(shati jeupe) akiwa na viongozi wa CCM mkoa wa Mwanza
Mwenyekiti wa Kampeni wa CCM Mh. Adbdulrahman Kinana ameeleza masikitiko yake dhidi ya CHADEMA kwa kuvunja maadili waliyosaini kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu, ambapo Bw. Mabere Marando ambaye ni Mwanasheria Kaongelea mambo ya EPA yaliyo mahakamani kinyume na Ethics za Taaluma
Amesdema katika taarifa ya habari ya TBC 1 kwamba CCM haiwezi kuongelea mambo yaliyo Mahakamani na kusisitiza ni vyema kutumia lugha isiyo ya matusi ili hata baada ya uchaguzi viongozi waendelee kuongea pamoja badala ya kukwepana.
Mwenyekiti wa Kampeni wa CCM Mh. Adbdulrahman Kinana ameeleza masikitiko yake dhidi ya CHADEMA kwa kuvunja maadili waliyosaini kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu, ambapo Bw. Mabere Marando ambaye ni Mwanasheria Kaongelea mambo ya EPA yaliyo mahakamani kinyume na Ethics za Taaluma
Amesdema katika taarifa ya habari ya TBC 1 kwamba CCM haiwezi kuongelea mambo yaliyo Mahakamani na kusisitiza ni vyema kutumia lugha isiyo ya matusi ili hata baada ya uchaguzi viongozi waendelee kuongea pamoja badala ya kukwepana.
Jamani, jamani CCM hata kama ndiyo chama tawala basi msiambiwe ukweli???
ReplyDeleteInajulikana kabisa EPA ilikuwa mpango wa makusudi.
TBC siwashangai kukata matangazo kwani nyie ni Radio ya Chama na wala siyo ya serikali.
Najua kuna ulipaji fadhila ndani yake....
People Power, sema Marando hata kama hawataki kusikia ukweli.
Hata kama itachukua miaka, lakini iko siku wadanganyika hawa wataupata ukweli wa ufisadi wa CCM.
Hakuna matusi yoyote ambayo CHADEMA wameongea, walichoongea ni ukweli mtupu kuhusu EPA ambao CCM hawataki wananchi waujue.
ReplyDeleteUSINIBANIE HII UNCLE,CCM WAACHE KULALALAMIKA, MBONA WAO WANAIMBA MPAKA NYIMBO ZA KEBEHI? WALIZOEA KUONA WAGOMBEA DHAIFU SASA WANAIPATA.
ReplyDeletechadema hawajui siasa,wanapandikiza siasa za chuki sana,usituharibie nchi yetu,hebu angalieni cuf,wamekuwa wapinzani muda mrefu lakini wanafanya siasa za kistaarabu sana.chadema tarime kipindi kile walikuwa wanaimba kama kenya na slaa na zito wanashangilia.juzi wametaka kumpiga muandishi wa tbc,hiki chama kiko kama cha wavuta bangi,ndo maana wameweza kumpitisha mr 2 kugombea uunge mbeya,wakati ananyimbo mpya ya anti virus imejaa matusi na maneno ya ajabu,hivi mnafundisha nini kwa kizazi kijacho,shukuruni sana JK ni mstaarab,ingekuwa enzi za mkapa na uhakika hiki chama kingefungiwa.hata gazeti lao la tanzania daima kila siku watu wanalalamika kwa kuingiziwa mambo,mgaya wamemchafua vibaya.shame on you chadema.tanzania ni wapenda amani,tunataka siasa za kumwaga sera,sio matusi jukwaani.
ReplyDeleteWapinzani wasiongee mambo yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi yetu kama EPA,RICHMOND,MEREMETA na TICS.
ReplyDeleteTunataka waongee vitu vya kawaida kama "mke wa rais wetu anaitwa SALMA; mtoto wake anaitwa Ridhwani,rafiki yake anaitwa LOWASSA na rais wetu anavaa miwani".
