Mwanalibeneke mkongwe Maggid Mjengwa wiki hii amemtembelea ankal na kupata naye dina la mchana nyumbani kwake maeneo ya nanihii. Mjengwa ni mmoja wa wanalibeneke wa mwanzoni kabisa kutuleta habari mbalimbali za vijijini, hasa mkoani Iringa anakofanyia kazi za jamii.
Katika maongezi yao yaliyonoga sana Maggid na Ankal walifikia makubaliano ya kuanza mchakato wa kuunda chama cha Mabloga wa Tanzania katika mkakati wa kujenga umoja pamoja na kutetea maslahi ya wanachama pamoja na libeneke. Hivyo wana libeneke kaeni mkao wa kula chama chetu kinanukia na karibuni mkutano utaitishwa kuzungumzia mstakabali huu. mawazo na maoni yanakaribishwa kwa mikono miwili toka kwa wadau...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2010

    Manalibeneke = Mwanalibeneke!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2010

    Dolaman,
    T-shirt hiyo inabidi ipigwe mnada au ziko nyingi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2010

    Hivi hayo maji ya chupa yamefuata nini hapo mezani wakati kabati la baridi linajitosheleza, au ni kwa sababu ya mgao?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2010

    umetulia.... hiyo ketchup mbona huwa haina radha acha kubania pesa nunua heinz
    friji lako bomba hujachacha, natumaini ni la europe na sio china litakuchosha haraka

    unakula nini mbona sioni vizuri??????????????????//

    ReplyDelete
  5. mottoemma.blogspot.comJuly 15, 2010

    Naomba pia mgetushirikisha tunaomiliki blogs ambao tuko nje ya Tanzania

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 15, 2010

    ankal kama unakunywa maji ya chupa sasa jokofu la maji kwa kubonyeza la nini?

    Ankal pls mpe mjengwa interview ndogo atuelezee juu ya lile tukio la kukutana na simba ana kwa ana pale Mikumi.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 15, 2010

    eheee hapohapo, ebu tuonyeshe tu aliyepika hilo dinner la mchana namaanisha mother house!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 15, 2010

    sasa na hiyo laptop hina fanya nini mwezani au nayo hina liwa? kaka kwa kujifagilia hiwe photoshop tu hii

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 15, 2010

    Kaka Michuzi na Mjengwa kazi yenu inatusaidia sana hasa sisi wa ughaibuni. Naomba kaka Michuzi uwe neutral achana na kushabikia vyama vya siasa sababu havijengi. Sasa hivi watu wanapigwa risasi sijui unaweza kujua sababu? Hata ukijua huwezi sababu umeshaonyesha mwelekeo wako.

    ReplyDelete
  10. Wazo la kuanzisha chama cha wanablogu ni zuri sana na limeshagusiwa hapa na pale mara nyingi. Mlikomalie basi safari hii liwe kweli.

    Nategemea kwamba hata sisi wanablogu tunaobeba maboksi huku nje mtatushirikisha katika umoja huo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 15, 2010

    Hilo krokapoti la ubwabwa mpaka mezani. Kweli bongo tambalale kila mtu ajue ubwabwa umepikwa katik krokopoti sio jiko la mkaa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 15, 2010

    Mapazia gani hayo? Ukitokea moto hapo! Acha!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 15, 2010

    Ancal bwana!! Eti maeneo ya naniii!? Si useme tuu Maeneo ya kwa Binti kaenga kule kigogo mwisho!!
    Jirani yako Kindamba wa pale Bondeni make wewe uko kwa juu kidogo!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 15, 2010

    KAKA MICHU MWENZIO NIPO SIRIASI NAHITAJI STORY NZIMA YA JINSI KAKA MJENGWA ALIVYOKUTANA NA SIMBA ANA KWA ANA ILIKUWAJE? PLZ NAOMBA HIYO STORY LABDA ITANISAIDIA KISAIKOLOJIA MANAKE MIMI HATA NINAPOANGALIA PICHA ZA WANYAMA ANAPOTOKEA SIMBA TUU MWILI HUVUJA JASHO NAJARIBU KUIMAJINI SIKU NIKIKUTANA NAYE LIVE ALAFU NIKIWA KATIKA KILE KINACHOITWA KUTEMBEA KWA MIGUU MBUGANI.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 15, 2010

    Ankal mbona shangazi umemtenga au bado utamaduni ni ule wa wanawake kulia jikoni? Alitakiwa awepo mezani bwana mambo gani tena haya ankal!11

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 15, 2010

    sasa ankal hiyo ni hotipoti au kitu gani...halafu rangi haijametisha na friji...oops kumbe imemetisha na mapazia safi sana.....lakini mbona mboga chache sana au makande hayo???

