watuhumiwa wakisubiri kusomewa mashtaka leo
Juu na chini watuhumiwa wakifikishwa mahakamani


Jumla ya watuhumiwa 7 wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakamaya Kisutu, Dar es Salaam, leo wakikabiliwa na makosa 54 ya kughushi nyaraka na kujipatia kiasi cha zaidi ya biloni 3 mali ya kampuni ya simu TTCL .

Waliofikishwa mahakamani hapo ni mhasibu wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Marcus Masila na Mtunza Fedha wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), Joyce Mwamagemo kwa tuhuma za kughushi nyaraka, kusafirisha pesa na kujipatia zaidi ya sh bilioni 3 mali ya kampuni hiyo.

Watuhumiwa wengine ni pamoja na Dickson Maira, Robert Mbweta, Gideon Otullo, Fortunatus Muganzi na Maryah Hostine, walipandishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mgeta, kujibu makosa 54 ya awali kwa watuhumiwa sita na mengine 23 kwa watuhumiwa wanne.Katika mashitaka 54.

Akiwasomea mashitaka katika kesi ya pili, watuhumiwa Marcus Masila, Dickson Maira, Robert Mbweta na Gideon Otullo, Wakili Lincoln alidai washitakiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kula njama, kughushi baadhi ya vyeti pamoja na makosa mawili ya kusafirisha pesa na kujipatia zaidi ya sh bilioni 3.
Mwendesha mashitaka alidai watuhumiwa walijipatia kiasi hicho cha pesa kutoka kwenye akaunti za kampuni mbalimbali zilizopo katika Benki za Barclays, CRDB, Standard Chartered na Kenya Commercial Bank (KCB), kwa kupitia akaunti ya TUCTA na ile ya TTCL.

Washtakiwa sita wanatuhumiwa kwa makosa ya kughushi nyaraka na moja la kusafirisha pesa ‘money laundry’ na kujipatia zaidi ya sh mil. 800.

wakati mtuhumiwa Joyce Mwamagemo anatuhumiwa kwa makosa 46, ya kughushi nyaraka na kuwasilisha hati feki kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwenye akauti za kampuni mbalimbali zilizopo katika benki zikiwamo za CRDB na NBC.

Akisoma hati ya mashitaka, Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln, alidai washitakiwa sita kwa pamoja wanatuhumiwa katika shitaka la nane la kusafirisha pesa, walilofanya kati ya Juni 30 na Agosti 29, mwaka 2008 jijini Dar es Salaam.

Washitakiwa wote wamerudishwa rumande kutokana na kosa hilo kutokuwa na dhamana hadi agosti 8 kesi yao itakapotajwa tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2010

    Bad oWazungu na Wahindi wale wanaoiba Nchini hapa na Vigogo ambao wapo serikalini na wanautumikia Serikali vbaya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2010

    Naonea buji tu, bona simba naogopa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    siamini, mapak 3b zinibiwa walikuwa wapi miaka yote hiyo?

    hawa kafara tuuu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    HII YOTE INATOKANA NA WATU WENGI KUISHI BEYOND THEIR MEANS KIASI KWAMBA INAWATAMANISHA WATU WENGINE KUFANYA KAMA WAO, HAYA NDO MADHARA YAKE. KAMA WATU WANAJUWA FULANI YUKO SERIKALINI NA KIPATA CHA SERIKALI KINAJULIKANA LAKINI ANA NYMBA YA GHORFA NA MAGARI KIBAO NA KILA SIKU KWA MAMA CHOMA YA BILA KIPATO CHA ZIADA CHA HALALI AU HAJAKOPA MAHALA POPOTE KIHALALI HIYO NI RAHISI PIA KU=RECRUIT WATU NAO WAKAENDA NJIA MOJA NA YEYE, NDI HILO LILOLTOKEA LA WATU KUJIUNGA KATIKA WEZI SIMPLY THEY WANT TO LIVE BEYOND THEIR FINANCIAL POWER, KUNA TAKIWA VITA YA MAKUSUDI MAZIMA YA KUPAMBANA NA WIMBI ZIMA LA UFUSADI NA RUSHWA ILI KUSAFISHA TABIA HII YA WIZI NA WATU TUISHI NDANI YA UWEZO WETU RUSHWA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2010

