Katibu mkuu kiongozi Mzee Philemon Luhanjo akimkabidhi tuzo ya utumishi bora Balozi Ombeni Sefue
Baadhi ya wadau wakijiandaa wakijiandaa kuingia kwenye boti tayari kwa Boat party iliyoandaliwa kama moja ya burudani ya mkutano huo
Dr Hamis Kibola akiwasilisha mada kuhusu UTT huku msaidizi wake Bi Nunu Sagafi akisaidia katika power point
Mwakilishi wa CRDB dada Farida akitoa maelezo ya jinsi ya kufungua tanzanite account kwa washiriki wa Diaspora.
Moderators wakijibu maswali kutoka kwa washiriki wa Diaspora mwenye mic ni Dr Semakula ,Bi Mahinga,Nyangoro na Negus Adrefris wa Ethiopia
Meza kuu ikiongozwa na Mzee Luhanjo ikipata Dinner ndani ya Boat
wadau wakiserebuka katika Boat party
Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) akiangalia mechi kati ya Kili stars na Houston iliyofanyika katika mji wa New Brighton nje kidogo ya jiji la Minneapolis.Houston iliibuka na ushindi wa mabao 6-2









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. US BloggerJuly 08, 2010

    Dr. US Blogger)

    Hii Diaspora halina maana yoyote, ni ya kutupiga changa la macho.Wanaojifanya wajuaji kama Dr. Shayo Nabii Yohanna Mashaka hawajapewa chochote licha ya jitihada zao uchwara

    Bingwa kama mimi msomi, wananiogopa kuingia kwenye sirikali yao, kwanza wanaogopa kunilipa mshahara wa hata Dola laki moja kwa mwezi tu, kwa hiyo wasitudanganye hapa na ma Diaspora. Kuna kuokota waosha wazee na wabeba boxi heti ma diaspora;
    bwana kuleni taimu na ma vimbwanga vyenu

    Nimetoka Oxford na phD ambayo inaheshimika dunia nzima, niliuwa na heshima kubwa kuliko wote na Tanzania haiwezi hata kunipa kazi ya uwaziri, licha ya yote sijaalikwa kwenye hiyo ma upuuzi
    Dr. US Bloggeer
    Alumni Oxford University
    Department of Economics

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2010

    Dr. US Blogger, nakubaliana na wewe mkuu. hawa viongozi wetu wapuuzi hawana maana yoyote na hiyo TANZANIA SIRUDI ng'o. wanaharibu hela za walipa kodi bure tu.Ni kweli Dr. Shayo amabye amesharudi Tanzania angepewa kazi nzuri tungekubali kumbe wanajitahidi, mashaka john ambaye yuko huko marekani ananufahisha wazungu naye angeshapewa kazi lakini wapi. hawa watu hawana maana yoyote, wanachofanya ni kwenda kuwaajiri watoto wa wakubwa wliokuja kusoma wakashindwa matokeo yake wakanunua vyeti feki na hapa ndio wanaorudishwa kuendeleza ufisadi benki kuu.habari ndo hiyo, hakuna cha diaspora, jaribu kurudi ulione joto la jiwe, mshaara hautoshi utabakia kufanya madili za kifisadi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2010

    Weee Dr USA Blogger kabla hujawa Waziri lazima uwe mbunge kwanza... huo usomi wako wa Oxford una uwalakini kama hujaliona hilo na kuna njia nyingi ya kutumia usomi wako pembeni ya Uwaziri!

    Diaspora ni chombo kizuri kuwaunganisha na kuwahabarisha wana-Diaspora yanayojiri nyumbani....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2010

    Kama una PHD kwanini usifundishe vyuoni? si lazima uwe waziri kwasababu PHD siyo qualification ya uwaziri!!. Watu wengi wenye PHD hawana experience ya kazi na ndiyo maana nchi ina siasa nyingi, PHD kafundishe na kuandika vitabu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2010

    US Bloger

    Pole sana, nani alikuambia PhD ni ya kupatia uongozi kama uwaziri?Naandika hapa ili basi tu lakini umeishanionyesha kuwa kama vile hazikutoshi, maana sijawahi kuona mtu wa PhD mwenye mawazo finyu namna hiyo kama kweli una hiyo PhD????
    Upo hapa Marekani wala hujajua namna ya kuitumia? Mbona vyuoni wanaitaka sana kwa nini usiende kufundisha na kuandika vitabu badala yake umebaki kuleta nuksi kwa diaspora kwa kuleta uzushi huo.Ualikwe wewe kama nani,mbona ilitangazwa kwa nini usijiandikishe na huyo Mashaka wako??

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2010

    Mie hii Diaspora pia naona changa la macho KWeli watoto wa Vigogo wengi wamesoma kidogo masomo yamewashinda, wamerudi wamepewa nafasi ambazo hawafai kupata, japo nakusema hivyo.

    US blogger japo nakusema hayo kidogo kuwa nanizamu yak uongea kama alivyosema mwengine kuwa na PHD sindio sababu ya wewe kuwa Waziri kuna vitu vingi vya wewe kuwa.

    Rudi Nchini TAnzania funguwa macho na akili za watu kwa kuwaelimisha si wote wanahizi Computer.

    tusiwe tunatupiana mate tu wakati wino upo na haukauki.

