MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MH. FREEMAN MBOWE LEO AMETANGAZA RASMI KWAMBA CHAMA HICHO KITAMSIMAMISHA KATIBU MKUU WAKE DK. WILBROAD SLAA KUGOMBEA KITI CHA URAIS KWENYE UCHAGUZI MKUU MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.
MH. MBOWE AMESEMA MCHANA HUU KWENYE MAKAO MAKUU YA CHADEMA YALIYOKO KINDONDONI JIJINI DAR KWAMBA KWA KAULI MOJA KAMATI KUU YA CHADEMA ILIYOMALIZA VIKAO VYAKE JANA IMEKUBALIANA KWA KAULI MOJA KUMUOMBA DK. SLAA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS, NA KWAMBA NAYE AMEKUBALI.
MBOWE AMEPANGUA HOJA KIBAO ZILIZOKUWA ZIKIPIGIA UKOPE UAMUZI WA CGHADEMA KUMPA DK. SLAA NAFASI HIYO AMBAYO MOJA KWA MOJA ATAKUWA HATETEI TENA KITI CHAKE CHA UBUNGE CHA KARATU, NA KWAMBA ENDAPO ATAKOSA URAIS ATAKUWA KAMALIZIKA KISIASA.
"OCTOBA 31 DK. SLAA ATAKUWA RAIS WA NCHI HII SASA UNAPOSEMA ATAKUWA AMEJIMALIZA KISIASA UNA MAANA GANI AMA NDIO UNAJIMU WENU AMBAO MMESHAUANZA.
"DK. SLAA NI MTU MAKINI NA MWENYE SIFA ZOTE ZA SIO TU KUWA RAIS BALI PIA KULETA MABADILIKO MAKUBWA AMBAYO NCHI HII INAYAHITAJI LAKINI HAKUNA WA KUTEKELEZA", ALISEMA MH. MBOWE KWA KUJIAMINI HUKU AKISHANGILIWA NA BAADHI YA WANACHAMA WALIOHUDHRIA MKUTANO HUO NA WANAHABARI.
MWENYEKITI HUYO WA CHADEMA PIA AMEKANUSHA VIKALI UVUMI KWAMBA DK. SLAA AMETUMWA NA KANISA LA DINI FULANI KUGOMBEA HUO URAIS, NA KUDAI HUO NI UMBEA WA BAADHI YA MAGAZETI AMBAYO KADAI AIDHA WAANDISHI AMA WAMILIKI WANATUMIKA KUKIPAKA MATOPE CHADEMA.
"kUNA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO VINABAKA WANANCHI KWA KUANDIKA HABARI ZA UMBEA NA KUPOTOSHA KWA MANUFAA YAO (WAANDISHI BINAFSI) AMA WAMILIKI WA VYOMBO HIVYO.
"NAOMBA BAADHI YA WAANDISHI WENYE TABIA HIYO WAIACHE WASIJE WAKAIPELEKA NCHI PABAYA", ALISEMA MH. MBOWE HUKU MEZA KUU WALIYOKETI VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHADEMA AKIWEMO NAIBU KATIBU MKUU MH. ZITTO KABWE, WAKITIKISA VICHWA KUUNGANA NA KAULI ZAKE.
KUHUSU UBUNGE JIMBO LA KARATU ATALOACHA WAZI DK. SLAA MWENYEKITI WA CHADEMA KASEMA WAO HAWANA WASIWASI KWANI HAKUNA CHAMA CHENYE YBAVU WA KUTWAA KITI KATIKA JIMBO HILO AMBALO ALIONGEZEA KWAMBA HALMASHAURI YAKE YA WILAYA IMEKUWA IKONGOZWA NA CHADEMA KWA MIAKA 10 SASA.
"DK SLAA PAMOJA NA KUWA CHACHU KUBWA YA USHINDI WA CHADEMA KARATU LAKINI SI YEYE PEKEE MWENYE UMUHIMU MKUBWA KULE JIMBONI. KUNA VIONGOZI WENZIE NA WANANCHI AMBAO KWA PAMOJA NDIO WALIOIFANYA CHADEMA ISIMAME.
"HIVYO KAA UKIHJUA TAYARI KUNA MGOMBEA MAKINI AMESHAANDALIWA NA ATAFANYA MAKUBWA KAMA ALIYOFANYA DK. SLAA", ALIFAFANUA.
Habari leo Nukuu
ReplyDeletekutokana na Slaa kuwa ni Padri wa Kanisa Katoliki na kwa kuwa aliwahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuna uwezekano mkubwa pia wenzake kumshawishi akubali nafasi hiyo kwa matarajio ya kuungwa mkono na Kanisa na waumini wake katika kinyang’anyiro hicho.
