Na Novatus Makunga,
Jumuia ya Afrika ya mashariki[EAC] yenye makao makuu yake mjini Arusha, imeikaribisha rasmi Jamhuri ya KiDemokrasia ya Congo (DRC) kujiunga na Jumuia hiyo ambayo kwa sasa ina nchi wanachama tano zikiwemo Tanzania,Uganda, Kenya.Rwanda na Burundi.
Ukaribisho huo umetolewa na katibu mkuu wa Jumuia ya afrika ya mashariki Balozi Juma Mwapachu wakati akipokea hati ya Balozi wa DRC hapa nchini,Juma-Alfani Mpango ili awakilishe nchi yake katika Jumuia hiyo.
Balozi Mwapachu amesema, DRC ina uhusiano wa karibu mno na nchi za EAC, hivyo kujiunga kwake na jumuia hiyo inakuwa ni tukio la kihistoria litakaloleta hatua nyingine ya uhusiano baina ya EAC na DRC.
Uhusiano wa karibu kati ya DRC na EAC unajidhihirisha katika nchi hiyo kushirikiana na nchi za jumuia hiyo katika miradi ya kufufua umeme katika nchi ya Uganda kupitia Ziwa Albert na pia nchi ya Rwanda kupitia Ziwa Kivu.
Aidha Balozi Mwapachu aliipongeza DRC kwa kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wake na pia alitoa rambirambi kutokana na tukio la kulipuka kwa lori la mafuta katika kijiji cha Sange na kuuwa watu zaidi ya mia moja wiki iliyopita.
Akiwasilisha hati yake iliyosainiwa na waziri wa mambo ya nje wa DRC April 24 Mwaka huu balozi Mpango alisema kuwa nchi yake imeamua kuchukuwa hatua hiyo kwa lengo la kuimarisha uhusiano uliopo na EAC.
Alisema kuwa seriklai ya nchi yake inaamini kuna mchakato wa mtangamano wa Jumuia ya Maendeleo kusini mwa Afrika(SADC),Jumuia ya soko nafuuoja kwa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika(COMESA) na EAC ambao utasaidia kupanua mahusiano yao katika nyanja zote muhimu.
DRC ni mwanachama wa COMESA na SADC ambazo kwa pamoja hivi sasa zipo katika mchakato wa kuoanisha sera na taratibu zao ili nchi zote ziingie katika eneo huru la biashara.
Balozi wa DRC anakuwa wa nne kuwasilisha hati ya utambulisho katika jumuia hiyo ya Afrika Mashariki. Mabalozi wengine ni pamoja na wa Marekani,Denmark na Uturuki
Kuongeza mahusiano baina nchi jirani sio wazo baya ila ni muhimu EAC kuazima policies za E.U na kutumia kama mfano wa kuendesha mipango yao, kwa mfano nchi zote kuwa na internal security,na equal economy,au economy ambayo inadevelop at a certain rate ni vigezo muhimu,kwa maana kama nchi ikiingia kwenye hii jumuiya na haina hali nzuri kiuchumi wananchi wake watahama kwenda nchi nyingine kutafuta kazi,sio mbaya lakini wakihama kwa wingi wanakuwa wananyima nafasi kwa wananchi wa zile nchi wanazohamia,especially kama kuna freedom of movement,so ni vema kutatua haya matatizo baina nchi wanachama wa EAC wakati bado jumuiya ni changa,kabla kukaribisha more members itakuwa vigumu zaidi ku-manage.
ReplyDeletesio wazo baya kukaribisha nchi nyingine ktk hiyo jumuiya,lkn cha msingi ni kuangalia hz nchi zinamaslahi gani kwa kila kwa nchi nyingine.Km alivyosema mchangiaji hp juu,nchi itakayobeba mzg ni Tz maana kenya wnakimbilia Tz sababu hawna aridhi,burundi,rwanda na DRC ni nchi zenye vita na wananchi wanakimbilia Tz kuokoa maisha yao,uganda wanamatatizo yao.Hivyo nafikiri nchi itakayoumia ni Tz au ndo ule msemo wa KICWA CHA MWENAWAZIMU?ni wkt viongozi wetu waamke usingizini na kuangalia maslahi ya watanzania na sio maslahi yao.
ReplyDeleteTutajaza wakimbizi tu saa bongo...Nyie hata mwezi haujaisha mkaona mafanikioao ya huu umoja manakaribisha wengine
ReplyDelete