JK akimpongeza Dr Raphael Mwita Akiri Askofu wa kwanza wa Dayosisi mpya ya Tarime ya Kanisa la Kianglikana Tanzania muda mfupi baada ya sherehe za kumsimika askofu huyo zilizofanyika mjini Tarime leo asubuhi.Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania Askofu Valentino Mokiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. MHESHIMIWA KIKWETE HONGERA KWA KULIONGOZA TAIFA.

    NAFAHAMU KUWA MUDA WA KAMPENI UMEWADIA SASA LAKINI NINACHOSHANGAA NI KUONA UMEELEMEA KUPIGA KAMPENI KATIKA MAKANISA .NA WALA HATUJAKUONA KUPITA MISIKITINI KUONANA NA VIONGOZI WA KIISLAM.

    FAHAMU KUWA WAPIGA KURA NI WATU WA DINI ZOTE,USIJISAHAU NA UKAELEMEA UPANDE MMOJA MHESHIMIWA.

    TUNAHITAJI CHAPO KUONA PHOTO OP NA VIONGOZI WA KIISLAMU.

    mUHIDINI UKIBANIA UJUMBE HUU TUTAFAHAMU KUWA NAW E NI...........

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2010

    we sedouf ebu acha udini una mambo ya ajabu kichwani kama sio nyenyere, uliambiwa kikwete alikwenda kupiga kampeni huko? si alialikwa kwa ajili ya kusimikwa askofu sasa mambo ya kampeni yametokea wapi?? yani wewe ni mdini mkubwa kwa taarifa yako hakuna dini bora duniani kama unavyodhani, dini safi ni kutazama wagonjwa, kusaidia yatima na wajane, wasiojiweza na kutotenda dhambi full stop hayo mengine dini ni nyongeza tu. kama viongozi wenu hawamualiki ulitaka ajilazimishe kuja? ukome kukurupuka hatuvutiwi na hayo mambo ya udini manake yanaendekeza chuki tu, badala ufikirie jinsi nchi yetu itakavyojikwamua kwenye umaskini huu ualeta udini kazi ipo.

    ReplyDelete
  3. Hyo maelezo yako ya dini bora ni maneno ya "kichaa"

    Hapa hakuna mtu aliyetaja udini wala kufarakisha dini na watanzania .

    Hapa kilichozungumzwa ni usawa wa kiongozi wa nchi katika kuwafikia raia zake ambao wapo waislamu,wakiristo na hata wasiokuwa na dini.


    Nilichokilalamikia ni kuwa Rais ameonekana kuelemea upande mmoja tu kuwafikia wananchi.

    usitake kunambia kuwa hapa Rais kaalikwa tu!!amka wewe huu ni wakati wa uchaguzi!

    Kuhusu Rais "kutoalikwa" na waislamu ,pia hilo ni kosa la Rais,maana Rais ana wafanya kazi wake maalum ambao huwa wana mikakati kama hii ya kumkutanisha na wananchi wake.

    Wanachi wenye imani ya KIISLAM wanamuhitaji rais wao hususan wakati huu kuelekea uchaguzi.

    Mheshimiwa Rais usisubiri Mualiko waislamu wana kiu kubwa ya kukutana nawe,watafute kama unaona wamechelewa kukutafuta!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2010

    Sedouf umelemaa akili tu kubali yaishe. Kila ijumaa yuko huko msikitini sasa unamtaka aende wapi tena? Si mnakutana huko kwenye misikiti? Unalotaka kumwambia baaada ya swala mfuate umweleze na Kama hamumpigi picha mkazileta huku kwa michuzi nani wakulaumiwa? Msione muislamu anaongea na wakristo basi mnazania anabadilishwa dini...Huyo aliyyesema hapo juu kasema yote sina la zaidi...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2010

    sedouf umechanganyikiwa unahitaji msaada yaelekea we ni king'ang'a, ati wananchi wenye imani ya kiislam wanamhitaji rais wao mh??? mjahidina utawajua tu kwa maneno yao,
    kwaheri

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2010

    Sedouf amewakilisha hisia za watanzania wengi. Tunasema "ukabila" haupo Tanzania lakini baadhi yetu hatutaki undugu na makabila mengine.

    Hii sasa ya dini ni "halali" kwani sera ya nchi iliua makabila kiasi kwamba sasa watanzania hata wa miaka 30 wengine hawawezi kuzungumza lugha zao za asili. KISWAHILI KITUKUZWE????

    Kwa wabaguzi udini upo hai Tanzania zaidi ya ukabila. Ndio maana ni vigumu kwa Tanzania kuwa na Rais kutoka dini moja mfululizo. Akitoka Mkristo anaingia Muislamu... Wahindi na wengineo hatuwahesabu sijui ni ubaguzi???

    Hii hapa imekaaje...
    Nyerere Mkristo...
    Mwinyi Muislamu
    Mkapa Mkristo
    Kikwete Muislamu

    Kwa hiyo kwa kufuata ubaguzi huu Rais atakayefuata 2015 atakuwa Mkristo labda tukivunja ubaguzi huu wa kidini... ni jadi yetu. Na tukiacha hilo wengi wetu wagumu kuruhusu ndugu zao kuolewa kwenye dini tofauti au nimekosea wadau? Udini upo hai katika jamii ya kitanzania.Watu wapenda amani tunapaswa kukumea ubaguzi wowote ule iwe ni kidini, kikabila etc. Tukianza kubagua mwishowe watoto wetu pia tutawabagua... na haitaishia hapo. UBAGUZI UNATISHA!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2010

    MHESHIMIWA KILA IJUMAA YUPO MSIKITINI. ZAIDI KAMPENI AMEFANYA VIZURI NA MANENO MAZURI YANYOPITA KATI YETU KWENYE MISKITI NI KUWA AWAMU YAKE YA PILI TUTAPATA MAHAKAMA YA KHAZI; TUNAMPONGEZA SANA KWA HATUHII MUHIMU YA MAENDELEO YA TANZANIA, HUSUSANI WAISLAMU, NASI TUNAKUWA KATIKA KIWANGO CHA KUTENDEANA HAKI KWA KUFUATA KANUNI AMBAZO WENZETU WA IRAN, AFGHANSTAN, SUNDAN NA SEHEMU KAZI HIZO WANAVYOPATA HAKI ZAO. ASANTE SANA SHEKHE MKUU SIMBA KWA CHANGAMOTO ULIYOMPATIA RAIS WETU MPENDWA CHANGUAO LA MUNGU,
    THAKIBIL

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...