    ReplyDelete
  17. Mdau, BloomsburyJuly 15, 2010

    Ankal,

    Inaelekea nyumba yako nzuri ila tu unahitaji kupamba kwa rangi zinazoshabihiana (co-ordination).

    Yaani hilo pazia la nylon la kijani limeniudhi!! Jamani Anko na kusafiri kote kweli umeweka pazia la aina hiyo? Hapo Dar unaweza kupata mapazia mazuri kabisa, kama vipi basi ukija tena Uingereza walau pita Primark (kama bei ni ishu) ujipatie

    Mdau uliesema krokapoti iko mezani, hiyo siyo rice cooker, ni hot pot la kuhifadhi joto kwenye chakula....ila tena ni la kijani, duh!

    ReplyDelete
  18. Kwanini isiendelezwe ile jumuiya ya wanablogu Tanzania

    http://blogutanzania.blogspot.com/

    Kwa muonekano kutakuwa na mlolongo wa vyama ambavyo mwisho wa siku vinaishia hewani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 15, 2010

    Misosi ya kibongo haina mboga, wali na mi kechap kibao. Unapozi na m-laptop wakati unakula, Michuzi wacha ushamba.

    ReplyDelete
  20. Mama WatotoJuly 15, 2010

    Duh! waosha vinywa wa blog hii mna visa,.. sasa mpaka kuingilia maisha ya ketchup ya mezani inahuuu! Ankal nyumba yako nzuri imetulia, tena safi wla hamna makorokoro mengi na ndivyo inavyotakiwa, achana na waosha vinywa waweke picha za nyumba zao tuone, tutaona mpaka mende na inzi!Midomo tu waone kwanza!Najua mtanisema lakini nishawazoea na usiku mtalala.,, msisahau kujifunika tu.

    Mama Watoto.

    ReplyDelete
  21. jamani wenzenu hawanywi maji ya bomba yaliyochemshwa wanakunywa mineral water ya klm...

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 15, 2010

    Kaka michuzi bwana, nilipishana na mtu Chefs Pride Hotel na hotpot kama hilo, nahisi hilo ni biriani toka chefs, hahahaaaaaa

    ReplyDelete
  23. Ni wazo zuri kuanzisha chama. Tuzidi kuwasiliana ili kama itawezekana chama kisimame kabla ya mwaka kuisha.
    Mdau
    Faustine
    drfaustine.blogspot.com

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 15, 2010

    loooo wadau hamna dogo?hahahaaa
    mie iyo ze fulanazzz na chakula aaaaah mwake,na mpiga picha apo ni mamsap au??hahahahaaa

    kumbe maggid ndo yuko ivo?okkkkk

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 15, 2010

    kaka misupu vyama kweli vizuri kwa ile maana halisi ya vyama lkn TZ hicho chama mnachotaka kuanzia huenda msifikie malengo kwa vile wengi wana notion ya lazima wachangiwe na chama chao michango ya harusi na misiba bila hivyo ataona chama hakina manufaa kwake!!!!toeni elimu kabla hamjaanza mchakato

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 15, 2010

    WE ANKAL MITHUPU MATATIZO SANA, HEBU TAZAMA SAHANI YAKO ILIVYO JAA NA YA MGENI WAKO KIDUCHU???
    HAAFU HOTI POTI, MAJI,TOMATO SOSI ZOTE UMEVUTIA KWAKO!!
    AKU, MIMI SIJI KUKUTEMBELEA BWANA

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 15, 2010

    Yaani hiyo nyumba inaonyesha kabisa haina maza house, hizo grill dirishani kweli unaishi kigogo mwisho hapo jamaa hawaingii, sasa jokofu linajitosheleza na maji vichupa hapo mezani vya nini? mbongo mbongo tu yaani anakal kusafiri kote safari za bure nje bado tu hujajifunza?? USINIBANIE siku moja moja lazma upate vidongo

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 15, 2010

    ankali ulaya hapa hapa DSM BONGO,ila wakati unajenga dinning uliifinya sana maana atakae kaa kiti hicho karibu na tembo hata akiwahi kumaliza kula lazima awe wa mwisho kunyanyuka uongo? azawaisi uko bomba

    ReplyDelete
  29. ZeroBrainJuly 15, 2010

    Kaka hilo limashine likubwa hapo kushoto yako pembeni ni yale ya kutengeneze AISHKRIMU za KONI?

