Waliofikishwa mahakamani hapo ni mhasibu wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Marcus Masila na Mtunza Fedha wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), Joyce Mwamagemo kwa tuhuma za kughushi nyaraka, kusafirisha pesa na kujipatia zaidi ya sh bilioni 3 mali ya kampuni hiyo.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Dickson Maira, Robert Mbweta, Gideon Otullo, Fortunatus Muganzi na Maryah Hostine, walipandishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mgeta, kujibu makosa 54 ya awali kwa watuhumiwa sita na mengine 23 kwa watuhumiwa wanne.Katika mashitaka 54.
Akiwasomea mashitaka katika kesi ya pili, watuhumiwa Marcus Masila, Dickson Maira, Robert Mbweta na Gideon Otullo, Wakili Lincoln alidai washitakiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kula njama, kughushi baadhi ya vyeti pamoja na makosa mawili ya kusafirisha pesa na kujipatia zaidi ya sh bilioni 3.
Mwendesha mashitaka alidai watuhumiwa walijipatia kiasi hicho cha pesa kutoka kwenye akaunti za kampuni mbalimbali zilizopo katika Benki za Barclays, CRDB, Standard Chartered na Kenya Commercial Bank (KCB), kwa kupitia akaunti ya TUCTA na ile ya TTCL.
Washtakiwa sita wanatuhumiwa kwa makosa ya kughushi nyaraka na moja la kusafirisha pesa ‘money laundry’ na kujipatia zaidi ya sh mil. 800.
Washtakiwa sita wanatuhumiwa kwa makosa ya kughushi nyaraka na moja la kusafirisha pesa ‘money laundry’ na kujipatia zaidi ya sh mil. 800.
wakati mtuhumiwa Joyce Mwamagemo anatuhumiwa kwa makosa 46, ya kughushi nyaraka na kuwasilisha hati feki kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwenye akauti za kampuni mbalimbali zilizopo katika benki zikiwamo za CRDB na NBC.
Akisoma hati ya mashitaka, Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln, alidai washitakiwa sita kwa pamoja wanatuhumiwa katika shitaka la nane la kusafirisha pesa, walilofanya kati ya Juni 30 na Agosti 29, mwaka 2008 jijini Dar es Salaam.
Washitakiwa wote wamerudishwa rumande kutokana na kosa hilo kutokuwa na dhamana hadi agosti 8 kesi yao itakapotajwa tena.
Bad oWazungu na Wahindi wale wanaoiba Nchini hapa na Vigogo ambao wapo serikalini na wanautumikia Serikali vbaya.
ReplyDeleteNaonea buji tu, bona simba naogopa.
ReplyDeletesiamini, mapak 3b zinibiwa walikuwa wapi miaka yote hiyo?
ReplyDeletehawa kafara tuuu.
HII YOTE INATOKANA NA WATU WENGI KUISHI BEYOND THEIR MEANS KIASI KWAMBA INAWATAMANISHA WATU WENGINE KUFANYA KAMA WAO, HAYA NDO MADHARA YAKE. KAMA WATU WANAJUWA FULANI YUKO SERIKALINI NA KIPATA CHA SERIKALI KINAJULIKANA LAKINI ANA NYMBA YA GHORFA NA MAGARI KIBAO NA KILA SIKU KWA MAMA CHOMA YA BILA KIPATO CHA ZIADA CHA HALALI AU HAJAKOPA MAHALA POPOTE KIHALALI HIYO NI RAHISI PIA KU=RECRUIT WATU NAO WAKAENDA NJIA MOJA NA YEYE, NDI HILO LILOLTOKEA LA WATU KUJIUNGA KATIKA WEZI SIMPLY THEY WANT TO LIVE BEYOND THEIR FINANCIAL POWER, KUNA TAKIWA VITA YA MAKUSUDI MAZIMA YA KUPAMBANA NA WIMBI ZIMA LA UFUSADI NA RUSHWA ILI KUSAFISHA TABIA HII YA WIZI NA WATU TUISHI NDANI YA UWEZO WETU RUSHWA
