kweupee pee...
jamaa wakivuta pumzi baada ya kazi ngumu ya kutembeza nyundozz katika eneo iliyokuwepo pub ya Mamaz.
hapa ndipo ilipokuwepo mafia fish bar ambapo sasa ni kweupe kabisa baada ya nyundozz kutembezwa siku za hivi karibuni.
hapa ndipo ilipokuwepo ile babaz pub.
mpaka sasa haijajulikana ni sababu gani zilizopelekea eneo hili kutembezewa nyundo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Aaah kijiwe chetu wenyewe cha CHIPS mzigo,shikaki kuuuubwa la alfu,au unakula nyama FOIL kwa buku 3 tu,nyama safi na laini,Wazee wa JIJI kwani imekuaje tena kaa????

    ReplyDelete
  2. Habari nyepesi mtaani zinasema wakazi/wanajeshi wanaoshi kwenye nyumba za eneo lile hasa ambao waliokuwa na viwanja vyao vikitumiwa na baa/biashara hizo zilizovunjwa, walikuwa na mgogoro wa ki-maslahi. Wakazi wengine nao wivu juu, kikaitwa kikao cha wajeda waishio kwenye kota hizo na wakaamua wavunje baa hizo kwani ni eneo la nyumba za jeshi na biashara hizo zilikuwa eneo lisilo rasmi. Wenye habari za uhakika zaidi wazimwage hapa, mi nimezipata kwa majirani wa hapo.

    ReplyDelete
  3. Usibanie Komenti Michuzi, Dah washatuharibia Ratiba za kudanganya Wife Kutizama Mipira au na mkutano na mtu flani hizi sehemu.

    ReplyDelete
  4. watu kwa kupenda mambo holela holela.....hapo mahali na hiyo biashara havifananii kabisa!....basi tu uswahili.

    ReplyDelete
  5. Ulikuwa ni uchafu tu. haiwezekani kila kona na eneo kuna baa/kijiwe. Ni usumbufu. makazi ni makazi, maeneo ya biashara ni maeneo ya biashara. siyo kila kitu holela. Ziko wapi club areas. zirudishwe mahala ambapo, mtakutana, mtafanya mazoezi, mtashauriana nk. siyo vijiwe vya pombe tu. Ni uchafu na ubabaishaji mtupu. Ningesema uswahili mtupu lakini nadhani siyo neno sahihi. Hongera City council,

    ReplyDelete
  6. Poa tu wazee huo ulikua uchafu hata kama kuna kisingizio kingine.

    Kama wakiweza kuanzisha biashara ndani ya nyumba zao poa

    ReplyDelete
  7. Bongo watu wanapenda sana kulala lala. Sijaona nchi yoyote watu wanapenda starehe wakati wa kazi kama Bongo, ndio maan umasikini hautaisha.

    ReplyDelete
  8. kwakweli nimefurahishwa sana na hli jambo maana ulikua ni uchafu tu ni mambo ya aibu atii hlo sio eneo la biashara ni makazi ya watu tunajenga kizazi gani?? City kazi nzuri mmelianzisha uko juu naomba mshukuke mitaa ya jackies,didz na hyo nyingine pembeni ya didz hyo ni OBay na wala si sinza.

    ReplyDelete
  9. dah masakiiiiiiiiiiiiiiiiiii kama sinza vile nyumba bar nyumba bar!!!Lkn masaki imeharibiwa na wanajeshi ukiangalia nyumba zote walizokaa wanajeshi either kuna biashara ya bar duka ama zimejengwa apartments hii yote hawa watu walizoea vya bure sasa mtu akishastaafu tu hajui aanzie wapi bili ya umeme, maji n nk hajui sababu alikua analipiwa wakitoka kwenye system sasa ndio wanahaha kama kuku. Serikali lijaribu kuliangalia hlo. Ankali jaribu kufanya na wewe research then utaniambia mm

    ReplyDelete
  10. KAKA MICHUZI,AU MTU YOYOTE YULE ANAYETAKA KUJUA TAARIFA ZAIDI JUU YA HILO TUKIO, NENDA PALE KWENYE NYUMBA ZA JESHI UKAMUONE MKUU MUWAKILISHI WA HICHO KIJIJI ANAYEITWA COLONEL MANGWAMBA.. YEYE ATAKUPA TAARIFA ZA UHAKIKA ZAIDI.. OTHERWISE HEAR SAY ZITAKUA BWENA MWANANGU.. GENERAL ALIYEAMURU KULE JESHINI MASAKI MWISHO KUVUNJWE NDiO HUYO HUYO KATOA ORDER KUWA NA PALE PIA PAPIGWE NYUNDO.. WHY? HAKUNA AJUAYE.. AMRI IKITOKA KWA MKUU NI LAZMA IFUATWE..!! hahahaha

    ReplyDelete
  11. Nawapa pongezi City Council kwa kazi nzuri sana waliofanya, maana vijana wamjini wamezidi kukaa vijiweni badala ya kuwahi majumbani mwao kucheza na watoto wao, nadhani hapo ni mwanzo tu kuvunjwa hizo bar. safi sana waliovunja pongezi kwao, kina baba watawahi hm sasa, dstv zipo home but wanapenda tu kwenda bar.

    ReplyDelete
  12. .....jamani mie nauliza tu wakubwa, hivi huu utaratibu wa kugeuza maeneo executive ya makazi kama kona ya st. peter, obay, chole, masaki ni sawa kufungua maduka, migahawa, apartment , hotels , night club na kadhalika*2? maana mpaka madada poa siku hizi wanasimama OBAY !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...