wa Jiji mpo??? Bravo ndg Mzushi.
    Ndimi, Eng. Italambaswa Mwaisumo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2010

    Bravoo mzushi...!!..nyie ndio mnaotakiwa huku kwenye hii nchi jamani..kwanini jiji lisiwe linatafuta watalaamu kama hawa ili mambo yaende safi? shida ya nchi yetu ni kujaza vihiyo kwenye sehemu nyeti ndo maana mambo hayaendi jamani..matokeo yake miti inapandwa siku ya Economic Forum kwa haraka haraka kuepusha aibu...why jamani? inakera sana. Manispaa ya jiji na watu wenu sijui mnasoma humu mlivoeleweshwa jamani. Labda uncle michuzi kwa kuwasaidia uprint hii uwapelekee maofisini mwao manake pengine wala hawajui kuna blogs na unaweza kupata habari kama hizi na wala hawaelewi nini maana ya blogs..TUTAFIKA KWELI?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2010

    Very good advice.This the way to go.Bravo.But the problem is the people in power done take free advice.They would always look for expensive advice.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2010

    asante mpenzi
    ntakupataje unishauri maua kwangu?napenda maua kwakweli

    ReplyDelete
  5. GOOD POINT MDAU....NYIE NDIYO MNATAKIWA NYUMBANI. KAMA UPO NJE YA NCHI MIMI NINAOMBA SANA URUDI NYUMBANI KUSAIDIA TAIFA KWA SABABAU INAONEKANA KUWA WEWE NI MTAALAMU FULANI.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2010

    Umetumia teminologies ambazo hawazijui!!! Maana kuna siku tutaona hata mkwaju umepandwa!! ha ha ha

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2010

    Hilo jina linakufaa kwelikweli!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 10, 2010

    kupendezesha mji kuendane na kupendezesha mifuko ya maskini sije hizo shrubs, palms n.k zikawa vificho bora vya vibaka.

    Mdau
    ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...