Hii inamaanisha nini, Slaa akiwa Raisi atakuwa wa wakatoliki tu au ?
Sasa Kura Yangu Ya RAIS imepata pa kwenda...CHADEMA IKULU 2010
ReplyDeleteebwana hapo ndio makao makuu au?
ReplyDeleteWe nyang'au mtoa maoni wa kwanza acha kupandikiza udini wako hapa. Pambavu mkubwa. Nani alikwambia Dr. Slaa ana udini. Changamoto ni nzuri ktk mchakato wakupata waviongozi imara. No dought kuwa Dr. ni muadilifu mkubwa na mtetezi wa wanyonge. umesahau alipobakia mwenyewe alipopinga ongezo la mishahara ya wabunge? Nyang'au mkubwa.
ReplyDeleteWewe mchangiaji wa kwanza funga mdomo wako na unyamaze kama huna la kuandika. Leo ndiyo unajua kuw Dr.Slaa alikuwa Padri na Katibu Mtendaji wa TEC, unasahau kuwa JK ni Luteni Kanali wa Jeshi kisha Alhaji, Makamba ni Luteni, George Mkuchika ni Kapteni, je kumekuwa na uanajeshi IKULU.
ReplyDeleteHoja ya maana ni kama anaweza. sasa CHADEMA wanakuambia anaweza basi subiri wakati wa kampeni ukasikilize ILANI yao.
MDAU NAMBA 1 UNA IQ ZAIDI YA 100 KWELI? KWAHIYO KIKWETE NI RAISI WA WAISLAMU?
ReplyDeleteAnon wa kwanza hapo juu siwezi kukujibu swali lako lakini nina swali ukiweza lijibu basi na lakwako litajibika hapo hapo. Kutokana na JK kuwa muumini wa kiislamu, mgombea mwenza muislamu, na raisi wa zanzibar muislamu (yaani Dr. Bilal na Shein wote waislamu) je ikishinda CCM Rais atakua wa-waislamu peke yao? Michuzi usiibanie hii sio personal ila nataka tuelimishane kwenye hili.
ReplyDeleteMdau unayeuliza hapo ndio makao makuu ingawa sijawahi fika, lakini sijashangaa kwasababu nategemea makao makuu pawe hivyo. Kwanini- kwasababu Tanzania ni nchi maskini na walio wengi ni maskini sana sasa makao makuu ya chama yakiwa yahali yajuu sana nitashangaa hawa viongozi wamepata wapi pesa yakujenga makao yakifahari wakati wananchi wanateseka?? Ni afadhali upeleke pesa kwenye maendeleo kuliko ujenge ofisi zakifahari. Hayo ni mawazo yangu.
ReplyDeletenaona watu washaanza propaganda ya udini sasa.kweli watanzania tunapendwa kuongozwa na mambumbumbu na sasa tumepata kiongozi wa maana watu wanaanza kujaribu kujenga hoja za chuki.
ReplyDeleteMimi kwamawazo yangu naona watanzania umefika wakati tuchague kiongozi sio kwasababu ya chama bali kutokana na uwezo wa mtu. Kuna watu wanakimbilia kugombania kupitia chama fulani lakini wanauwezo mdogo kabisa lakini kwasababu chama kina-nguvu wanauhakika wa kupata. Nawapo wenye uwezo lakini hawachaguliwi kwasababu wako kwenye chama fulani. Mi naona chagua kutokana na uwezo wa mtu, kama ni CUF, CCM, CHADEMA no problem tukipata wabunge, madiwani mchanganyiko wanaojua kufanya kazi watashindana kwa hoja nchi itasonga mbele. Trust me: "Problems become opportunity When the right people come together".
ReplyDeleteJamani turudi kwenye TOPIC huyo annony wa kwanza kawekwa makusudi ili tusijadili POST tumjadili yy na upuuzi wake. Huyo ni mjinga tu pamoja na wale waliomtuma!!!
ReplyDelete.........................
baada ya tarehe 31/10/2010 tunaweza kuongea habara mpya.
VIVA SLAA...VIVA CHADEMA.
EEE MUNGU TUSAIDIE TUMECHOKA KUNYANYASWA NA HAWA GREEN.
I think they need to get a Brand and Activation Manager to manage the brand "Chadema" as the event has been done not to the level of presidential. Very poor back ground and picture apperance. Does not potray seriousness.
ReplyDeleteAT MY AGE OF 35. FOR THE FIRST TIME AM GOING TO VOTE!