Hayo mengine msiyaongee;kwanza ni ya jeshi.
KWA KWELI INGAWA MIE SI MSHABIKI WA CHAMA CHOCHOTE CHA SERIKALI,
ReplyDeleteNIKWELI SIJAPENDEZEWA NA KAULI ZA CHAMA CHA CHADEMA,ILE SI KAMPENI BALI NI LUGHA CHAFU ZIMEWATAWALA WAMEPIGWA CCM HIO SIO VIZURI KABISA,YANI MI NIGEKUWA MWANACHAMA WA CHADEMA NINGESHAJITOA
SIWEZI KUENDELEA KUSIKILIZA LUGHA CHAFU NAMNA ILE.
la sikuelewa kama mambo ya EPA ni matusi
ReplyDeleteMichuzi ni mtu usiyefaa kabisa inapofikia mahali tunaita 'bias' Maana CCM walipozindua kampeni ulimwaga picha kede kede. Leo Chadema wamezindua unaweka katangazo kama kitu cha mtaani. Mtu mzima aibu tupu. CCM hata kule Ngara ulitoa picha zao. Tanzania hatutafika mbali tukiwa na mabloga kama nyinyi. Najua huta-publish malalamiko yangu lakini ujumbe umeupata.
ReplyDeleteUkweli Siku Zote Unauma..
ReplyDeletesio kweli kwamba kitu kikiwa mahakamani hakitakiwi kiongelewe hapo kinana utakuwa na wewe unakosea kisichotakiwa ni kukijaji kitu kilichopo mahakamani,
ReplyDeletemabele marando taaluma yake ni mwanasheri sidhani kama atajuwa amekulupuka kwa kuongelea hilo pia hata mimi sioni ni kitugani kilicho wafanya msikitike kwa kuongelewa kwa EPA kwani kuna siri tena juu ya hilo?
CCM imeshikwa pabaya.
ReplyDeleteHakuna kufurukuta.
Wanasema imekula kwao.
Kwaherini CCM.
Maskini KINANA huyoooooooo kaishiwa hoja.
ReplyDeleteCCM IMEFULIA
Hivi Kikwete alipozungumza kule Karagwe kuhusu jinsi serikali yake inavyoshughulikia rushwa na kujitapa kuwa wako viongozi wenzake wako mahakamani na akauliza "walijipeleka wenyewe?" alikuwa anazungumzia mambo yaliyo Kanisani?
ReplyDeleteAhh CCM, kwani huo si ukweli. Mi nafikiri kampeni ni comparison, na kama CCM wana kesi za ufisadi sioni kwani zisiwe kigezo kikubwa kwa wapiga kura...
ReplyDeleteCCM oyeee !!ndio chama pekee chenye mwelekeo kwa wa-Tanzania..wengine kama hao chadema njaa tupuuu
ReplyDeleteCCM hakuna haja ya kujibu shutuma za Vyama vya siasa, Endeleeni kunadi sela zenu
ReplyDeleteMdau MZALENDO kwikwikwikwi SHIKAMOO NIMECHEKA MPAKA NIMETAKA KULIA:::HASWAAAAAAAAAAAAAAAAAA na umesahau lingine kwao chalinze, anapenda kula nini ila sijui tukigusia pia mianguko itakuwa vibaya mdau MZALENDO au hahahahahahahaha yani umenichekesha mnoooooooooo
ReplyDeleteNi juavyo mimi matusi ni kutaja viungo vya mwili ambavyo ni private, lakini kusema fulani,na fulani walihusika na wizi wa EPA hakuna tusi, labda Kinana ana kamusi yake mpya. Kimahaka ile inaitwa tuhuma, tangu lini tuhuma ya ubadhirifu ikawa TUSI?. Marando ni wakili wa utetezi wa baadhi ya washitakiwa Kesi ya EPA, ni wazi aliwahoji wahusika ili waseme ukweli aweze kuwatetea, hivyo basi uwezekano wa alichosema pale jukwaani kuwa kweli hilo sitoshangaa. Kinana pia mbona naye alipataga skendo ya biashara chafu za makampuni ya meli na leo hii yupo CCM kwa cheo kile alichonacho, Michuzi we ni mwandishi wa siku nyingi hili si geni kwako, je likitajwa hapa nalo ni TUSI? Lowassa alijiudhuru uwaziri mkuu, watu wakisema kwamba alijiudhuru je ni TUSI?
