Ndugu Michuzi;
Kwa heshima na unyenyekevu, ninapenda kuwatangazia watanzania na watu wote wanaoishi katika jiji hili la Dallas -Texas kwamba kutakuwa na SEMINA ya siku mbili ya neno la Mungu katika jiji letu la Dallas-Texas.

Semina hii itaendeshwa na watumishi wa Mungu PASTOR ABIUD & CATHERINE PAMOJA NA EV.LENATA KUTOKA TANZANIA. Watumishi wa Mungu Mr&Mrs Abiud wanaheshimika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na wito wao wa kumtumikia Mungu kwa upendo na unyenyekevu mkubwa.

Kwa sasa hawa watumishi wameweka maskani yao katika jiji la Kansas -Missour (USA).Ninaomba kwa kila mtu atakaesoma tangazo hili amkaribishe mwenzake.Pamoja na semina ya Mungu, watumishi hawa watapata nafasi ya kutoa ushauri kwa watu wanye matatizo binafsi na kuwaombea.Kama unahitaji ushauri wa ndoa,uchumba, mahusiano na mambo kama hayo usisite kutujulisha ili utengewe muda wa kukutana nao ana kwa ana..

Kumbuka tarehe ni 17-18/7/2010-Jumamosi na Jumapili ya wiki hii.
Mahali ni-Umoja Church,127217 Hillcrest Rd,Dallas Texas 75230
Muda ni:Saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku (11-2 usiku) 5pm 8Pm.
Maelezo zaidi;214 554 7381,682 552 6402,214 773 6697.

NB:Kutakuwa na chakula maalumu pamoja na vinywaji kila baada ya semina ili kufahamiana zaidi.

Karibuni wote

Uongozi wa kanisa la Umoja Dallas Texas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. TAFADHALI NAOMBA EMAIL ADDRESS YA MRS CATHERINE. NILIPOTEZANA NAYE SIKU NNYINGI. NAOMBA NISAIDIWE EMAIL ADDRESS YAKE ILI NIWEZE KUWASILIANA NAYE NA PIA KUPATA MSAADA ZAIDI WA NENO LA MUNGU. NAOMBA SANA. MDAU WA TZ.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2010

    Abihud tulisoma wote pale UDSM kumbe sasa mwenzetu ni Pastor! Mungu azidi kukubariki na akutie nguvu ktk kazi kubwa hii unaifanya ya kumtumikia ktk shamba lake. Ninaamini mbegu unazozipanda zitatoa mavuno. Naomba e mail yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...