ReplyDeleteNOW WE HAVE THE PRESIDENT !! LETS MAKE REVOLUTION!! VIVA DR. SLAA!
AM SICK AND TIRED WITH CHA CHA MAFISADI (CCM).
Wawaaaa!! zats ma presidaa!!
ReplyDeletewera weraaaa dr. slaaaaa!!!
MWaka huu nitapiga kura...Sasa ole wenu ninyi CCM mje na matokeo yenu ya asilimia hata 45% eti za uraisi wa mzee wa kucheka, tutaingia mitaani
ReplyDeleteWe anony wa Wed Jul 21, 05:11:00 PM
ReplyDeleteJK hajawahi kuwa kiongozi wa waislamu (Bakwata na taasisi nyingine) wala hajawahi kuwa shekhe wala imam wa msikiti wowote. Kwahiyo wanaomlinganisha Kikwete na Dr. Slaa mnakosea. Lazima ukubali kuwa mtu utetea anachokiamini na kama alisha kuwa kiongozi wa kanisa atetea kanisa baada ya nchi na ukizingatia hivi sasa nchini kwetu kuna udini udini, kwahiyo tunaitaji kiongozi asiyekuwa na masirahi na dini yoyote. Ndio maana ata bungeni mtu ukiwa na masrahi na hoja yoyote unatakiwa uweke wazi (uainishe)
Ankali nashukuru kwa hii. Naomba utafute picha ya nje ya makao makuu ya hiki chama uniwekee kwenye libeneke nipate hatma ya kura yangu. Tayari nina masikitiko kwa hii niliyoiona.
ReplyDeleteNDUGU ZANGU WAISLAM MSICHAGUE MGOMBEA URAISI WA CHADEMA, ANA MASILAHI BINASFI NA KANISA KATOLIKI (ALIKUWA PADRI) NA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA(ALIKUWA KATIBU). ALISHA TUMIKIA TAASISI ZOTE HIZO MBILI NA AMETUMWA NA TAASISI HIZO KUGOMBEA URAISI KWA MASLAHI YAO. CHAGUENI MTU YOYOTE KUTOKA CHAMA CHOCHOTE AMBAYE HANA MASILAHI NA DINI YOYOTE ILE JAPO KUWA ANAWEZA KUWA MUUMINI WA DINI YOYOTE. HATUTAKI VIONGOZI WALIOWAHI KUTUMIKIA(KUONGOZA) TAASISI ZA DINI KAMA MAKANISA, BAKWATA NA NYINGINE WANAKUWA NA MASILAHI NA TAASISI ZAO. CHAGUENI WAGOMBEA WA URAISI KUTOKA CCM, CUF NA TLP NA VYAMA VINGINE WAKIJITOKEZA AMBAO HAWANA MASILAHI NA TAASISI ZA DINI ILA SIO CHADEMA.
ReplyDelete" A person can be good in a bad word, but a bad world cannot be better unless those who value good unite, organize, and mobilize in a struggle to change the world," (Rweyongeza owa Maruku, 2010). Kwa matinki hiyo basi wana wa Karatu, kilimanjaro, Manzese, kibiti, Maruku, Kagera, Bagamoyo, Tanga, lindi, Mtwara, Songea, Iringa, Morogoro, Dodoma, Mburahti na Tanzania kote: Wakati mmoja tulimtaka Salim Salum (retired and seasoned Diplomate) wakampiga majungu ya kijinga, ambayo baadae tumeyaoona kwenye uongozi wa miaka mitano; wapiga domo kaya tupu na poda kwa wingi, rangi za kuficha mvi kwa wingi, bila kufanya kazi za kitaifa; Sana sana ni self-care!SASA TUMEPATA KILIO CHA SAUTI YA WOTE; NA TENA SI MPIGA ZUMARI TU...NI MSEMA UKWELI NA MTENDAJI MAKINI; Sisi Waislam, Wakristu, Wenye Dini zetu za Aslili, na ambao hatuamini katika Dini yoyote tunakuombea Dua ndugu yetu Dr. Slaa (Tena Doctor wa Darasani, na si wakupewa kwenye sinia degree ya wale wenye kutaka kuvyonza madini la raslimali zetu): Upepo wa Mapindu ya kweli waja, through a good person like Dr. Slaa and Dr. Hamis "Igunga): Tuunganishe nguvu kwenye sanduku la kura walau CCM walambe vumbi. CCM bye bye.....
ReplyDeleteTz ni nchi ya kisekyula, hata hivyo kuwa na raisi aliyeshika madaraka makubwa kwenye dini kunaweza kuwa changamoto akiteleza kidogo.
