
Katika maongezi yao yaliyonoga sana Maggid na Ankal walifikia makubaliano ya kuanza mchakato wa kuunda chama cha Mabloga wa Tanzania katika mkakati wa kujenga umoja pamoja na kutetea maslahi ya wanachama pamoja na libeneke. Hivyo wana libeneke kaeni mkao wa kula chama chetu kinanukia na karibuni mkutano utaitishwa kuzungumzia mstakabali huu. mawazo na maoni yanakaribishwa kwa mikono miwili toka kwa wadau...
Manalibeneke = Mwanalibeneke!
ReplyDeleteDolaman,
ReplyDeleteT-shirt hiyo inabidi ipigwe mnada au ziko nyingi?
Hivi hayo maji ya chupa yamefuata nini hapo mezani wakati kabati la baridi linajitosheleza, au ni kwa sababu ya mgao?
ReplyDeleteumetulia.... hiyo ketchup mbona huwa haina radha acha kubania pesa nunua heinz
ReplyDeletefriji lako bomba hujachacha, natumaini ni la europe na sio china litakuchosha haraka
unakula nini mbona sioni vizuri??????????????????//
Naomba pia mgetushirikisha tunaomiliki blogs ambao tuko nje ya Tanzania
ReplyDeleteankal kama unakunywa maji ya chupa sasa jokofu la maji kwa kubonyeza la nini?
ReplyDeleteAnkal pls mpe mjengwa interview ndogo atuelezee juu ya lile tukio la kukutana na simba ana kwa ana pale Mikumi.
(US Blogger)
eheee hapohapo, ebu tuonyeshe tu aliyepika hilo dinner la mchana namaanisha mother house!
ReplyDeletesasa na hiyo laptop hina fanya nini mwezani au nayo hina liwa? kaka kwa kujifagilia hiwe photoshop tu hii
ReplyDeleteKaka Michuzi na Mjengwa kazi yenu inatusaidia sana hasa sisi wa ughaibuni. Naomba kaka Michuzi uwe neutral achana na kushabikia vyama vya siasa sababu havijengi. Sasa hivi watu wanapigwa risasi sijui unaweza kujua sababu? Hata ukijua huwezi sababu umeshaonyesha mwelekeo wako.
ReplyDeleteWazo la kuanzisha chama cha wanablogu ni zuri sana na limeshagusiwa hapa na pale mara nyingi. Mlikomalie basi safari hii liwe kweli.
ReplyDeleteNategemea kwamba hata sisi wanablogu tunaobeba maboksi huku nje mtatushirikisha katika umoja huo.
Hilo krokapoti la ubwabwa mpaka mezani. Kweli bongo tambalale kila mtu ajue ubwabwa umepikwa katik krokopoti sio jiko la mkaa.
ReplyDeleteMapazia gani hayo? Ukitokea moto hapo! Acha!
ReplyDeleteAncal bwana!! Eti maeneo ya naniii!? Si useme tuu Maeneo ya kwa Binti kaenga kule kigogo mwisho!!
ReplyDeleteJirani yako Kindamba wa pale Bondeni make wewe uko kwa juu kidogo!!
KAKA MICHU MWENZIO NIPO SIRIASI NAHITAJI STORY NZIMA YA JINSI KAKA MJENGWA ALIVYOKUTANA NA SIMBA ANA KWA ANA ILIKUWAJE? PLZ NAOMBA HIYO STORY LABDA ITANISAIDIA KISAIKOLOJIA MANAKE MIMI HATA NINAPOANGALIA PICHA ZA WANYAMA ANAPOTOKEA SIMBA TUU MWILI HUVUJA JASHO NAJARIBU KUIMAJINI SIKU NIKIKUTANA NAYE LIVE ALAFU NIKIWA KATIKA KILE KINACHOITWA KUTEMBEA KWA MIGUU MBUGANI.