ReplyDeleteWADAU WAZIPIGA LAIVU, MWANANYAMALA
ReplyDelete******************************
MUJOMBA ISSA MUHIDIN MICHUZI,BWANA MIMI NAKUONYA NA KAMA WEWE NI MUTU WA KUSIKIA USIKIE. USIWEKE ATIKO ZA NABII ZA YOHANA MASHAKA KWENYE HII BULOGU YAKO. KWANI LEO WATU WAMEZICHAPA KIKWELIKWELI PALE MWANANYAMALA KWENYE BAA. WALIKUWA WANAJADILI VIJANA WAKALI SANA NJE NA NDANI YA INCHI. SASA WENGINE WAKAANZA KUBISHA KWAMBA ZITTO NI MKALI KULIKO MASHAKA NA KUNDI LA MASHAKA NALO LIKAWA ALITAKA KUAMBIWA, BASI HAPO NDO NGUMI ZIKAANZA JAMAA WAWILI WAKAPIGANA KWELI KWELI, BILA SISI KUWEPO WANGUMIZANA. KWA HIYO MICHUZI KUANZNIA LEO TUNAOMBA USIWEKE MAKALA YA JOHN MASHAKA KWA MAANA JAMAA NI KONTREVESHO SANA KWENYE HII NCHI AKAE HUKO HUKO MAREKANI ASIRUDI HAPA NA VIZUNGU VINGI VYA KUOKOTA BWANA.
% Naona mngeanza na MIJIFISADI PAPA! Sio kuonea hivi VIJIDAGAA tuu!
ReplyDelete% Mngesafishana woooote kwanza, mlioko kwenye system! I am talking to 'YOU'!
% For those of you who 'CAN'T READ WITHOUT YOUR GLASSES', muisome hiyo, japo KIMYA KIMYA!
% TIME IS ALL YOU HAVE!
% MJIFUNZE KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI!
% STAY TUNE FOR MORE!
% WATAKAORUDI VIJIJINI MBONA WENGI MWAKA HUU!
% %%% I AM KEEPING MY MOUTH SHUT BUT MY EYES WIDE OPEN!
% IT IS TIME FOR ......!
% IKIRUDI PANCHA HIYO!
Wabongo bwana ...wenye pesa wengi wao wanaiba...tofauti ni kwamba some are smarter than others
ReplyDeletemabilionea hawa mbona wamechoka?
ReplyDeleteMashaka
Jamani ii inji?! Kwani si waambiwe tu warudishe pesa halafu wataachiliwa? Au ni kwa kuwa wao ni wamatumbi?
ReplyDeleteKama memori yangu inanihudumia vyema, kuna kipindi wadosi waliachiwa/walisamehewa baada ya kurudisha paasenti flani ya zile pesa walizozichotaga kwa kuEPA?
dayasipora daamu
Jamani ii inji?! Kwani si waambiwe tu warudishe pesa halafu wataachiliwa? Au ni kwa kuwa wao ni wamatumbi?
ReplyDeleteKama memori yangu inanihudumia vyema, kuna kipindi wadosi waliachiwa/walisamehewa baada ya kurudisha paasenti flani ya zile pesa walizozichotaga kwa kuEPA?
dayasipora daamu
we acha za kuleta eti wanapigania atiko za mashaka?
ReplyDeleteYeye anatafuta umaarufu kwa kupitia mlango mbovu sana? mwambieni akajipime kwa Lakailo huko Rorya aone ndipo aache kujiita nabii au sijui rais wa wapi!
Mwizi anamkamata mwizi kazi ipo wafungwa msijali kwa kuwa wote tu wezi mtarudi tu nyumbani kama wale wengine ambao wapo majumbani mwao wameweka miguu juu. Sisi wakulima na walala hoi ndiyo hata maji ya kupikia watoto hatuna.