    WADAU WAZIPIGA LAIVU, MWANANYAMALA
    ******************************

    MUJOMBA ISSA MUHIDIN MICHUZI,BWANA MIMI NAKUONYA NA KAMA WEWE NI MUTU WA KUSIKIA USIKIE. USIWEKE ATIKO ZA NABII ZA YOHANA MASHAKA KWENYE HII BULOGU YAKO. KWANI LEO WATU WAMEZICHAPA KIKWELIKWELI PALE MWANANYAMALA KWENYE BAA. WALIKUWA WANAJADILI VIJANA WAKALI SANA NJE NA NDANI YA INCHI. SASA WENGINE WAKAANZA KUBISHA KWAMBA ZITTO NI MKALI KULIKO MASHAKA NA KUNDI LA MASHAKA NALO LIKAWA ALITAKA KUAMBIWA, BASI HAPO NDO NGUMI ZIKAANZA JAMAA WAWILI WAKAPIGANA KWELI KWELI, BILA SISI KUWEPO WANGUMIZANA. KWA HIYO MICHUZI KUANZNIA LEO TUNAOMBA USIWEKE MAKALA YA JOHN MASHAKA KWA MAANA JAMAA NI KONTREVESHO SANA KWENYE HII NCHI AKAE HUKO HUKO MAREKANI ASIRUDI HAPA NA VIZUNGU VINGI VYA KUOKOTA BWANA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2010

    % Naona mngeanza na MIJIFISADI PAPA! Sio kuonea hivi VIJIDAGAA tuu!

    % Mngesafishana woooote kwanza, mlioko kwenye system! I am talking to 'YOU'!

    % For those of you who 'CAN'T READ WITHOUT YOUR GLASSES', muisome hiyo, japo KIMYA KIMYA!

    % TIME IS ALL YOU HAVE!

    % MJIFUNZE KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI!

    % STAY TUNE FOR MORE!

    % WATAKAORUDI VIJIJINI MBONA WENGI MWAKA HUU!

    % %%% I AM KEEPING MY MOUTH SHUT BUT MY EYES WIDE OPEN!

    % IT IS TIME FOR ......!

    % IKIRUDI PANCHA HIYO!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2010

    Wabongo bwana ...wenye pesa wengi wao wanaiba...tofauti ni kwamba some are smarter than others

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2010

    mabilionea hawa mbona wamechoka?

    Mashaka

    ReplyDelete
  9. Jamani ii inji?! Kwani si waambiwe tu warudishe pesa halafu wataachiliwa? Au ni kwa kuwa wao ni wamatumbi?

    Kama memori yangu inanihudumia vyema, kuna kipindi wadosi waliachiwa/walisamehewa baada ya kurudisha paasenti flani ya zile pesa walizozichotaga kwa kuEPA?

    dayasipora daamu

    ReplyDelete
  10. Jamani ii inji?! Kwani si waambiwe tu warudishe pesa halafu wataachiliwa? Au ni kwa kuwa wao ni wamatumbi?

    Kama memori yangu inanihudumia vyema, kuna kipindi wadosi waliachiwa/walisamehewa baada ya kurudisha paasenti flani ya zile pesa walizozichotaga kwa kuEPA?

    dayasipora daamu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2010

    we acha za kuleta eti wanapigania atiko za mashaka?
    Yeye anatafuta umaarufu kwa kupitia mlango mbovu sana? mwambieni akajipime kwa Lakailo huko Rorya aone ndipo aache kujiita nabii au sijui rais wa wapi!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2010

    Mwizi anamkamata mwizi kazi ipo wafungwa msijali kwa kuwa wote tu wezi mtarudi tu nyumbani kama wale wengine ambao wapo majumbani mwao wameweka miguu juu. Sisi wakulima na walala hoi ndiyo hata maji ya kupikia watoto hatuna.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2010