ReplyDeleteAnkal mbona shangazi umemtenga au bado utamaduni ni ule wa wanawake kulia jikoni? Alitakiwa awepo mezani bwana mambo gani tena haya ankal!11
ReplyDeletesasa ankal hiyo ni hotipoti au kitu gani...halafu rangi haijametisha na friji...oops kumbe imemetisha na mapazia safi sana.....lakini mbona mboga chache sana au makande hayo???
ReplyDeleteAnkal,
ReplyDeleteInaelekea nyumba yako nzuri ila tu unahitaji kupamba kwa rangi zinazoshabihiana (co-ordination).
Yaani hilo pazia la nylon la kijani limeniudhi!! Jamani Anko na kusafiri kote kweli umeweka pazia la aina hiyo? Hapo Dar unaweza kupata mapazia mazuri kabisa, kama vipi basi ukija tena Uingereza walau pita Primark (kama bei ni ishu) ujipatie
Mdau uliesema krokapoti iko mezani, hiyo siyo rice cooker, ni hot pot la kuhifadhi joto kwenye chakula....ila tena ni la kijani, duh!
Kwanini isiendelezwe ile jumuiya ya wanablogu Tanzania
ReplyDeletehttp://blogutanzania.blogspot.com/
Kwa muonekano kutakuwa na mlolongo wa vyama ambavyo mwisho wa siku vinaishia hewani.
Misosi ya kibongo haina mboga, wali na mi kechap kibao. Unapozi na m-laptop wakati unakula, Michuzi wacha ushamba.
ReplyDeleteDuh! waosha vinywa wa blog hii mna visa,.. sasa mpaka kuingilia maisha ya ketchup ya mezani inahuuu! Ankal nyumba yako nzuri imetulia, tena safi wla hamna makorokoro mengi na ndivyo inavyotakiwa, achana na waosha vinywa waweke picha za nyumba zao tuone, tutaona mpaka mende na inzi!Midomo tu waone kwanza!Najua mtanisema lakini nishawazoea na usiku mtalala.,, msisahau kujifunika tu.
ReplyDeleteMama Watoto.
jamani wenzenu hawanywi maji ya bomba yaliyochemshwa wanakunywa mineral water ya klm...
ReplyDeleteKaka michuzi bwana, nilipishana na mtu Chefs Pride Hotel na hotpot kama hilo, nahisi hilo ni biriani toka chefs, hahahaaaaaa
ReplyDeleteNi wazo zuri kuanzisha chama. Tuzidi kuwasiliana ili kama itawezekana chama kisimame kabla ya mwaka kuisha.
ReplyDeleteMdau
Faustine
drfaustine.blogspot.com
loooo wadau hamna dogo?hahahaaa
ReplyDeletemie iyo ze fulanazzz na chakula aaaaah mwake,na mpiga picha apo ni mamsap au??hahahahaaa
kumbe maggid ndo yuko ivo?okkkkk
kaka misupu vyama kweli vizuri kwa ile maana halisi ya vyama lkn TZ hicho chama mnachotaka kuanzia huenda msifikie malengo kwa vile wengi wana notion ya lazima wachangiwe na chama chao michango ya harusi na misiba bila hivyo ataona chama hakina manufaa kwake!!!!toeni elimu kabla hamjaanza mchakato
ReplyDeleteWE ANKAL MITHUPU MATATIZO SANA, HEBU TAZAMA SAHANI YAKO ILIVYO JAA NA YA MGENI WAKO KIDUCHU???
ReplyDeleteHAAFU HOTI POTI, MAJI,TOMATO SOSI ZOTE UMEVUTIA KWAKO!!
AKU, MIMI SIJI KUKUTEMBELEA BWANA
Yaani hiyo nyumba inaonyesha kabisa haina maza house, hizo grill dirishani kweli unaishi kigogo mwisho hapo jamaa hawaingii, sasa jokofu linajitosheleza na maji vichupa hapo mezani vya nini? mbongo mbongo tu yaani anakal kusafiri kote safari za bure nje bado tu hujajifunza?? USINIBANIE siku moja moja lazma upate vidongo
ReplyDeleteankali ulaya hapa hapa DSM BONGO,ila wakati unajenga dinning uliifinya sana maana atakae kaa kiti hicho karibu na tembo hata akiwahi kumaliza kula lazima awe wa mwisho kunyanyuka uongo? azawaisi uko bomba
ReplyDeleteKaka hilo limashine likubwa hapo kushoto yako pembeni ni yale ya kutengeneze AISHKRIMU za KONI?
