Meneja masoko wa kampuni ya Zanzibar Media Corporation ND Said Khamis akimkabidhi Balozi wa Marekani nchini zawadi ya Mlango wa Asili wa Zanzibar (ZANZIBAR DOOR)Serikali ya Marekani imesema wananchi wa Zanzibar wanapaswa kushikamana katika kuijenga upya nchi yao baada ya kukubali kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kupitia kura ya maoni.
Akizungumza na Zenji fm Radio balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhert’s amesema hatua hiyo iliyochukuliwa na wananchi wa Zanzibar itasaidia sana kudumisha uhusiano wa nchi mbili hizo.
Amesema azma ya Marekani ni kuendelea kuisaidia Zanziar katika miradi ya maendeleo ambayo nchi hiyo imekuwa ikitoa misaada yake kama vile mradi wa umeme unaofadhiliwa na shirika la Millenium Challenge.
Aidha balozi Alfonso amesema Marekani inatarajiwa kuisaidia Zanzibar kutekeleza mradi mpya wa karne ya 21 wa elimu ya msingi na mafunzo ya amali utakaozinduliwa hivi karibuni.
Amesema mradi huo utawasaidia wanafunzi kujua na kutumia kompyuta wakiwa katika skuli za msingi, kunyanyua somo la hesabati pamoja na utowaji wa mafunzo kwa walimu wa skuli za msingi.
Marekani pia imetoa misaada kwa Zanzibar katika sekta ya afya ukiwemo mradi wa kukataa malaria, kukabiliana na tatizo la ukimwi na kifua kikuu, utowaji wa vitabu vya sayansi kwa skuli za sekondari na maeneo mengine ya kiuchumi na kijamiiKufuatia kura ya maoni iliyopigwa na wanachi wa Zanzibar iliykubali kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa zaidi ya asilimia 60 nchi nyingi za wahisani na mashirika ya kimataifa yameipongeza Zanzibar kwa hatua yake hiyo.


Huo ni mlango asili wa kiarabu, Zanzibar ilikuwa na milango yake kabla mwarabu hajaja, na hiyo ndio milango ya asili ya Zanzibar.
ReplyDeleteMh!! bila shaka kuna jambo huuu ugeni si bule tuu!! either anataka kuchukua plot kama walivyofanya kigambon! au kapeleka net zenye dawa ya kuu mmbu miaka 5 wa kuacha sumu kwa mwanadamu anayetumia imiadhili maisha yake yote!! au kapeleka propaganda za zungumza na umpendae kwa msaad wa wamerekani , wakat marekan ndoa zinaongoza kwa kuvunjika, kuuana na kusalitiana..ndo anataka kuyaleta Zenji haya!!!!! ?? Hatudnyangikiiii!!
ReplyDeleteMashallah msk Zenj fm iko juuu
ReplyDeleteBLOG SASA INAISHA UMAARUFU WAKE KWA KUEGEMEA CCM... JAPOKUWA MIE SIFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE, KUTOKUPATA PICHA YA UPANDE WA PILI WA CCM INANIKERRRRA!!
ReplyDelete