Meneja wa Kampeni wa CCM Bw Abdulhaman Kinana
(shati jeupe) akiwa na viongozi wa CCM mkoa wa Mwanza

Mwenyekiti wa Kampeni wa CCM Mh. Adbdulrahman Kinana ameeleza masikitiko yake dhidi ya CHADEMA kwa kuvunja maadili waliyosaini kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu, ambapo Bw. Mabere Marando ambaye ni Mwanasheria Kaongelea mambo ya EPA yaliyo mahakamani kinyume na Ethics za Taaluma

Amesdema katika taarifa ya habari ya TBC 1 kwamba CCM haiwezi kuongelea mambo yaliyo Mahakamani na kusisitiza ni vyema kutumia lugha isiyo ya matusi ili hata baada ya uchaguzi viongozi waendelee kuongea pamoja badala ya kukwepana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Jamani, jamani CCM hata kama ndiyo chama tawala basi msiambiwe ukweli???
    Inajulikana kabisa EPA ilikuwa mpango wa makusudi.
    TBC siwashangai kukata matangazo kwani nyie ni Radio ya Chama na wala siyo ya serikali.
    Najua kuna ulipaji fadhila ndani yake....
    People Power, sema Marando hata kama hawataki kusikia ukweli.
    Hata kama itachukua miaka, lakini iko siku wadanganyika hawa wataupata ukweli wa ufisadi wa CCM.

    ReplyDelete
  2. Hakuna matusi yoyote ambayo CHADEMA wameongea, walichoongea ni ukweli mtupu kuhusu EPA ambao CCM hawataki wananchi waujue.

    ReplyDelete
  3. USINIBANIE HII UNCLE,CCM WAACHE KULALALAMIKA, MBONA WAO WANAIMBA MPAKA NYIMBO ZA KEBEHI? WALIZOEA KUONA WAGOMBEA DHAIFU SASA WANAIPATA.

    ReplyDelete
  4. chadema hawajui siasa,wanapandikiza siasa za chuki sana,usituharibie nchi yetu,hebu angalieni cuf,wamekuwa wapinzani muda mrefu lakini wanafanya siasa za kistaarabu sana.chadema tarime kipindi kile walikuwa wanaimba kama kenya na slaa na zito wanashangilia.juzi wametaka kumpiga muandishi wa tbc,hiki chama kiko kama cha wavuta bangi,ndo maana wameweza kumpitisha mr 2 kugombea uunge mbeya,wakati ananyimbo mpya ya anti virus imejaa matusi na maneno ya ajabu,hivi mnafundisha nini kwa kizazi kijacho,shukuruni sana JK ni mstaarab,ingekuwa enzi za mkapa na uhakika hiki chama kingefungiwa.hata gazeti lao la tanzania daima kila siku watu wanalalamika kwa kuingiziwa mambo,mgaya wamemchafua vibaya.shame on you chadema.tanzania ni wapenda amani,tunataka siasa za kumwaga sera,sio matusi jukwaani.

    ReplyDelete
  5. Wapinzani wasiongee mambo yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi yetu kama EPA,RICHMOND,MEREMETA na TICS.
    Tunataka waongee vitu vya kawaida kama "mke wa rais wetu anaitwa SALMA; mtoto wake anaitwa Ridhwani,rafiki yake anaitwa LOWASSA na rais wetu anavaa miwani".
    Hayo mengine msiyaongee;kwanza ni ya jeshi.

    ReplyDelete
  6. KWA KWELI INGAWA MIE SI MSHABIKI WA CHAMA CHOCHOTE CHA SERIKALI,
    NIKWELI SIJAPENDEZEWA NA KAULI ZA CHAMA CHA CHADEMA,ILE SI KAMPENI BALI NI LUGHA CHAFU ZIMEWATAWALA WAMEPIGWA CCM HIO SIO VIZURI KABISA,YANI MI NIGEKUWA MWANACHAMA WA CHADEMA NINGESHAJITOA
    SIWEZI KUENDELEA KUSIKILIZA LUGHA CHAFU NAMNA ILE.

    ReplyDelete
  7. la sikuelewa kama mambo ya EPA ni matusi

    ReplyDelete
  8. Michuzi ni mtu usiyefaa kabisa inapofikia mahali tunaita 'bias' Maana CCM walipozindua kampeni ulimwaga picha kede kede. Leo Chadema wamezindua unaweka katangazo kama kitu cha mtaani. Mtu mzima aibu tupu. CCM hata kule Ngara ulitoa picha zao. Tanzania hatutafika mbali tukiwa na mabloga kama nyinyi. Najua huta-publish malalamiko yangu lakini ujumbe umeupata.

    ReplyDelete
  9. Ukweli Siku Zote Unauma..

    ReplyDelete
  10. sio kweli kwamba kitu kikiwa mahakamani hakitakiwi kiongelewe hapo kinana utakuwa na wewe unakosea kisichotakiwa ni kukijaji kitu kilichopo mahakamani,
    mabele marando taaluma yake ni mwanasheri sidhani kama atajuwa amekulupuka kwa kuongelea hilo pia hata mimi sioni ni kitugani kilicho wafanya msikitike kwa kuongelewa kwa EPA kwani kuna siri tena juu ya hilo?

    ReplyDelete
  11. CCM imeshikwa pabaya.
    Hakuna kufurukuta.
    Wanasema imekula kwao.
    Kwaherini CCM.

    ReplyDelete
  12. Maskini KINANA huyoooooooo kaishiwa hoja.
    CCM IMEFULIA

    ReplyDelete
  13. Hivi Kikwete alipozungumza kule Karagwe kuhusu jinsi serikali yake inavyoshughulikia rushwa na kujitapa kuwa wako viongozi wenzake wako mahakamani na akauliza "walijipeleka wenyewe?" alikuwa anazungumzia mambo yaliyo Kanisani?