ReplyDeleteKama ndio naomba nije kuzila, huwa nazipenda sana tafadhali
ANKAL KUMBE WEWE NI JIRANI BLOCK 41. AISEE DUNIA NDOGO KWELI. HIYO NYUMBA NILIKUWA NACHEZA WAKATI NIKO MDOGO NA MPAKA LEO NAIKUMBUKA.
ReplyDeleteNashukuru sana wanalibeneke kwa kazi nzuri sana mnayoifanya, naomba tu usiwasilkize hao makiritimba wa jokofu, T-shirt, majina n.k naomba pia hata kama unajuwa nyumbani kwa mtu siyo kazi yako kutangaza, naomba tufikirie kabla hujaandika. Je kunamtu ambae kweli anajuwa hata maji tunakunywa hapa nchini kwenye hizo chupa kweli yanatoka wapi? Mimi kuna mtu aliniambia mama chemsha maji ni salama zaidi kuliko hayo ya kwenye chupa. Mimi naomba mtu wa kunigahamisha kam kuna mtu anejuwa haya maji ya kama Kilimanjato na mengineyo yanatoka wapi yani chanjo chake. Pia naomba tuendelaa nakazi njema sana Kaka Michuzi mimi nakuunga mkono asilimia mia unachokifanya bali naomba utowe zaidi habari za %80 ya watanzania wanoishi vijijini pia kwani naona mambo mengi ni ya mjini zaidi, kwani kuna mengi hata nje tu kidogo ya Dar kona zote wananchi wengi wanapata shida lakini hatuoni maoni yao au kitu gani kinaendelea haswa ukingalia shunguli za maji, umeme , shule, hospitali na kadhalika. Nashukuru sana tena sana kwa uwezo wako na naomba uendelee kuutumia zaidi. Mungu akubariki sana.
ReplyDeleteAnkal,
ReplyDeleteNawapa hongera nyingi nyote wawili!! Hii ni hatua nzuri ya maendeleo na manufaa kwa wote.
Mie naiunga mkono na niko tayari kuchangia kwa hali na mali.
Shukran.
Storming
Mdau wa www.uksokainbongo.blogspot.com & www.sokainbongo.com
Ankal,
ReplyDeleteNi hatua njema na yenye manufaa kwa wote!
Pongezi zangu za dhati!
Nipo tayari kutoa mchango wa hali na mali.
Storming
MDAU: www.uksokainbongo.blogspot.com
[www.sokainbongo.com]
wewe ndiyo mshamba hiyo ni hot pot bwana,kwa nini anunue heinz wakati dabaga halisi yake mtz hipo
ReplyDeleteAHAAA! MJOMBA MBONA NYUMBANI KWAKO KUMEKAA KIKRITU-KRISTU.HATA KULA YAKO NI YA KIKRITU.
ReplyDeleteHAYA BWANA.
Ankal kwa kula tu!
ReplyDeleteIt is a nice move,but please Ankal and other motherland bloggers let embracing Link exchange with bongo's bloggers living in abroad so people at home can learn what happen in other angles of this planet..forinstance, i got your blog as my favourite blog coz my viewers will also be interested to see what happen in the motherland. advice not a demand Thanks Mdau Singida
ReplyDeleteNimeipenda hiyo jokofu kwa nyuma tu..
ReplyDeleteAminia babake ankal unatisha....harufu ya maakuli naisikia hadi hapa nilipo...ni pilao tu hilo! kule kwetu Mafia linaitwa "mpunga", Morogoro wakaguru wanaliita "mavi ya panya", nursery school wanaliita "cha ndege", au ukipenda liite "mpunyenye" na kwa bongo Darisalama linaitwa "mnuso". Poa ankal..
ReplyDelete