Aliyekuwa kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo, ameagwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika hafla fupi iliyoandaliwa na TFF Msasani jirani na shule ya Feza jijini Dar es salaam. Katika hafla hiyo, pamoja na mambo mengine, Kocha Maximo alipewa zawadi mbalimbali ikiwemo ya kinyago alichopewa na Mwenyekiti Mtendaji wa kiwanda cha Serengeti, Jaji Mark Bomani.
Ni dhahiri kwamba kocha huyo atakumbukwa kwa kazi yake aliyoifanyia Tanzania japokuwa bado kuna wadau wa soka ambao wanasema hakufaya kitu ila tunaojua kusema asante tunasema Maximo amefanya kitu kikubwa katika soka letu lililokuwa la kichwa cha Mwendawazimu enzi hizo, na anastahili kupongezwa mpaka hapa alipotufikisha manake kuna methali inayosema "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni"
Yote kwa Yote tunasema Watanzania tunajifanya tunajua sana mpira wakati kujua kwetu kuko vinywani zaidi kuliko vitendo na kama ndiyo hivyo basi tukubali kwamba hatujui jamani.
Maximo akiwa na baadhi ya wachezaji

kwa chanzo na picha na habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Tanz 1 Brasil 5

    Tanz 1 Egypt 5

    Rwanda 1 Tanz 0

    Rwanda 2 Tanz 0

    Yemeni 2 Tanz 1

    Cameroon 2 Tanz 1

    Tanz 0 Msumbiji 1 (uwanja mpya wa taifa)


    Record kenge hii

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2010

    nenda salama ulipo tufikisha si haba mpaka nasisi leo tunaongea watakae kuponda sio wana michezo tuna thamini mchango wako.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2010

    Sisi watanzania maneno mengi lakini mpira hatujui, Ni kama vile waingereza walivyo kubwabwaja kwingi wakiingia uwanjani wanakula magoli

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2010

    Uliyeandika matokeo ya kufungwa hujui kitu nyamaza, kama hutanyamaza andika na ya kushinda basi, au andika na yakufungwa ya miaka miwili ya kabla hajafika Maximo.
    Utakuta Ushelisheli, Somalia, Djibout, na viji-team fulani vilitufunga sana tu. Mkiendekeza fitina na majungu hata aliyekuja mtasema hana kitu wakati ana record kubwa tu. Waswahili bwana!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    Ndio hao wakiona kwa jirani wanakula nyama mara samaki ananuna!!
    Hao waliokuwa wanapika majungu mbona hizo form za kuomba kuifundisha timu hawakuchukua? Soka ni science!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    we fala hapo juu mbona umechagua rekodi za kuweka
    kuna nyingi za mafanikio.
    tan 1 bukinafaso 0
    tan 1 senegal 1
    tan 1 cameroon 1
    tan 2 uganda 1
    tan 3 kenya 1
    kima wewe,kazi chuki binafsi tu,muache maximo wa watu arudi nyumbani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2010

    huyo mjinga aloweka rekodi za kumponda maximo lazima ni chadema,maana ndo kila kitu kwao mavi tu,hata ufanye nini wanapinga tu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2010

    We kenge, mbona mechi ya new zeland huitaji? Mechi tulizoshinda na kushiriki kwa wachezaji wa nyumbani husemi? Vijana wa Ghana wanavyofurahisha ni kwa kuwa watu wao ni wavumilivu kwa kocha na wamamwelewa. Sisi tutabakia kushangilia wengine na kujifanya wajuaje. Hapa hata aje wenger au mourinho, kazi bure tu. Sababu ya watu kama wewe.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2010

