MKURUGENZI MKUU wa Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC), Bw. Tido Mhando
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC), Tido Mhando amewataka Watanzania kuwa na mwamko wa kutumia mfumo mpya wa kisasa kurushia matangazo ya televisheni kwa kutumia vinga’muzi ujulikano kwa jina la ‘digitali’ ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi huyo mara baada ya waandishi wa habari kumaliza ziara fupi ya kutembelea Kampuni ya Star Times iliyopo Mikocheni katika ofisi za TBC, Kariakoo na kutembelea mnara wenye urefu wa mita 136 ambao ni mrefu kwa Afrika Mashariki wa kurushia matangazo hayo uliopo eneo la Kisarawe, mkoa Pwani.

“Wananchi wanatakiwa kujua umuhimu wa kutumia ving’amuzi (digital) ili kuendana na mabadiliko ya dunia,” alisema Mhando.

Mhando alisema TBC ilipewa kazi na Serikali ya kusambaza mfumo huo nchi nzima ifikapo mwaka 2012, ambapo ilitafuta mwekezaji kwa ajili ya kazi hiyo.

Aliongeza kuwa mwekezaji huyo, Star Times ambaye ameingia ubia na TBC anajulikana kwa jina la Star Media Tanzania.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Star Media Tanzania, Charles Liu, alisema kampuni hiyo imewaajiari Watanzania 185 kwa ajili ya kazi hiyo na wategemea kuajiri Watanzania 2000 mitatu. Aliitaja mikoa ikayofuatia kutekelezwa suala hilo katika awamu ya pili ni, Mbeya, Moshi, Tanga na Shinyanga.

Mkurugenzi Msaidizi wa Star Media Tanzania, Lilian Masanche, alisema watahakikisha kila familia katika mikoa yote nchini wanafurahia matangazo hayo kwa kutumia huduma hiyo ya kisasa.

Kampuni hiyo inafanya kazi hiyo hivi sasa katika mikoa ya Dares Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma. Jumla ya dola za Marekani zaidi ya milioni 200 zitawekezwa katika suala hilo na tayari wameshawekeza dola za Marekani milioni 30.ends

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2010

    Mwanzo na mwelekeo mzuri lakini hamna matayarisho kuendana na teknolojia. King'amuzi cha Star Times sio automatic. Ukilipia, inawachukua muda zaidi ya wiki mbili kurudisha huduma. Kweli maendeleo tunayataka lakini tuwe serious, ndio maana DSTV wanapiga bao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2010

    Kwa king'amuzi hicho cha Star Times kama mambo yake yataendelea kama yalivyo bila uboreshaji wowote kwa kweli mtachemsha tena mapema sana. Pengine kifo cha Star Media kitakuwa cha mapema zaidi hata ya chama cha CCJ!
    Kwanza habari iliyopo ni kwamba baada tu ya kwisha kwa kombe la dunia wateja wapya wa Star Times wamepungua sana.Sasa na ukiongeza na huduma zisizoridhisha hadi hivi leo ndiyo wanajimaliza kabisa. TBC na mbia wenu shughulikieni malalamiko haya na kuboresha huduma zenu. Vinginevyo..... haya, yetu macho!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2010

    Cha kwangu nilisha kitupa potelea mbali 79,000 ilikwenda lakini nilifanya hivyo kutokana na upumbavu wao siku ya fainali. Maana ilinilazimu kwenda baa kuepuka kero niliyokua naiona kwenye TV. Kingine ni udanganyifu waliowafanyia watanzania ili kuviuza vidude vyao. Kibaya zaidi hizi namba za simu 0767 000 705/6/7 unaweza kupiga nusu siku zimefungwa zoote ati huduma kwa wateja. Kwa sasa Tido na hao patners wako itabidi mtumie gharama kubwa sana kurudisha mteja aina ya mimi kwenye soko lenu, kwani kwa mimi bidhaa yenu ipo kwenye decline stage!Nadhani kwa sasa mnasubiri kutokea kwenye ligi za Ulaya, try this.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...