Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ni mdhamini mkuu wa timu za Simba na Yanga zinazoshiriki ligi kuu ya soka ya Vodacom premier league leo imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu hizi mbili kwa ajili ya kuvitumia katika maandalizi ya ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara mzunguko wa kwanza.
Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Bw. George Kavishe alisema bia ya Kilimanjaro imekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu nchini.
Bw. Kavishe alisema vifaa vilivyokabidhiwa leo vina thamani ya shilingi milioni sitini na nne (64,000,000/=) na vitatumiwa na timu hizo kwenye mazoezi na michezo ya ligi ya Vodacom .
Aidha alisema udhamini wa bia ya Kilimanjaro kwa timu za Simba na Yanga unahusisha kupatiwa vifaa vya michezo kwa awamu mbili za ligi, awamu ya kwanza ikiwa ni kipindi cha mzunguko wa kwanza na awamu ya pili ikiwa ni Mzunguko wa pili,udhamini huu unahusisha pia kulipa mishahara kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi ya timu hizo, ikumbukwe pia kwamba Kilimanjaro Premium Lager tayari ilishazipatia magari mawili kwa kila timu kwa ajili ya safari za timu na viongozi.
Alisema udhamini wa Bia ya Kilimanjaro kwa timu za Simba na Yanga ni sehemu ya mkakati mkubwa wa Bia hiyo wa kuhakikisha inafanikisha Soka la Tanzania kufikia kilele cha mafanikio.
“Kampuni ya Bia Nchini TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, inafofuraha kubwa kutoa vifaa vya maandalizi kwa timu za Simba na Yanga ambazo tumekuwa tukizidhamini kwa muda sasa na hakika zimekuwa na maendeleo na mafanikio makubwa kwenye ligi kuu ya mpira wa miguu hapa nchini na hii inatupa matumaini makubwa na leo tunakabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni sitini na nne kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu hapa nchini Tanzania na hii ni sehemu ya mkakati wa bia ya Kilimanjaro kuhakikisha soka la Tanzania lina kuwa na kufika kwenye kilele cha mafanikio .”Alisema bwana Kavishe.
Kwa upande wao wawakilishi wa timu hizo waliishukuru bia ya Kilimanjaro kwa kuendelea kuvidhamini vilabu hinyo na kuahidi kuendeleza makali yao pindi mzunguko wa kwanza wa ligi kuu utakapoanza Aug 21,2010.
Timu za Simba na Yanga zimekuwa zikishiriki ligi kuu ya Tanzania Bara kwa muda mrefu ambapo kwa msimu uliopita timu ya Simba iliibuka kidedea huku timu ya Yanga ikishika nafasi ya pili ambapo Simba italiwakilisha Taifa katika mashindano ya club Bingwa barani Africa huku Yanga nao wakishiriki kwenye mashindano ya shirikisho barani Africa.
Ankal massad kwenye tuta !
ReplyDeleteNATAFUTA KIJANA WA KUUZA DUKA.
SIFA:
-Awe tayari kufanya kazi mpaka saa 3 usiku
-Awe na idear ya computer
-Awe mkazi wa Dar
Tuwasiliane kwa email address: infotechnician2004@yahoo.com
Thanks,
Mdau
Kama kawa TBL wanapata coverage kubwa sawa na wanzao vodacom, mwamvita, ridhiwani, january ect etc but anyways they've got money so what do ya expect
ReplyDeleteSasa ujinga gani huo jamani?baadala ya kuzisaidia timu nyonge za mikoani ili waweze kukuza vipaji vya vijana chipukizi,... ati tunazisaidai timu mbili kubwa ambazo zina wafadhili magabacholi wa kihindi!!!ahh bwana mbongo ujinga mpaka kiama!
ReplyDeleteEdithaaaaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeleteNdio maana gani kusaidia Simba na Yanga pekee? Kwani ndio timu pekee kwenye ligi kuu? Wao kama wafadhili wa ligi basi kwanini wasisaidie na time nyingine especially za mikoani? Lalafu tunashanga timu ya taifa hifanyi vizuri!!! Bongo tambarare kwelkwel!! - Mdau, Geneva.
ReplyDeleteMalalamiko malalamiko wabongo bwana. TBL anatangaza biashara ndio maana ya udhamini na wanafanya kitu ambacho kwa mfanyabiashara yoyote mwenye akili ni sahihi. Ndio maana mabango ya biashara yanawekwa pembeni ya barabara na si chini ya madaraja kwa nini ukafadhili timu amabayo haijazi uwanja kama haichezi na simba au yanga wakati ukifadhili simba na yanga unauhakika wanajaza uwanja kila siku? fikiria kabla ya kunena hii ni biashara na si msaada kwa wanyonge.
ReplyDeletekaseja mbona mavazi yanapingana na hali ya hewa au unaishi iringa?
ReplyDeletenimalizie pia edithaaaaa khaaaa
ReplyDeleteniulize pia maana si ujinga ati,,ivi kampuni za bia mbona ni wachaga mwanzo-mwisho???????????
no wonder wazanzibar hatutaki huu ufadhili najisi!hivi kwanini tunaongoza kwa mipombe ivi?
ReplyDeleteHIVI HICHI KIWANDA CHA BIA SIKU HIZI KIMENUNULIWA NA WACHAGA NINI? MAANA NAONA MAJINA YA VIONGOZI WOTE NI WALE WALE WA KUTOKA CHINI YA MLIMA KILIMANJARO KINA MINJA,KAVISHE,MUSHI NI NINI KINAENDELEA HAPO?
ReplyDeleteYakheee Kaseja, kunani, mbona 'umeficha uso'!!
ReplyDeleteNkyabo - Bongo
Kwa hiyo timu ni simba na Yanga tuu??au inakuwaje hapo sasa!!Labda sielewi vizuri!je na timu nyingine za ligi wanapewa seti za vifaa vya michezo??!!sijakaa sawa kabisa hapo!!!hoooi bin taaban!!
ReplyDeleteMwisho wa reli hapa!!
Mushi Mungi Masawe wa Thu Jul 22, 05:04:00 PM, inaonekana una matatizo, jina la kilaji ni'Kilimanjaro', sasa unataka wakulya ndo waajiriwe huko.
ReplyDeleteNkyabo _ Bongo