    Wabongo tumesahau kabisa mpira kabla ya Maximo ulivyokuwa mmbaya.Tatizo tunataka mabadiliko overnight kitu ambacho hakiwezekani. Lazima tujifunze kuandaa mafanikio kwa kupanga program za muda mrefu. Maendeleo ya jamii bongo yanapimwa na idadi ya maghorofa wakati miundo mbinu ni ya nyumba za udongo. Maandlizi ya wachezaji yanaanzia utotoni , si mazoezi tu bali hata lishe. Wachezaji walioshupaa kwa kukosa malazi hawana nafasi kwenye dunia hii ya leo ya michezo.
    Fungua macho.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2010

    maximo ameinua soka kiasi kwamba hata kenge said anafuatilia matokeo siku hizi ingawa anafuatilia matokeo mabaya tu, enzi za kichwa cha mwendawazimu alikuwa hafuatilii soka kabisa! kama anabisha mwambie atoe data nzuri za enzi ya kichwa cha mwandawazimu.

    The Brain.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2010

    Afadhali aondoke bwana, Serikali na Taasisi mbalimbali zilijitahidi kutoa misaada ya hali na mali lakini Maximo alishindwa kutufanya tujivunie taji angalau hata moja la ubingwa wa Afrika Mashariki katika kipindi cha miaka 4 aliyokaa Bongo. Hoja kwamba tulikuwa nyuma si sahihi, mbona zamani bila ya Maximo kombe la Afrika Mashariki tulikuwa tunachukua? Hakuna kitu alichofanya zaidi ya kuturudisha nyuma tu. Fedha zilizokuwa zinatolewa na Serikali na Taasisi kadhaa ndizo zilizokuwa zinaifanya timu kujikongoja siku moja moja. Katika kiwango cha FIFA tumeendelea kuporomoka kwa sababu ya ukuda wake Maximo.Mimi binafsi simfagilii kabisa. Ngoja tumuone kocha mpya kama hatokuwa mkuda kama Maximo tutafika tunakokutaka sisi tunaojua soka.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2010

    Nadhani huyu bwana ataikumbuka sana Tanzania kwa "uvumilivu" usiopimika, hasa baada ya kuona makocha wenzake waliofungwa ktk kombe la dunia wanavyofanya.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2010

    we anoy wa kwanza mwogope Mungu usitanganye umma Egypt hawajawahi kucheza na staz iliyofungwa 5 na timu ya egypt ni simba sc
    maximo nenda mwalimu nenda sisi waungwana tunakushukuru kabla yako hatukuijua hata jesi ya timu ya taifa lakini sasa kila anayeenda ulaya katika vitu anavyokumbuka kubeba ni pamoja na jesi ya timu ya taifa

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 01, 2010

    Si mfuatiliaji sana wa mpira wa Tz,sabu sipo hom kwa5yrs sasa,ila jinsi ambavyo nimekuwa nikiiskia Staz si sawa na nlipokuwa Tz,ya sasa naiskia most frequently in best ways even zoo niko far frm source of in4mations,naamini now2ko beta zan wher We wer b4zis Man kem,yes4sure!!
    Afu kuna jamaa anaongelea kuwa kipindi Serikali na Taasisi mbalimbali zinatoa misaada Staz ilikuwa fresh zoz tmz,sa'kwanini asiombe ukocha hata yeye ili akafanye kazi yenye mafanikio ya ushindi chini ya hizo fedha zen!!?
    Nakubaliana na wadau wanaokubali mafanikio since aje Maximoz!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 01, 2010

    Huyu bwana kwa kweli mimi naona amaeleta mabadiliko makubwa saaaana katika soka la nchi nchi yetu.kabla hajaja taifa stars ilikuwa ikiitwa kichwa cha mwendawazimu lakini alipokuja ,hata nchi zingine za Africa zilikiri kwamba soka yetu imebadilika na kupnda ghafla.Kwa hiyo ni bora tuwe waungwana na kudhamini mchango wa huyu bwana kwani ipo siku tutamkumbuka tuuu.Mtihani ni kwamba, je huyu kocha mpya ataendeleza libeneke mbele kwa mbele pale ambapo maximo ameepaachia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...