JK akiwa na Mama Salma Kikwete muda mfupi baada ya kuvikwa mavazi ya kijadi kama mtemi na malkia wa Wanyamwezi leo wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Urambo Mshariki leo mchana
Mama Salma Kikwete akivishwa joho kwa ajili ya kumsimika kama mlezi wa Mke wa Mtawala wa Kabila ya Wanyawezi. zoezi hilo lilifanyika mara baada ya Rais Kikwete kutawazwa leo wilayani Urambo kuwa kiongozi wa Kabila la Wanyamwezi
JK akikata utepe kufungua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta (Kushoto) ambaye pia ni Spika wa Bunge. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.JK akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Aliyesimamam ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta.
JK akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge akiwakaribisha waheshimiwa wabunge mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege Urambo kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Kushoto ni Mbunge wa Mafia Mhe. Abdukarim Shah
JK akiwahutubia mamia ya wananchi wa Urambo mkoani Tabora wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Mbunge wa jimbo la Urambo Mshariki leo. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. VOICE OF URAMBOJuly 14, 2010

    DU!JK URAMBO PICHA MOJA TU!NO PICHA INAYOMUONYESHA JAPO MBUNGE WA SEHEMU HUSIKA,HEBU WEKENI PICHA YA MH.MBUNGE WETU ALAA!MZIGO MZITO MPENI MNYAMWEZI ATAUBEBA TU

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2010

    naomba kuuliza, wabunge wote wanakaa dar, then wanajengewa ofisi ya sh.milioni 170 huko jimboni ambako huwa wanakaa muda mchache sana, wangejenga hata ofisi ya sh.milioni 10 angalau,kwanini hizo hela zisingefanyiwa kitu kingine cha maana zaidi kwa mfano kuboresha huduma za afya, bado kinamama wajawazito na waliojifunguawanalala chini mahospitalini,inasikitisha sana.
    mdau USA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2010

    Huu tunaambiwa ni wakati wa kuminya matumizi ya serikali!

    "Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini."

    Hivi tuna wabunge wangapi nchini?

    Halafu ufanye hesabu...na huku shule za kata zikidorora...wanafunzi wanakalia mawe na kuumiza matako yao!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2010

    Mdau wa USA,
    Mbona USA Senetors na Congress men/women wanakaa D.C? Mbona wengi wana ofice D.C na kule kwenye majimbo yao wanayotoka. Kwa mfano senetor wa Illnois ana Ofisi D.C na pia kwao Illnois. Na muda mwingi ukienda kwenye ofisini kwake Illnois unakuta staff aide ambao wanaweza kukushughulikia mambo yako chap chap.

    Je hauoni hizi ofisi zitawafanya wananchi wawe karibu na wabunge wao?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2010

    WEe acha umbeya unayesema masenator wanakaa DC yes kweli 100% wanarent huko DC...lakini kwetu hawakai Dodoma wanakaa Dar you get the difference..Ni kama masenator wote wakae NY city have you seen that ...Kaa kimya kama kitu hujui aliyeuliza kasema kweli all that money for the building that no one will use it...I hope they will use as something for the villagers to go and rest if they need a break from their boiling mud huts in that kind of weather we have.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 15, 2010

    jamani office na nyumba ni tofauti !! office hina weza kuwa ndani ya nyumba hila nyumba haiwezi kuwa ndani ya office !! hapa wanazo zungumzia ni nyumba !!got ma point. wabunge wanapenda sana umwinyi wakati kazi awapendi kufanya ! hizo pesa bora wa wanunulie wanafunzi madawati

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 15, 2010

    Jamani hebu tumieni busara. Munalinganisha ofisi za maseneta wa Marekani na wabunge wetu?. Kuweni na taswira halisi ya mambo si mulinganishe nchi mbili ambazo hazilingani kwa aina yeyote. La msingi ni labda kupunguza gharama za hizo ofisi kwani fedha hizo ni nyingi sana ukilinganisha na hali yetu kifedha.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 15, 2010

    Wee mdau wa Tarehe Thu Jul 15, 12:47:00 AM,

    Asante sana. Wape vidonge vyao hao. Wamezidi kuchonga!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 15, 2010

    MIJITU ISIYO NA UJUZI KUHUSIANA NA GHARAMA ZA UJENZI UTAYAONA TUU. ETI OFISI YA MILLIONI KUMI IANTOSHA. HIVI UNAJUA KWAMBA MILIONI KUMI HAITOSHI HATA KWA KUFANYA FINISHING YA NYUMBA YA KAWAIDA YENYE VYUMBA VITATU?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 15, 2010

    Jamani ya Marekani yaachwe huko huko Marekani! Hata Wamarekani wakiwa na ofisi za madiwani potelea mbali coz they can afford it na at least matatizo ya kimsingi ya wananchi wao yanaangaliwa. Sasa nchi ambayo wananchi wake kuwa na maji safi ya kunywa bado ni ndoto kweli tunahitaji majengo haya? Hivyo vituo vya afya tu kwenye ngazi ya chini bado ni vichekesho kweli tunaongelea miradi kama hii ambayo kimsingi anaangaliwa mtu mmoja tu katika kila jimbo la uchaguzi rather than wananchi walio wengi? Na je, ukaaji wa hao waheshimiwa huko zinakojengwa ofisi za gharama hizi ukoje? (Wote tunajua makazi yao yalipo) Mimi nilifikiri tunapoambiwa tufunge mikanda kwa kuwa serikali haina pesa inakuwa imemaanishwa! Waheshimiwa mko serious kweli wenzetu?