    ReplyDelete
  14. Ahh CCM, kwani huo si ukweli. Mi nafikiri kampeni ni comparison, na kama CCM wana kesi za ufisadi sioni kwani zisiwe kigezo kikubwa kwa wapiga kura...

    ReplyDelete
  15. CCM oyeee !!ndio chama pekee chenye mwelekeo kwa wa-Tanzania..wengine kama hao chadema njaa tupuuu

    ReplyDelete
  16. CCM hakuna haja ya kujibu shutuma za Vyama vya siasa, Endeleeni kunadi sela zenu

    ReplyDelete
  17. Mdau MZALENDO kwikwikwikwi SHIKAMOO NIMECHEKA MPAKA NIMETAKA KULIA:::HASWAAAAAAAAAAAAAAAAAA na umesahau lingine kwao chalinze, anapenda kula nini ila sijui tukigusia pia mianguko itakuwa vibaya mdau MZALENDO au hahahahahahahaha yani umenichekesha mnoooooooooo

    ReplyDelete
  18. Ni juavyo mimi matusi ni kutaja viungo vya mwili ambavyo ni private, lakini kusema fulani,na fulani walihusika na wizi wa EPA hakuna tusi, labda Kinana ana kamusi yake mpya. Kimahaka ile inaitwa tuhuma, tangu lini tuhuma ya ubadhirifu ikawa TUSI?. Marando ni wakili wa utetezi wa baadhi ya washitakiwa Kesi ya EPA, ni wazi aliwahoji wahusika ili waseme ukweli aweze kuwatetea, hivyo basi uwezekano wa alichosema pale jukwaani kuwa kweli hilo sitoshangaa. Kinana pia mbona naye alipataga skendo ya biashara chafu za makampuni ya meli na leo hii yupo CCM kwa cheo kile alichonacho, Michuzi we ni mwandishi wa siku nyingi hili si geni kwako, je likitajwa hapa nalo ni TUSI? Lowassa alijiudhuru uwaziri mkuu, watu wakisema kwamba alijiudhuru je ni TUSI?

    ReplyDelete
  19. Mwanakijiji una hit the freakin nail on the head!!!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  20. CCM..... ELEZENI MAMBO YA EPA NA MENGINEO, MBONA SANA MNAJING'TA? SEMENI WAKATI NDIO HUO.....

    ReplyDelete
  21. CCM ZIIIIIIII CCM ZIIIIIII CCM ZIIIIIIII
    CCM CHINI CCM CHINI CHINI ZAIDI

    ReplyDelete
  22. HEKO BLOG KWA KUCHAKACHUA MAONI.

    ReplyDelete
  23. Waambieni watu wenu wamtumie Michuzi picha za vyama vyenu ataweka. Yuko kazini kwenye mambo ya serikali hivyo hawezi kuwa na picha za kila kampeni na kila chama.
    Mibichwa yenu ielewe na sio kuandika tu ovyo

    ReplyDelete
  24. Ankal nimeamini wewe ni Kada wa CCM,
    Lakini panapo ukweli lazima usemwe. Marando hana haja ya kuficha ukweli wenyewe. EPA inajulikana wazi ilikuwa ufisadi wa Wakubwa kuelekea uchaguzi wa 2005, upende usipende.
    Na TBC twaelewa wote mlengo wake uko chama gani, na Wakubwa lazima kulipana fadhila.
    People Power....
    Slaa, Marando semeni hata kama itawachukua miaka kuwaelimisha wadanganyika, naamini minyororo hiyo iko siku itakatika.
    Ankal ukibana na hii tena shauri yako
    Msemakweli

    ReplyDelete
  25. Mijitu mizima hovyooooo, kama mlizoea kukiuka maadili mbelke ya watoto mnategemea mtaendelea kupewa shikamoo, badilisheni nyendo zenu mtaheshimiwa, wanablog wengine hovyooooo kabisa, sasa amani itavunjikaje ina bidi tukupeni maana halisi ya amani kwani najua hamjui kwa sababu amani hujawahi kuipata na hujui utamu wake

    ReplyDelete
  26. Hii comment imehaririwa maana ya mwanzo Michuzi umeibania, naendelea..
    Ni juavyo mimi matusi ni kutaja viungo vya mwili ambavyo ni private au kuhusisha akili na weledi wa mtu, lakini kusema fulani,na fulani walihusika na wizi wa EPA sidhani kama kuna tusi, labda CCM wana kamusi yao mpya. Kimahakama ile inaitwa tuhuma, tangu lini tuhuma ya ubadhirifu ikawa TUSI?. Marando ni wakili wa utetezi wa baadhi ya washitakiwa Kesi ya EPA, ni wazi aliwahoji wahusika ili waseme ukweli aweze kuwatetea, hivyo basi uwezekano wa alichosema pale jukwaani kuwa kweli hilo sitoshangaa. Kinana ..............."sehemu hii imehaririwa"....kwa cheo kile alichonacho, Michuzi we ni mwandishi wa siku nyingi hili si geni kwako, je likitajwa hapa nalo ni TUSI? Waziri Mkuu alijiudhuru uwaziri mkuu, watu wakisema kwamba alijiudhuru je ni TUSI? Bania na hii

    ReplyDelete
  27. Mheshimiwa Amatus Liumba akata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi yake ya Uf...., Mh. Basir Mramba ashinda kesi ya matumizi mab....ya of... , ipo siku sehemu zilizohaririwa tutaambiwa nazo ni matusi. By Ankal ze coment chakachuwaz!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...