Meneja wa Bia ya Kilimanja,George Kavishe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliofika leo katika ukumbi wa mikutano TFF kwenye makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa timu za Simba na Yanga.kushoto ni Meneja Uhusiano wa TBL,Editha Mushi
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akikabidhi jezi kwa mwenyekiti wa Yanga,Lloyd Nchunga kwa ajili ya timu ya Yanga.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akikabidhi jezi kwa makamu mwenyekiti wa Simba,Geofrey Nyange Kaburu kwa ajili ya timu ya Simba.kulia ni Meneja Uhusiano wa TBL,Editha Mushi na kushoto ni Mjumbe wa Simba.
Wachesaji wa timu ya Yanga,Athuman Iddy na Abdi Kassim wakiwa wametinga nyuzi mpya zilizotolewa leo na kampuni ya bia TBL kupitika kilaji chake cha Kilimanjaro.
Nyanda wa timu ya Simba,Juma Kaseja akiwa ametinga nyuzi mpya zilizotolewa leo na kampuni ya Bia TBL kupitika kilaji chake cha Kilimanjaro.


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ni mdhamini mkuu wa timu za Simba na Yanga zinazoshiriki ligi kuu ya soka ya Vodacom premier league leo imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu hizi mbili kwa ajili ya kuvitumia katika maandalizi ya ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara mzunguko wa kwanza.

Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Bw. George Kavishe alisema bia ya Kilimanjaro imekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu nchini.

Bw. Kavishe alisema vifaa vilivyokabidhiwa leo vina thamani ya shilingi milioni sitini na nne (64,000,000/=) na vitatumiwa na timu hizo kwenye mazoezi na michezo ya ligi ya Vodacom .

Aidha alisema udhamini wa bia ya Kilimanjaro kwa timu za Simba na Yanga unahusisha kupatiwa vifaa vya michezo kwa awamu mbili za ligi, awamu ya kwanza ikiwa ni kipindi cha mzunguko wa kwanza na awamu ya pili ikiwa ni Mzunguko wa pili,udhamini huu unahusisha pia kulipa mishahara kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi ya timu hizo, ikumbukwe pia kwamba Kilimanjaro Premium Lager tayari ilishazipatia magari mawili kwa kila timu kwa ajili ya safari za timu na viongozi.

Alisema udhamini wa Bia ya Kilimanjaro kwa timu za Simba na Yanga ni sehemu ya mkakati mkubwa wa Bia hiyo wa kuhakikisha inafanikisha Soka la Tanzania kufikia kilele cha mafanikio.

“Kampuni ya Bia Nchini TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, inafofuraha kubwa kutoa vifaa vya maandalizi kwa timu za Simba na Yanga ambazo tumekuwa tukizidhamini kwa muda sasa na hakika zimekuwa na maendeleo na mafanikio makubwa kwenye ligi kuu ya mpira wa miguu hapa nchini na hii inatupa matumaini makubwa na leo tunakabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni sitini na nne kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu hapa nchini Tanzania na hii ni sehemu ya mkakati wa bia ya Kilimanjaro kuhakikisha soka la Tanzania lina kuwa na kufika kwenye kilele cha mafanikio .”Alisema bwana Kavishe.

Kwa upande wao wawakilishi wa timu hizo waliishukuru bia ya Kilimanjaro kwa kuendelea kuvidhamini vilabu hinyo na kuahidi kuendeleza makali yao pindi mzunguko wa kwanza wa ligi kuu utakapoanza Aug 21,2010.

Timu za Simba na Yanga zimekuwa zikishiriki ligi kuu ya Tanzania Bara kwa muda mrefu ambapo kwa msimu uliopita timu ya Simba iliibuka kidedea huku timu ya Yanga ikishika nafasi ya pili ambapo Simba italiwakilisha Taifa katika mashindano ya club Bingwa barani Africa huku Yanga nao wakishiriki kwenye mashindano ya shirikisho barani Africa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2010

    Ankal massad kwenye tuta !

    NATAFUTA KIJANA WA KUUZA DUKA.

    SIFA:

    -Awe tayari kufanya kazi mpaka saa 3 usiku
    -Awe na idear ya computer
    -Awe mkazi wa Dar

    Tuwasiliane kwa email address: infotechnician2004@yahoo.com

    Thanks,
    Mdau

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2010

    Kama kawa TBL wanapata coverage kubwa sawa na wanzao vodacom, mwamvita, ridhiwani, january ect etc but anyways they've got money so what do ya expect

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2010

    Sasa ujinga gani huo jamani?baadala ya kuzisaidia timu nyonge za mikoani ili waweze kukuza vipaji vya vijana chipukizi,... ati tunazisaidai timu mbili kubwa ambazo zina wafadhili magabacholi wa kihindi!!!ahh bwana mbongo ujinga mpaka kiama!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2010

    Edithaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  5. Mdauz, GenevaJuly 21, 2010

    Ndio maana gani kusaidia Simba na Yanga pekee? Kwani ndio timu pekee kwenye ligi kuu? Wao kama wafadhili wa ligi basi kwanini wasisaidie na time nyingine especially za mikoani? Lalafu tunashanga timu ya taifa hifanyi vizuri!!! Bongo tambarare kwelkwel!! - Mdau, Geneva.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2010

    Malalamiko malalamiko wabongo bwana. TBL anatangaza biashara ndio maana ya udhamini na wanafanya kitu ambacho kwa mfanyabiashara yoyote mwenye akili ni sahihi. Ndio maana mabango ya biashara yanawekwa pembeni ya barabara na si chini ya madaraja kwa nini ukafadhili timu amabayo haijazi uwanja kama haichezi na simba au yanga wakati ukifadhili simba na yanga unauhakika wanajaza uwanja kila siku? fikiria kabla ya kunena hii ni biashara na si msaada kwa wanyonge.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2010

    kaseja mbona mavazi yanapingana na hali ya hewa au unaishi iringa?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2010

    nimalizie pia edithaaaaa khaaaa

    niulize pia maana si ujinga ati,,ivi kampuni za bia mbona ni wachaga mwanzo-mwisho???????????

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2010

    no wonder wazanzibar hatutaki huu ufadhili najisi!hivi kwanini tunaongoza kwa mipombe ivi?

    ReplyDelete
  10. MUNGI MUSHI MASAWEJuly 22, 2010

    HIVI HICHI KIWANDA CHA BIA SIKU HIZI KIMENUNULIWA NA WACHAGA NINI? MAANA NAONA MAJINA YA VIONGOZI WOTE NI WALE WALE WA KUTOKA CHINI YA MLIMA KILIMANJARO KINA MINJA,KAVISHE,MUSHI NI NINI KINAENDELEA HAPO?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2010

    Yakheee Kaseja, kunani, mbona 'umeficha uso'!!


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  12. Kwa hiyo timu ni simba na Yanga tuu??au inakuwaje hapo sasa!!Labda sielewi vizuri!je na timu nyingine za ligi wanapewa seti za vifaa vya michezo??!!sijakaa sawa kabisa hapo!!!hoooi bin taaban!!
    Mwisho wa reli hapa!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2010

    Mushi Mungi Masawe wa Thu Jul 22, 05:04:00 PM, inaonekana una matatizo, jina la kilaji ni'Kilimanjaro', sasa unataka wakulya ndo waajiriwe huko.

    Nkyabo _ Bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...