Ma DJ wakongwe nchini Seydou Mukandara (kati) na John Peter Pantalakis wakiwa na Kaka Muddy wakati wa onesho la Old Skul halisi viwanja vya Karimjee hall jijini Dar usiku wa kuamkia leo
wakongwe wa muziki wa dansi nchini katika picha ya pamoja baada ya onesho lao la Old Skul usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Karimjee hall jijini Dar. Onesho hilo lililofana sana linatarajiwa kuwa tukio la kila mwaka ili kuwakutanisha wakongwe na pia kuonesha njia vijana wa leo kuhusu nini cha kufanya katika kuendeleza libeneke
abou semhando 'Baba Diana' akikaanga chipsi zake

mkongwe wa tumba Ali Jamwaka akiwajibika
wakongwe jukwaani
hapa toka shoto ni Shabani Lendi, Yusufu Joseph,

Mafumu Bilali Bombenga, Saidi Mabera na Juma Ubao

Toka shoto ni Shabani Lendi, Yusufu Joseph, Mafumu Bilali Bombenga, Saidi Mabera, Muhidin Maalim Gurumo, Kikumbi Mwanza Mpango King Kikii, Kabeya Badu na Hassan Rehani Bitchuka 'Super Stereo

Toka shoto ni Abdul Salvador 'Key-devu' Komandoo Hamza Kalala na Saidi Mabera

Mdau wa Chelsea Club ya Helsinki (kuume) akiwa na mdau

Vijana wa zamani kibao walikuwepo
Nyuzi bin nyuzi zikipishana. Hapo ni Hamza Kalala, Saidi Mabera na Juma Ubao. Nyuma yao ni mchawi wa kupiga kinanda Abdul Salvador 'Key-devu'.
Mratibu wa onesho Waziri Ally (kuume) akiwa na

Ma-DJ wakongwe John Peter Pantalakis (shoto) na Neagre Jay

Wakongwe Komandoo Hamza Kalala na King Kikii wakibadilishana mawazo huku Bi. Shakila Saidi akiwa amebana pembeni

Wakongwe kabla ya onesho kuanza. Toka shoto ni Komandoo Hamza Kalala, Kaka Muddy,
Yusuf Joseph, Juma Ubao na DJ Neagre Jay aliyekuwa MC wa shughuli hii

Mkongwe John Kitime na DJ Neagre Jay
Vijana wa zamani wakiburudika na Old Skul ya kufa mtu
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2010

    wapi mzee gurumo kasongo mpinda bichuka,kasim mapili kankukeli,ama mmechaguana ?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2010

    Huyo DJ Jay kama Masoud Masoud !!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2010

    wee ananoy wa kwanza sio kabisa bichuka mbona yupo? Halafu mbona kama watu walikuwa wachache? weka kideo cha youtube basi tuburudike wabeba box

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2010

    This is the only thing I can say I HAVE MISSED BEING OUTSIDE TANZANIA. TRUE MUSIC, TRUE TALENTS, TRUE LEGENDS. tO HELL WITH BONGO FLEVA NONSENCE.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2010

    Mswahili utamjua mazuri yote hayaoni anatafuta mabaya. Gurumo alikuweko,Bichuka alikuweko, Kelly yuko nje ya nchi, na si rahisi wakongwe wote kuwepo....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2010

    wapi John kitime mnene wa Jodanah kama nakuona vile unavyopenda raha.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2010

    Masikitiko kwa sisi tuliokuwa mbali haya si mambo ya kuyakosa,hata hivyo nimefurahi kuwaona vijana wenzangu wa zama za kale,hapakukosekana zaidi ya ndugu zetu marehemu waliotutangulia.
    Nakuona balozi John Kitime na DJ John Peter`s umenikumbusha mbali wapi dada Jullie Peters wangu zilipendwa kama bado yupo mpe salaam zangu mwambie kama bado anaikumbuka "Sea View Disco ya 70`s" santuri zilipigwa mpaka asubuhi ndiyo tunatoka kuitafuta UDA ya Kinondoni/Mwananyamala.

    OLD SKULL ipangwe tena nasi wadau tulio mbali na nyumbani tupate nafasi ya kufurahia tukirudi.

    Mickey Jones

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2010

    Je yuko wapi mtaalamu wa solo guitar Shaban Yohana"Wanted"

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2010

    anony Thu Jul 08, 04:07:00 PM unayesema dj jay kama masoud masoud inaelekea bayankata hukuyakuta mjini.
    ni dj neagre jay na sio dj jay.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2010

    Hongereni sana wakongwe tamasha kama hili lingekua linafanyika mara kwa mara lingejenga na kuimarisha msingi mkubwa wa mziki
    kwa wanamziki wa kisasa na pia washabiki,hongereni sana tunawatakieni mafanikio mema na maisha marefu
    Wadau
    "The Ngoma Africa band" aka FFU
    Ujerumani

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2010

    Ningeshauri hao wazee waendeleze libeneke kwa kubadili genre ya muziki.

    Wajifunze namna ya "transfer of learing" kwa kujiunga kutuburudisha na genre ya Jazz - after all, bendi zao nyingi zinajulikana kwa jina la "...Jazz Band."

    Wanayo nafasi ya kuzidi kututumbuiza (hata kwenye mahoteli mengi ya utalii), ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kusshiriki popote duniani!

    Jazz ni muziki wa wazee wa kazi!

    (Born Again Pagan)

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 08, 2010

    Hebu tukumbushane nyimbo za king kiki na hamza kalala sikiimba ulikua wapi...

    weweee those were the days...Nilikua nikisikia kipindi kinaanza cha wafanyakazi basi ndio naenda kuoga niwahi class .

    Hiyo ndio miziki ya kukuzwa...

    Hongera waliofanya haya mambo...muwe mnafanya kila miaka na record zenu muziuze tena jamani...mimi nitanunua hizo saaana tu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 09, 2010

    John Peter alikuwa jirani yangu huko Mwananyamala A. Nasikia mshkaji wake Choggy sly alifariki(RIP).John na dada zake akina Jackie na July!.John alikuwa Bitozi babkubwa enzi hizo na akina Moshi Majungu(aliyekuwa mchezaji wa Yanga),unajua tena mambo ya Rungwe oceanic.Jamani tumetoka mbali,siku hizo ukiwa na jeans basi utapata madem kibao!.

    ReplyDelete
  14. Michuzi ee,

    Mbona simuoni PARASHI hapo?

    Lukumbule Lulembo Parash.

    "...ufitinaaa, na upelelzi ni sumu ya mapeeeenzii,
    Ufitinaaaaaaa, na upelelzi ni sumu ya mapenzi,

    Mimi kupendwa yeye...."

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 09, 2010

    Hii inanikumbusha enzi hizo maeneo ya Bukoba wali kilikuwa ni chakula adimu sana, kilikuwa kinaliwa xmas na iddi-el-fitri. ukipikwa hata baba hatoki mpaka kieleweke.

    Nkyabo- Bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...