Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi(CUF) na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akionyesha kwa waandishi wa habari ilani ya uchaguzi wa Chama hicho ya mwaka 2010 jana jijini Dar es salaam .Kushoto ni Mgombea mwenza wa CUF Juma Duni Haji na kulia ni Mkurugenzi wa Siasa Taifa Mbarala Maharagande.


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi(CUF) na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akizindua jana jijini Dar es salaam ilani ya Chama hicho ya mwaka 2010.Kushoto ni Mgombea mwenza wa CUF Juma Haji Duni na kulia ni Mkurugenzi wa Siasa Taifa Mbarala Maharagande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. HUYU LIPUMBA ANA TAMAA SANA YA URAISI ,YAANI NI MARA YA NNE SASA ANAGOMBEA.HAONI KUWA WATU HAWAMTAKI?

    CHA KUJIULIZA KUWA NITAMPAJE KURA YANGU PROFESA LIPUMBA MTU AMBAYE HAJAWAHI KUWA DIWANI AU MBUNGE.NITAJUAJE KUWA LIPUMBA ATAKUWA KIONGOZI MZURI WA NCHI HII.HANA REKODI ZA UONGOZI WA NCHI HII.AFADHALI YA SEIF SHARIF HAMAD ALISHAKUWA WAZIRI KIONGOZI.LIPUMBA KILICHOBAKI AKAFUNDISHE TU UCHUMI AU KUSHAURI BASI ,URAIS HATAUPATA NG'O.
    Nicholas Kimara-DSM

    ReplyDelete
  2. mie naona hawa jamaa wana nia ya kupunguza kura za dr slaa. hivi lipumba haoni anachakachua uchaguzi. hata mrema ameona inatosha. kuwania urais mara nne ni tamaa. ni vema awaache akina-Slaa wafanye vitu vyao. enzi zake za kina mrema na cheyo kwishne.

    hivi kuna mtu duniani amewahi kugombea (kuwania) urais mara nne akiwa siyo rais?

    ReplyDelete
  3. profesa tuko nyuma yako,kura zetu unazo usjali,japo wapinzani nao wamekuwa maadui zetu tusikate tamaa.

    ReplyDelete
  4. KITU KINACHOFANYA NIMKUBALI PROFESA LIPUMBA NI KUWA MU WA KUMWAGA SERA,ANASEMA ANACHOTAKA KUWAFANYIA WATANZANIA,SIYO VYAMA VYINGINE VYA UPINZANI HAVINA SERA WAMESIKILIA UFISADI,WATANZANIA WANATAKA SERA,SIO KELELE,PRO LIPUMBA NDO ALOANZISHA KUFICHUA UFISADI NCHI HII LAKINI ANASONGA MBELE NA SERA MPYA,YEYE NDO ALOFICHUA NDEGE YA RAIS,RADA,UBALOZI ITALY NA BARICK.

    ReplyDelete
  5. jk ndo rais,hilo lipo wazi,lakini pro lipumba ni chachu ya kumpunguzia kikwete ushindi wa kishindo,nakumbuka 2000 pro lipumba ulimfanya mkapa apate only 67 ya kura,na 2005 ulimpunguzia kikwete pia asilimia zake,hatutaki mambo ya kagame bongo kupata asilimia 94

    ReplyDelete
  6. Prof Lipumba hauna jipya kabisa. CUF mnahitaji kutia nguvu Zanzbar ambapo kuna dalili ya kushinda.Tanganyika Mh Lipumba unapoteza pesa na muda bora umuunge mkono Dr Slaa. Mh Lipumba bora uende ukagombanie ubunge against Prof Kapuya ili elete changamoto bungeni.

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi hongera SANA umetukumbuka wana CUF safi sana. Mzee upo juu sana kweli hii ni blogu ya jamii. Bravo mkuu

    ReplyDelete
  8. yaliyomo yamoAugust 27, 2010

    ilani ya chama mbona ina picha za watu???
    chama hakina logo yake???

    ReplyDelete
  9. ooh Chadema matumbo joto, matumbo joto, wakati wenzenu wakikwambieni tushirikianeni kwa ubinafsi wenu hamtaki leo mnaona kuwa hakuna dalili ya Dr Slaa kushinda. Mmemponza kaacha kugombea ubunge na saa zenyewe za majeruhi hizi (uzee ushamnyemelea) Sasa mwamdanganya mtampa ubunge mkewe si rushwa hiyo mnamhonga mkewe ubunge wa viti maalumu. Na bora mvipate hivyo viti ama sivyo huko ndani kwa Dr. Slaa patakuwa hapatoshi!

    Mwisho CUF ni chama pekee cha upinzani Tanzania chenye mwelekeo wa kueleweka sio nyie msokuwa na sera zaidi ya wimbo mmoja kama santuri iliyochuja! Sidhani hata kama wanajua santuri ni nini?

    Haya vijana wa Chadema jibuni swali hili,

    SANTURI ni kitu gani?

    ReplyDelete
  10. Hao ni vibaraka na wapenda ukabila na udini lakini kwa siasa ni Lipumba baba daktari bingwa wa uchumi na siyo daktari wa historia ya kanisa katoliki Padri Slaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...