ReplyDeleteMie sidhani kama wana kosa.. hawa wanaiga mabosi wao. kamateni mabosi kwanza ... mbona mnaogopa. Matajiri wooooooote nchi hii ni wezi. Hakuna mTZ hata mmoja mwenye mshahara wa kujenga majumba ya kifahari, na magari ya kifahari.... labda wafanya biashara tu, lakini nao vile vile hudhurumiana na kutumia ushirikina..Hawa waacheni tu kamata kwanza walioanza kutuhumiwa then hawa.
ReplyDeleteuhhhh what is this? yani wanakaa kujishuhurisha na hawa vii billion 3 wakina richmond na mafisadi wengine wako wapi?mbona hatuoni wa epa hapa?.serikali yetu is so unfair.kama serikali is trying to win back our trust waache ku deal na hawa unknown ambao wameshawishika kuiba kutokana na mifano wanayoona kutoka kwa wakuu wetu...wale wote MAFISADI waliokuwa na majina makubwa they prove to be untouchable should be dealt with na hapo ndiyo wananchi tutaamini serikali tena other wise upuuzi mtupu
ReplyDeletenaomba mnisaidie, hivi mhasibu anaweza 'kuprocess' kila kitu mpaka pesa ikatoka bila kumhusisha bosi wake. Nafikiri kuna haja ya ya kuwaunganisha mabosi. Please polisi fanyeni kazi yenu, acheni woga.
ReplyDeleteNkyabo - Bongo
Mm! Tangu mwaka 2008 ndo wanastuka leo,muda woote huo walikuwa wapi.Oky nlkuwa nmesahau kumbe uchaguzi iz around the corner! Ila thakx God hamna mchaga hata mmoja coz watu wangezusha ndo tabia yao!kalagabao
ReplyDeleteBro misupu usinibanie commet yangu!
Genius wa kitaa
Halafu bado mnasema waChagga wezi?
ReplyDeleteKila kabila lina wezi.
Pia, hii mbona sasa kama mchezo wa kuigiza? Hizo bilioni 3 tu wataandamwa wee, halafu warushwe lupango. Lakini akina Chenge, Mramba, Yona na kadhalika wataambiwa warudishe tu taratibu
Hawa sio vidagaa. Bilioni 3 ni nyingi sana.
ReplyDeleteWatanzania wana Tamaa ya kuishi maisha ya juu huku hakuna means za ku support maisha ya juu.
Magari Mazuri, Majumba mazuri. Ukiwatazama elimu hakuna !!
Mawaziri wenyewe ukiwaangalia hawana elimu.
Hii imekuwa ni nchi ya wasanii!
Duh me sishangai sana ndo mambo yenyewe hayo ya kila siku huko makwetu.kinachonisikitisha zaidi ni kuona mahakama na polisi wamesahaulika,majengo ni ya kutisikitisha,itakuwa vp hawa watu mishahara yao?kama imeshindikana kujenga huko,sheria haki haitakwenda na ndo maana tunasikia kila kukicha ngoma zinapepea na kusahaulika,watu wameshakula chao hapo.Jamani Tz tuamke.Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
ReplyDeleteMwenye miwani anaitwa Robert tulimaliza nae form 4 Azania mwaka 1998 ni kijana mtaratibu sana pole ndg yangu yataisha katika maisha misukosuko haikosekani
ReplyDeleteBONGO SIRUDI HATA NIKISIKIA YESU KARUDI BONGO .HATARUDI YEYE MI NO .
ReplyDelete"Money laundry"....kicheko kicheko kicheko...hivi vimombo...mie sisemi...
ReplyDeleteHapo sioni sura ya billioneaz
ReplyDeleteHawa ni kafara tu
bongo kuna uonevu jamani!wapi big fish?wanaonewa watu ambao wametumiwa tu tena wengine bila kujua
ReplyDeleteHii yote sineme ya 2010, ama kweli uchaguzi unatia wazimu.......hebu serikali ikaangalie ni jinsi gani itasaidia amabao hawajawahi kuona umeme wa TANESCO maishani mwao badala ya kupoteza hela kufuatilialia kesi za kusimuliwa." hadithi hadithi... hapo mwaka 2008... eeeh...." achane hizo bwana tunaakili siku hizi. Alaaaah
ReplyDelete