    Mie sidhani kama wana kosa.. hawa wanaiga mabosi wao. kamateni mabosi kwanza ... mbona mnaogopa. Matajiri wooooooote nchi hii ni wezi. Hakuna mTZ hata mmoja mwenye mshahara wa kujenga majumba ya kifahari, na magari ya kifahari.... labda wafanya biashara tu, lakini nao vile vile hudhurumiana na kutumia ushirikina..Hawa waacheni tu kamata kwanza walioanza kutuhumiwa then hawa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2010

    uhhhh what is this? yani wanakaa kujishuhurisha na hawa vii billion 3 wakina richmond na mafisadi wengine wako wapi?mbona hatuoni wa epa hapa?.serikali yetu is so unfair.kama serikali is trying to win back our trust waache ku deal na hawa unknown ambao wameshawishika kuiba kutokana na mifano wanayoona kutoka kwa wakuu wetu...wale wote MAFISADI waliokuwa na majina makubwa they prove to be untouchable should be dealt with na hapo ndiyo wananchi tutaamini serikali tena other wise upuuzi mtupu

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2010

    naomba mnisaidie, hivi mhasibu anaweza 'kuprocess' kila kitu mpaka pesa ikatoka bila kumhusisha bosi wake. Nafikiri kuna haja ya ya kuwaunganisha mabosi. Please polisi fanyeni kazi yenu, acheni woga.


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 23, 2010

    Mm! Tangu mwaka 2008 ndo wanastuka leo,muda woote huo walikuwa wapi.Oky nlkuwa nmesahau kumbe uchaguzi iz around the corner! Ila thakx God hamna mchaga hata mmoja coz watu wangezusha ndo tabia yao!kalagabao
    Bro misupu usinibanie commet yangu!

    Genius wa kitaa

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 23, 2010

    Halafu bado mnasema waChagga wezi?

    Kila kabila lina wezi.

    Pia, hii mbona sasa kama mchezo wa kuigiza? Hizo bilioni 3 tu wataandamwa wee, halafu warushwe lupango. Lakini akina Chenge, Mramba, Yona na kadhalika wataambiwa warudishe tu taratibu

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 23, 2010

    Hawa sio vidagaa. Bilioni 3 ni nyingi sana.

    Watanzania wana Tamaa ya kuishi maisha ya juu huku hakuna means za ku support maisha ya juu.

    Magari Mazuri, Majumba mazuri. Ukiwatazama elimu hakuna !!

    Mawaziri wenyewe ukiwaangalia hawana elimu.

    Hii imekuwa ni nchi ya wasanii!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 23, 2010

    Duh me sishangai sana ndo mambo yenyewe hayo ya kila siku huko makwetu.kinachonisikitisha zaidi ni kuona mahakama na polisi wamesahaulika,majengo ni ya kutisikitisha,itakuwa vp hawa watu mishahara yao?kama imeshindikana kujenga huko,sheria haki haitakwenda na ndo maana tunasikia kila kukicha ngoma zinapepea na kusahaulika,watu wameshakula chao hapo.Jamani Tz tuamke.Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 23, 2010

    Mwenye miwani anaitwa Robert tulimaliza nae form 4 Azania mwaka 1998 ni kijana mtaratibu sana pole ndg yangu yataisha katika maisha misukosuko haikosekani

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 23, 2010

    BONGO SIRUDI HATA NIKISIKIA YESU KARUDI BONGO .HATARUDI YEYE MI NO .

    ReplyDelete
  22. "Money laundry"....kicheko kicheko kicheko...hivi vimombo...mie sisemi...

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 23, 2010

    Hapo sioni sura ya billioneaz
    Hawa ni kafara tu

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 23, 2010

    bongo kuna uonevu jamani!wapi big fish?wanaonewa watu ambao wametumiwa tu tena wengine bila kujua

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 31, 2010

    Hii yote sineme ya 2010, ama kweli uchaguzi unatia wazimu.......hebu serikali ikaangalie ni jinsi gani itasaidia amabao hawajawahi kuona umeme wa TANESCO maishani mwao badala ya kupoteza hela kufuatilialia kesi za kusimuliwa." hadithi hadithi... hapo mwaka 2008... eeeh...." achane hizo bwana tunaakili siku hizi. Alaaaah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...