
Asalaam Aleuikhum Ankali
Hivi hili suala ya kupita service road traffic wamelishindwa au vp?hebu ona hapo pichani njia ya kinondoni karibu na ubalozi wa india madaladala yanapita hata bila wasi.Hivi wiki ya nenda kwa usalama ndio imeisha au traffic wapo likizo.
Me naona wamejazana njia ya Ali hassan mwinyi na hizi njia nyingine wamezisusa.
Naomba kutoa hoja.
Mdau Mac Temba Jr
Sent on the move from my BlackBerry® smartphone
Hivi hili suala ya kupita service road traffic wamelishindwa au vp?hebu ona hapo pichani njia ya kinondoni karibu na ubalozi wa india madaladala yanapita hata bila wasi.Hivi wiki ya nenda kwa usalama ndio imeisha au traffic wapo likizo.
Me naona wamejazana njia ya Ali hassan mwinyi na hizi njia nyingine wamezisusa.
Naomba kutoa hoja.
Mdau Mac Temba Jr
Sent on the move from my BlackBerry® smartphone
from Vodacom Tanzania


pole sana mdau kwa kuumiza kichwa kiasi hicho hayo yote ni matokeo ya rushwa,uzembe,ujinga,miundombinu mibovu,madereva kutojua sheri, watu kujiamulia watakavyo,polisi kulala usingizi,tuna watunga shria lakini hakuna walinda sheria na mika inavyozidi kwenda mbele ndio hali itazidi kuwa mbaya zaidi usishangae na itachukua miaka zaidi ya 60 kuondoa matatizo kama hayo so JUST RELUXY MEN
ReplyDeletete te te! haya matukio ni characterists of third word countries bila mambo kama hayo tanzania itakuwa sio nchi ya dunia ya tatu
ReplyDeleteIli upate msaada wa uhakika kwanza fafanua hili. Je? Hilo tatizo limekuanza sasa wakati wa mfungo au hata siku za kawaida? Inawezekana kufunga huko!!!
ReplyDeleteNaogopakukubali kwamba hizi ni tabia za dunia ya tatu, ni tabia za watanzania kwasababu drivers wetu siyo professional, wamepata driving license kwa kununua, tembea nchi nyingi za kiafrica kama Ghana, Lesotho, Ethiopia, Botswana, Sudan na nyingine nyingi upumbavu wa aina hii hawana na third world Countries!!! hapa hatuhitaji msaada wa polisi tunahitaji mtu katili kusimamia sheria, pata mkuu wa mkoa mwendawazimu na waziri wa mambo ya ndani katili kabisa ili kama inawezekana drivers wa namna hii wachapwe viboko na kuondoa kabisa gari yake barabarani kwa kipindi cha miezi hata mitatu na fine juu. hakika kama mtu anajua thamani halisi tunayotumia kujenga barabara zetu asingekumbatia uhuni unaofanywa na drivers wetu, kwani ni kuhujum uchumi wa nchi yetu na miondombinu.
ReplyDeletekuna afande anaitwa samuel ndiye anasababisha hayo yote, anawaweka kwenye foleni dakika 30-40 kwa hao watu wanaotokea kinondoni, mtu anatoka mwenge anatumia dakika 20 wa kinondoni 40, acha watanue na trafiki waendelee kuzuia magari yanayotokea njia ndogo na kuruhusu magari ya barabara ya ali hassan mwinyi
ReplyDeleteHaya ndio matatitizo ya kuona "sharia"inakiuka haki za binadamu.Muda mwingine tutumia "sharia". sheria watu hawaziogopi!
ReplyDeletekaka michuzi
ReplyDeleteMi nadhani ile system ya fine ya 200,000 au jela irudi tena na polisi wangekua wana fanya hilo zoezi mara kwa mara inasaidia. Kwa mfano siku hizo foleni pale morogoro road mataaa ya ubungo watu wamekua wastarabu huoni mtu anapita pembeni hata kama traffic hayupo si daladala wala watu binafsi.
Mdau Bongo Forever
MTAZAMO WAKO NDIO UNAOKUSUMBUA, HAPO KWENYE PICHA ULIYOTUMA KUNA MAGARI SABA KAMA SIKOSEI (MADALA DALA MANNE NA GARI NDOGO TATU) UNGELIKUWA NA MTAZAMO SAHIHI UNGESEMA MAGARI YANAYOPITA PEMBENI NA SIO MADALA DALA.