ReplyDeleteBora hao viongozi wasio na dini (kama kingunge) au wafuasi wadogo (kama sumaye). Kwanza hawachanganyi dini na siasa,kama tulivyoshuhudia nyuma.
U-alhaji si o cheo, mtu yeyote aweza kuwa.
Dini yake we inakuhusu nini au unagwaya atakuwa St. asiyetoka sisiemu?
ReplyDeleteJina langu ni Said Omary Yakub na e mail yangu ni saidyakub@yahoo.com najiweka wazi kwamba mimi ni Muislam, lakini napingana waziwazi na mdau wa kwanza na wote wanaomkataa Dr. Slaa ati kwa sababu ya ukatoliki wake au wale waliomjibu mdau wa kwanza kwa kutoa mifano ya viongozi waislamu. Sidhani katika Bunge letu tukufu hakuna mtu asiye na dini pale. Hii si nchi ya Kiislamu, Kiyahudi, Kikristu, Kibhuda, Ki kila kitu bali ni nchi yenye uhuru wa kuabudu.
ReplyDeleteTunachoangalia hapa si udini, au ukabila. Tunachoangalia hapa ni uadilifu wa kiongozi. Nadiriki kusema kwamba wapumbavu wachache kama annoni wa kwanza ndio wanaaopaza sauti zao kutetea masuala ya udini. Udini ni kitu sensitive sana sio kitu cha kufanyia mzaha kama wapumbavu wachache wanavyoendekeza.
Mimi kama mpenda amani na maendeleo na muislam, sioni kasoro ya kumchagua kiongozi bora na mzalendo hata kama si wa dini yangu sababu nimezaliwa nikamkuta Nyerere ni Rais na nimemsikiliza na kuelewa falsafa zake kuhusu Udini na ukabila jinsi alivyokua akituelewesha na kutufundisha athari zake.
Tukirudi kwenye mada binafsi nampongeza Dr. Slaa kwa kuchaguliwa kwake na kwa umuhimu na mchango wake kwa Taifa kwa kutufungua macho hadi leo hii hata asiyekwenda shule anajua EPA ni kitu gani hivyo basi namtakia kila la kheri katika safari yake hiyo.
Nyie mliochangia hapo juu. Mnaukumbuka WARAKA wa KANISA kuwataka waumini wake wamchague nani? Je mnakumbuka mahubiri ya yule padre wa Manzese kuhusiana na serikali inayoongozwa na CCM? Sasa wakati wa kuutekeleza waraka umefika. Je huyo mgombea mnamfahamu vizuri kweli? Kweli kasomea sheria ya CANON LAW inayofundishwa na kanisa lake. Mimi sitampa kura yangu. Najua kura yangu nitampa nani. Siyo huyo.Waulizeni watu wa kwao. Waulizeni NGO alizoongoza na kutafuna fedha yake. Hivi mnajua kwa nini alifukuzwa upadre? Mnajua?
ReplyDeleteDr slaa ni mtetezi wa wanyonge,ni mtu anaejali maslahi ya watu wa chini,ata ufisadi wa bot aliupigia kelele sana ata tukajua tumepigwa changa la macho
ReplyDeletejamani sisi ni nchi maskini,tusiangalie ubinafsi wa wajinga wachache wanaoendekeza dini maana hamna siku dr slaa amekua anaongelea dini au kutetea dini yoyote
VIVA DR SLAA,U HAVE MY VOTE
MAY GOD BLESS SLAA,GOD BLESS TANZANIA!!
kama ni maswala ya udini mbona wakristo tumekuwa wavumilivu sana? Wapi umeona katika baraza la mawaziri ZNZ kuna mkristo au mtu kutoka bara? Lini ZNZ watapata rais mkristo au waziri kiongozi mkristo? mbona katika Serikali ya muungano tunao wawakilishi wengi kutoka ZNZ (yaani mawaziri) na hata bungeni tunaowawakilishi na wote ni waislamu, je hakuna wakristo wenye sifa kuchaguliwa katika nafasi hizo?? Tumekuwa wavumilivu sana. Lately CMM imefanya uteuzi wa wagombea Urais wa ZNZ,TZ na mgombea mwenza wa TZ wote waislamu. Kwa nini sasa kuna mapandikizi yanayotaka kuleta uchochezi juu ya uteuzi wa Dr. Slaa? Mbona alivokuwa bungeni hatukuona akirepresent maslahi ya dini fulani bali watanzania wote?? Jamani mwenye macho haambiwi tazama. Kama tukitaka kuchochea udini katika uteuzi wa wagombea, nafahamu vyama ambavyo vitakuwa most affected so CCM na hao wengine better stay quite...