    MZ.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2010

    Wewe Us blogger, hakuna kitu kama Mshahara wa dollar LAKI MOJA. Hata hao ma-profesor wa hapa hawalipwi dollar laki moja. kwa kifupi mtu mwenye Phd hahitajiki kuongoza nchi.Au kwa maneno mengine watu wengi wenye Phd hawazitumii kabisa katika kazi zao ndio maana utakuta mtu ana Phd lakini haonyeshi tofauti yoyote kiutendaji na mtu mwenye first degree au second degree. Hapa USA watu wengi wenye phd ni waalimu au wako katika ma-reserch na kuandika vitabu na wala si mawaziri au Ma- CEO.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2010

    Kichaa Roby Kataaraia nakufagilia mwanangu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2010

    Wewe US Blogger pamoja na PhD yako, bado una mapungufu kama wanadamu wengine. You may be book smart, lakini huna wisdom. Huwezi kuwa waziri kwa sababu tu ya PhD. Pia inabidi uwe mbunge. Halafu inabidi ujuwe kuwa position ya uwaziri ni political. Kama wewe sio politician, utakuwa unachemsha tu na huo uwaziri wako. Ni tatizo pale wasomi wanapojihusisha na siasa badala ya kutumia muda wao kuelimisha jamii katika field yao. Kwa mfano, Sarungi medical doctor walimpa uwaziri, akawa anakwenda kwenye majukwaa na kupayuka sera za CCM badala ya kufundisha wanafunzi wa medicine, au ni bora wangemuacha pale pale alipokuwa director wa Muhimbili, field yake. Tatizo ni mis-alocation ya resources. Mwache engineer awe engineer, na doctor awe doctor. Pia kuwa na PhD sio kujua kila kitu. We learn daily as we go till we die regardless of our education levels.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2010

    WENYE PHD WALA HAWAPIGI KELELE WALA HAWAHITAJI UWAZIRI WA SERIKALI YOYOTE!

    Kwa sababu kama una Phd kwelu ya OXford tena ya economics mwanawane wala usingekuwa unangojea kujifagilia kwenye blogu ya Michuzi, kuna Postdoctorate kibao tu ambazo ungefanya kama ndio umemaliza recently, pili kazi za tafiti ziko kibao na zinalipa vizuri, kuna kazi kwenye mashirika ya kimataifa ambayo mishahara yake ni mikubwa kuliko hiyo ya mawaziri! Leo unalilia uwaziri???

    Yaani kweli sasa nimekujua kuwa wewe US Blogger hujakwenda shule kabisa na kama una Phd ni zile za kupewa kwenye Internet za wiki moja ua siku 7, yaani PhD feki. PhD yako ni feki kabisa kabisaa na hapa leo umewathibitishia watanzania hilo. Kwanza kila kitu kinachotolewa na kina Mashaka na wengine WEWE KAZI YAKO NI KUDANDIA TU. Hujawahi kuja na mada yako hata siku moja. Tahadhari kuna siku utakuja KUDANDIA TRENI KWA MBELE!! oOHOoo! Haya wee!

    Pili hata level za mishahara hujui kabisa, maana kama kweli ungekuwa umesoma hiyo doctorate, ungepewa kazi ya kufundisha undergraduate na kusimamia master students, na ungejua kuwa hakuna kitu kama huo mshahara wa dola laki moja uliotaja. Inaelekea wewe ni mbeba box wa nguvu na limeshakuganda na kukuzoea. Tatu ungejiregister kama ambavyo unatakiwa kujiregister kwenye conference yoyote ambayo uliatend ukiwa unasoma kama kweli ulisoma!

    Nina mashaka sana na elimu yako

    Mswahili

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2010

    wewe US Blogger acha kuchafua ma jina ya universities za watu !mimi na question sana kama umemaliza hiyo PHD na hichi chuo unacho dahi .kwani naonaga comments zako za kitoto sana sasa kama hapa unacho lala mika nini!! wewe ungekuwa na PHD usinge lia lia njaa humu! grow up bro !!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2010

    mimi naona mnamsema huyo us blooger kwa vile alisema ana phsd lakini point yake mmeshindwa kuielewa. Ni kweli hii midispora sijui nini ni changa la macho na kujifanya tu ili kupata safari za nje . Watuonyeshe hao waliorudi nyumbani ni nini wamefanikiwa kabla ya kuja kutafuta wengine?

    Nani kweli watoto wa watu wenye majina wameshindwa shule huku na wemerudi nyumbani na wanakazi za ambazo unajiuliza aliipataje na kwa elimi ipi. ( I am not here to name names) lakini I know couple of people ambao life iliwagonga sana huku na wamerudi na wanakazi nzuri sana..cousins zangu wana masters zao nao kiherehere wakarudi home na kunisemema sana mimi nilieng'ang'ania huku. Sasa hivi wana stress, depression na disappointing ya life big time.. Kazi wanazofanya niza afadhali anayefuta sijui vibibi huku

    Hawa hawana lolote wameona watu wamefunguka macho sasa wanahitaji hata hiki kidogo tunachopata tukitupe huko nchini wazidi kula...

    Wenyewe wenye vijisenti wanavihifadhi vijisent vyao nje ya nchi sisi tunaohangaika na kutoa jasho la hela yetu ati unaniambia nikawekeze bongo...Hata mtoto mdogo asiye na akili atauliza swali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...