ReplyDeleteMwanakijiji una hit the freakin nail on the head!!!
ReplyDelete(US Blogger)
CCM..... ELEZENI MAMBO YA EPA NA MENGINEO, MBONA SANA MNAJING'TA? SEMENI WAKATI NDIO HUO.....
ReplyDeleteCCM ZIIIIIIII CCM ZIIIIIII CCM ZIIIIIIII
ReplyDeleteCCM CHINI CCM CHINI CHINI ZAIDI
HEKO BLOG KWA KUCHAKACHUA MAONI.
ReplyDeleteWaambieni watu wenu wamtumie Michuzi picha za vyama vyenu ataweka. Yuko kazini kwenye mambo ya serikali hivyo hawezi kuwa na picha za kila kampeni na kila chama.
ReplyDeleteMibichwa yenu ielewe na sio kuandika tu ovyo
Ankal nimeamini wewe ni Kada wa CCM,
ReplyDeleteLakini panapo ukweli lazima usemwe. Marando hana haja ya kuficha ukweli wenyewe. EPA inajulikana wazi ilikuwa ufisadi wa Wakubwa kuelekea uchaguzi wa 2005, upende usipende.
Na TBC twaelewa wote mlengo wake uko chama gani, na Wakubwa lazima kulipana fadhila.
People Power....
Slaa, Marando semeni hata kama itawachukua miaka kuwaelimisha wadanganyika, naamini minyororo hiyo iko siku itakatika.
Ankal ukibana na hii tena shauri yako
Msemakweli
Mijitu mizima hovyooooo, kama mlizoea kukiuka maadili mbelke ya watoto mnategemea mtaendelea kupewa shikamoo, badilisheni nyendo zenu mtaheshimiwa, wanablog wengine hovyooooo kabisa, sasa amani itavunjikaje ina bidi tukupeni maana halisi ya amani kwani najua hamjui kwa sababu amani hujawahi kuipata na hujui utamu wake
ReplyDeleteHii comment imehaririwa maana ya mwanzo Michuzi umeibania, naendelea..
ReplyDeleteNi juavyo mimi matusi ni kutaja viungo vya mwili ambavyo ni private au kuhusisha akili na weledi wa mtu, lakini kusema fulani,na fulani walihusika na wizi wa EPA sidhani kama kuna tusi, labda CCM wana kamusi yao mpya. Kimahakama ile inaitwa tuhuma, tangu lini tuhuma ya ubadhirifu ikawa TUSI?. Marando ni wakili wa utetezi wa baadhi ya washitakiwa Kesi ya EPA, ni wazi aliwahoji wahusika ili waseme ukweli aweze kuwatetea, hivyo basi uwezekano wa alichosema pale jukwaani kuwa kweli hilo sitoshangaa. Kinana ..............."sehemu hii imehaririwa"....kwa cheo kile alichonacho, Michuzi we ni mwandishi wa siku nyingi hili si geni kwako, je likitajwa hapa nalo ni TUSI? Waziri Mkuu alijiudhuru uwaziri mkuu, watu wakisema kwamba alijiudhuru je ni TUSI? Bania na hii
Mheshimiwa Amatus Liumba akata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi yake ya Uf...., Mh. Basir Mramba ashinda kesi ya matumizi mab....ya of... , ipo siku sehemu zilizohaririwa tutaambiwa nazo ni matusi. By Ankal ze coment chakachuwaz!
ReplyDelete