    Ankal, please don't bana this, acha tusio na pa kusemea tuseme yanayotukera...

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 15, 2010

    jamani nimempenda yule mbunge wa kushoto abulkarim yaani ana body nzuri kweli halafu ni msafi yaani napendaga disaini za namna hii

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 15, 2010

    Naona mila,desturi na tamaduni za makabila zimepoteza muelekeo.nini hasa maana ya kuwa mtemi au chifu wa kabila fulani?
    Ni mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi wa mila wa kabila lolote alipendalo nchini?
    Nadhani rais wetu ana majukumu mengi sana,haya ya kuongoza makabila tuwaachie wahusika wengine.
    Badae tutasikia kabadilishiwa kabila.
    NADHANI SASA HII NI CV YAKE
    Rais wa jmhuri ya muungano wa tanzania,amirijeshi mkuu,chifu wa wasukuma,mtemi wa urambo,mangi wa kibosho,mwenyekiti wa ccm taifa dr.Jakaya Mrisho Kikwete.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 15, 2010

    Nijuavyo Mimi, Mpango wa serikali ni kweli wanajitihada ya angalau kumwezesha kila mbunge kuwa na Ofisi katika majimbo yao angalau kuwe na sehemu ya kukutana na wananchi wao pamoja na wageni mbalimbali tofauti na sasa ambapo mbunge akipata mgeni wanakutana Hotelini au nyumbani. Na pia mpango wa serikali sio kujenga ofisi hizo kwa gharama ya Tsh 170. JK Mwenyewe (Fuatiliana News za Jana) kawaasa wabunge kuwa serikali haitajenga Ofisi zote kwa kiwango cha Ofisi ya Mbunge wa Urambo. Ule ni upendeleo pekee kwa Mbungu huyo kwa nafasi yake aliyonayo ya Uspika. ambayo anaamini atashinda tu katika Uchaguzi ujao na kurudia kiti chake.
    Lakini pia Mbunge kuwa na ofisi ni muhimu kwa kuwa hata kama atakuwa dsm, ofisi haiwezi fungwa! watumishi wapo. mfano mzuri ni kwa watani zetu Kenya ambako mbunge anaofisi Bungeni na Jimboni (Nzuri) tofauti na sie ukitaka kumuona mbunge wako Dodoma ni ama mkutana kanteen au umvizie akiwa anatoka mjengoni! Nadahani uwamuzi wa serikali kwa hili ni poaaaaaa

    Mdau toka Umatumbini.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 15, 2010

    Mbunge kuwa na ofisi jimboni ni muhimu sana. Kama ni mwakilishi mzuri anatakiwa apate muda wa kukaa jimboni na kujitahidi kusikiliza na kushughulikia na kuyapeleka kunako husika matatizo ya watu wake. Labdo hapo swala la gharama za ujenzi ndio liangaliwe ila kuwa na ofisi ni hatua nzuri.

    ReplyDelete
  15. VOICE OF URAMBOJuly 15, 2010

    ASANTE BWANA BLOGGER KWA KUSIKILIZA KILIO CHANGU SASA NIMEZIONA PICHA ZA MBUNGE WANGU WA URAMBO ZA KUTOSHA HUMU NDANI,INATIA MOYO SANA KUONA MNAJALI MAONI NA VILIO VYA WANAJAMII.IDUMU DAIMA MICHUZI BLOG,ANAESEMA IFE AFE YEYE KWANZA

    ReplyDelete
  16. mtani wa wakwereJuly 15, 2010

    Hongera mh.JK kwa kufanya ziara Tabora ambako mimi binafsi nahisi ndio kwenu,kwa kuwa huo mwili ulionao si mwili wa kikwere huo ni mwili wa kinyamwezi,wakwere ni watu ambao miili yao huwa midogo midogo,hilo lako ni dongo la kinyamwezi pure

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 15, 2010

    Tatizo hapa ni priorities. Jk na utawala wake hawajui prioritization kabisaaaa. Unajenga ofisi kubwa hivyo ya kisasa wakati hosipitali na shule za huko Urambo ni zakujikongoja. Kwanini usijenge simple office kwakutumia cheap resources hata ikiwa ni kubadilisha contena iwe ofisi alafu hela nyingine tumieni kwa maendeleo mengine.Hapo utakua umeua ndege wawili jiwe moja. Yaani I real don't get it. Michuzi usiibanie hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...