umati mkubwa umekusanyika usiku huu kushuhudia mechi ya Ghana na Uruguay kwenye viwanja vya Biafra jijini Dar katika screen kubwa kuliko yote nchini kwa hisani ya AfriCinema inc. ambayo Mkurugenzi wake mkazi Tanzania Bw. Stephen Rweikiza amesema huu ndio mwanzo tu wa mchakato wa kampuni hiyo kuonesha kwa umma uhondo kama huu
sehemu ya umati usiku huu viwanja vya Biafra
Mkrugenzi Mkazi wa AfriCinema Bw. Stephen Rweikiza (wa nne kutoka shoto) akisimamia maonesho ya bure ya kombe la dunia katika viwanja vya Biafra kwa projector ya kisasa na screen kubwa kuliko yote nchini




Uruguay not Paraguay.
ReplyDeleteScreen? Au Projector?
Inakuwaje hapo mvua ikishuka?
ReplyDeleteSi mchezo! Naona Africinema inatutoa kimasomaso. Kwenye nchi ambayo sio kila mtu ana uwezo wa kununua TV, hii imetulia. Niliona ni vizuri nijifunze zaidi kuhusu hawa jamaa wa Africinema, tovuti yao ni www.africinema.com
ReplyDeleteplase,ni projector hiyo!
ReplyDeleteSo what ni screen au projector who cares>>>Acheni wivu wapongo bwana...badala ya kuangalia maendeleo ya mtu mnakwanyua vijimaneno vyenu...Najua mliokomalia hiyo difference pua zinawavuja jasho kwa wivu tu hapo mlipo
ReplyDeleteMvua ikija watajua jinsi ya kufanya acheni longo longo
Hizi ndio faida za Open space inamsaidia kila mtu tatizo Mifisadi wakikutana na wazee wa mtindio wa ubunifu (JIJI) wanamegeana tu kwa kisingizio cha kuwekeza,Mahotel nk si wakejenge huko nje ya miji mbona maviwanja kibao??
ReplyDelete