    Kama ndio naomba nije kuzila, huwa nazipenda sana tafadhali

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 15, 2010

    ANKAL KUMBE WEWE NI JIRANI BLOCK 41. AISEE DUNIA NDOGO KWELI. HIYO NYUMBA NILIKUWA NACHEZA WAKATI NIKO MDOGO NA MPAKA LEO NAIKUMBUKA.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 15, 2010

    Nashukuru sana wanalibeneke kwa kazi nzuri sana mnayoifanya, naomba tu usiwasilkize hao makiritimba wa jokofu, T-shirt, majina n.k naomba pia hata kama unajuwa nyumbani kwa mtu siyo kazi yako kutangaza, naomba tufikirie kabla hujaandika. Je kunamtu ambae kweli anajuwa hata maji tunakunywa hapa nchini kwenye hizo chupa kweli yanatoka wapi? Mimi kuna mtu aliniambia mama chemsha maji ni salama zaidi kuliko hayo ya kwenye chupa. Mimi naomba mtu wa kunigahamisha kam kuna mtu anejuwa haya maji ya kama Kilimanjato na mengineyo yanatoka wapi yani chanjo chake. Pia naomba tuendelaa nakazi njema sana Kaka Michuzi mimi nakuunga mkono asilimia mia unachokifanya bali naomba utowe zaidi habari za %80 ya watanzania wanoishi vijijini pia kwani naona mambo mengi ni ya mjini zaidi, kwani kuna mengi hata nje tu kidogo ya Dar kona zote wananchi wengi wanapata shida lakini hatuoni maoni yao au kitu gani kinaendelea haswa ukingalia shunguli za maji, umeme , shule, hospitali na kadhalika. Nashukuru sana tena sana kwa uwezo wako na naomba uendelee kuutumia zaidi. Mungu akubariki sana.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 15, 2010

    Ankal,

    Nawapa hongera nyingi nyote wawili!! Hii ni hatua nzuri ya maendeleo na manufaa kwa wote.
    Mie naiunga mkono na niko tayari kuchangia kwa hali na mali.
    Shukran.
    Storming
    Mdau wa www.uksokainbongo.blogspot.com & www.sokainbongo.com

    ReplyDelete
  33. sokainbongoJuly 15, 2010

    Ankal,

    Ni hatua njema na yenye manufaa kwa wote!

    Pongezi zangu za dhati!

    Nipo tayari kutoa mchango wa hali na mali.

    Storming
    MDAU: www.uksokainbongo.blogspot.com
    [www.sokainbongo.com]

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 16, 2010

    wewe ndiyo mshamba hiyo ni hot pot bwana,kwa nini anunue heinz wakati dabaga halisi yake mtz hipo

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 16, 2010

    AHAAA! MJOMBA MBONA NYUMBANI KWAKO KUMEKAA KIKRITU-KRISTU.HATA KULA YAKO NI YA KIKRITU.
    HAYA BWANA.

    ReplyDelete
  36. Ankal kwa kula tu!

    ReplyDelete
  37. It is a nice move,but please Ankal and other motherland bloggers let embracing Link exchange with bongo's bloggers living in abroad so people at home can learn what happen in other angles of this planet..forinstance, i got your blog as my favourite blog coz my viewers will also be interested to see what happen in the motherland. advice not a demand Thanks Mdau Singida

    ReplyDelete
  38. Nimeipenda hiyo jokofu kwa nyuma tu..

    ReplyDelete
  39. Aminia babake ankal unatisha....harufu ya maakuli naisikia hadi hapa nilipo...ni pilao tu hilo! kule kwetu Mafia linaitwa "mpunga", Morogoro wakaguru wanaliita "mavi ya panya", nursery school wanaliita "cha ndege", au ukipenda liite "mpunyenye" na kwa bongo Darisalama linaitwa "mnuso". Poa ankal..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...