ReplyDeleteWandugu mimi ni MKATOLIKI lakini kura yangu nampa Jakaya. Naungana na wote wapinga udini nchi yetu haina sifa ya kuchagua Maaskofu au Mapadri waasi. Dr. Slaa ni Padri muasi au Katibu mstaafu wa TEC muasi hivyo hafai hata kidogo. Kama liweza kulisaliti Kanisa kwa tamaa za dunia atashindwa kutuuza wananchi tusio na hatia,HAFAIII..HAFAIII...HAFAII
ReplyDeleteBana R.(Mkatoliki mkereketwa)
Vancouver,
British Columbia
AT LEAST KWASASA NITAWEZA NIKAPANGA FOLENI KUPIGA KURA.
ReplyDeleteWewe uliyeandika maoni ya 10:45 acha kuchafua majina ya watu, wewe si Saidi Yakub. Saidi Yakub ni Afisa wa Bunge kama una chuki nae binafsi usilete humu. Hapa hatuzungumzii mambo ya Bunge tunazungumzia Urais,Slaa hafai Urais Ubunge ndio unamfaa. Hatopata kura labda Moshi na Arusha tu
ReplyDeleteHapa nilipo ninalia sana kwa Dr. Slaa kuachia kiti cha Karatu, haya ndio kama yale ya yule Mpendazoe,Dr. Slaa umeshajimaliza kisiasa masikini. Dr. Slaa umerogwaje hadi ukakubali ushauri mbovu? Je, ulituuliza sisi wanachama wa jimbo lako? Kati ya Mbowe na sisi wa jimbo lako nani ulipaswa kumsikiliza? Sisi hatukukuruhusu ukagombee Urais tulikutaka jimboni mbona unalikoroga halafu unatuachia sie tulinywe hapa Karatu?
ReplyDeletePaul Nditi, Arusha
jamani viongozi wangapi wa Kiislamu wamekwenda HIJJA wakiwatayari wamechaguliwa na wamerudi tumewapigia tena kura bila matatizo?
ReplyDeleteSlaa amekuwa bungeni kwa miaka 10 sasa. ni lini alijihusisha na hoja zenye udini?
huko jimboni kwake amechaguliwa na watu wa dini zote, Waislamu included, na hatujawahi kusikia matatizo yoyote yale.
tuachane na chokochoko za udini.
anoan wa Thu Jul 22, 09:16:00 AM,
ReplyDeleteni vizuri kuvumilia lakini pia ni vizuri kujua uhalisia.
Ndoto yako inwezekana kutimia baada ya miaka mingi saana.
Kumbuka serikali ya muungano ni ya woote na ya ZN ni yao peke yao.
Tungetafuta serikali ya wada(ta)nganyika pia usingeona mzenji katika uongozi.
we anony wa Thu Jul 22, 04:47:00 PM
ReplyDeleteKwenda hijja ni kufanya ibada tu kama kwenda mskitini au kanisani, sio kuongoza taasisi ya dini. Sisi hatukatai mtu kuwa na dini yake, kwenda msikitini au kanisani, tunakataa mtu mwenye maslahi na kanisa au taasisi ya dini yoyote kuongoza nchi. Mimi ningepinga hivi hivi kama amtu angetoka bakwata akaja kugombea uraisi wa TZ.
Na wewe anony wa Thu Jul 22, 09:16:00 AM.
Nenda kasome Katiba ya nchi kwanza kabla haujaleta hoja. na population ya Zanzibar ni 99% waislamu sasa wewe unategemea mkiristo atoka wapi hapo.
Anony 23 july, 01:43 am
ReplyDeleteOK so 1% ya wakristo ZNZ hawana representation then lazima waislamu wa znz wa takuwa na maslahi makubwa zaidi katika serikali.
na pia kuna watu wa imani zao ambao siyo viongozi wa kanisa wala misikiti lakini wana 'interest' katika dini zao ndiyo maana tunasikia wabunge wengi wa kiisalmu wadai mahakama ya kadhi...
Ndugu Nditi, nakusihi usiogope kuwa umempoteza Slaa Karatu. Watanzania wanamhitaji alikomboe taifa. Taifa ni zaidi ya Karatu. Taifa likimpata Slaa basi Karatu nayo imempata Slaa. Tunaombea ushindi. Tuungane tumumuunge mkonno Slaa.
ReplyDeleteSlaa mbele kwa mbele
ReplyDelete