ufunguzi wa mradi wa maji Kemgesi
Mitungi ya kuifadhia Maji Majumbani ikiwa imezunguka na wakazi wa kijiji hicho
Wakina mama wakipata huduma ya maji wa ukaribu kabisa.
Tank la kuhifadhia Maji shuleni

Mpendwa michuzi

Naomba kuwakilisha ujumbe huu Mzuri na wa kuigwa kwa kazi nzuri zinazofanywa na NGO ya CARE International katika vijiji vya wilaya ya Serengeti Kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.Shirika hili limekuwa likifanya kazi zake hasa kwa upande wa Mazingira (Elimu ya maji na Mazingira (Sanitation)Pamoja na Hygiene(Elimu Siha).Hivyo nikiwa kama mdau na mwenyeji wa Serengeti kwa yeyote anaeifahamu vizuri kama jamii ya wafugaji anaelewa nazungumzia nini kwani hali ya usafi wa mazingira bado ni mbaya sana.

Shirika hili limejitahidi kujenga Vyoo na matank yakuvunia maji katika shule za msingi,kuvijengea vyanzo vya maji na kuweka vituo vya kuchotea maji ili kuwapunguzia majukumu mama na dada zetu.Pia wamejitahid kujenga vyoo vya mfano vya mabampa (saniplat) kwa kutumia vifaa rahisi na vinavyopatikana kwenye mazingira husika hii ni kutokana mazingira halisi karibu nusu ya familia hutumia vichaka kujisaidia na kusababisha vinyesi kutapakaa ovyo.

Ombi ningependa na mashirika mengine wajitolee ili watu wa Serengeti tuweze kubadilika

Naomba kuwakilisha

Wako Mpenda Maendeleo

Chacha Wambura

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...