ReplyDeleteMTAZAMO KAMA WAKO NDIO UMESABABISHA TATIZO LIWE SUGU, MAANA NI KWELI MADALA DALA YALIACHA KUPITA PEMBENI LAKINI GARI NDOGO ZIKAWA NDIO ZIMEFUNGULIWA NJIA, NA KWA KUWA HAWA NI WAFANYA BIASHARA ILIWABIDI NA WAO KUREJEA KWENYE NJIA HIZO ILI WAKIDHI MATAKWA YA MATAJIRI NA WAO WAWEZE KUPATA PESA KIDOGO YA KUJIKIMU (KUMBUKA MADEREVA WA MADALA DALA HAWANA AJIRA YA KUDUMU)
TATIZO KUBWA NI TRAFFIC WETU. WAJIPANGE UPYA NA IKIWEZEKANA WARUDISHWE MAFUNZONI ILI WAJUE NINI CHA KUFANYA, NATAKA NIKUPE MFANO TRAFFIC ANASIMAMISHA MAGARI YA (MAIN ROAD)NA KUITA MAGARI YA (FEEDER RD)TENA WAKIONA STK, STH, RANGE, PRADO, LANDCRUISER ETC WANACHANGANYIKIWA KABISA WALA HAWANA UJASIRI WA KUWAULIZA KWANINI ANAPITA PEMBENI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE. AMEN
Hii shughuli naona wangetupa wajasiriamali tu. Tunakamata magari na kutoza faini then tunagawana revenues. Kazi inaweza kufanywa kiulaini bila utemi na kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Kwa hesabu ya haraka haraka Jeshi la Polisi litaingiza 10m kwa siku kwa DSM pekee ambazo zitasaidia sana kuboresha Jeshi hilo.
ReplyDeleteKWELI WATUNGA SHERIA TUNAO NA SASA HIVI WAKO KWENYE MCHAKATO LAKINI KINACHOKOSEKANA NI NANI ATALINDA HIZO SHERIA?
ReplyDeleteKweli hiyo ni tabia ya nchi za Dunia ya tatu.Leo nenda Masaki ukashudie jinsi inavyobadilishwa! ni msururu wa Maduka, Mabaa, migahawa mama Ntilie, Club za Usiku...yaaani you name it, hata Dada poa (changu Doa) nao wanaonekana mitaa hiyo, yaaani hovyo kabisa na watunga sheria wapo na wanatizama tu. Kisha wanakuja na kampeni "ifanye kinondoni kuwa safi" Kila mahali panabadishwa mandhari yake na waheshimiwa wapo wanatizama. Sasa hivi kuna fashion imeingia ya kujenga "APARTMENTS" basi zinapigwa kila mahali hawjali nini wala nini......wazee wamesha pozwa! yaani HOVYOO KABISA!!!
ReplyDeleteMkaanga MBUYU.
hilo sio tatizo lao.dar kako overpopulated na hakuna haja ya kuwalaumu hawa jamaa.. maana bila hivyo foleni itaanzia getini kwako,cha maana nikuondoa ofisi hasa za selikali na kuzisambaza pembeni ya mji ili kuanzisha mji mpya! ni hayo tu....
ReplyDeleteHapa Jamni Ndugu zangu wanajamii wenzangu!! Tusiangalie tulipoangukia Ila tuangalie tulijikwaa wapi! HII Mifolen imetoka wapi na Itaisha vipi ndio la msingi!! We unadhani hata mie ntaacha kufurahi dereva akitanua wakati nataka niwahi FUTARI!! Nini Kifanyike Kuondoa Hizi Foleni Thats the case.Binafsi wazo la kuanzia Trafic Light ziwe perfect askari waondoke kwenye makutano ya barabbara!! Wanajisahau saana we unaita upande mmoja nusu saa!! Unategemea nini kitatokea
ReplyDeletewewe mdau uliyeleta habari hii mi naona unatangaza biashara , maana ooh sent by my blckberry from vodacom, sisi inatuhusu nini ? au ndo vodacom wamekuajili wanakupa chakula chako ?
ReplyDeleteankal na wewe edit coment zingine...
SISI TUNAOPITA BARABARA HIYO NDIO TUNAOJUA TATIZO ,TRAFFIQ WA PALE KWENYE MAKUTANO YA STANBIC NA NJIA YA KWENDA OYSTERBAY NDIO WAZEMBE UNAWEZA KAKUTA FOLENI IKO KWA MANYANYA SASA UTAFANYA NINI? TRAFFIQ ANAITA BARABARA YA A.H MWINYI TU KAMA VILE UPANDE MWINGINE HAUNA MAGARI SIELEWI SABABU AU KUNA HAWARA ZAO WANAPITIA BARABARA YA A.H MWINYI.
ReplyDeletembona hata marekani wanaendesha breakdown lane
ReplyDeletekaka hayo yote ni kutokana na sera mbovu, hapa mjini tunaye Planing Engeneer ambaye serikali inamlipa pesa lakini kutokana na ujinga alio kuwa nao yeye anakubali kutoa vibali vya majengo marefu mjini wakati haangalii uwezekano wa kufika hapo upo vipi, ni upumbavu mkubwa sana halafu tunasema ni maendeleo? huo ni ujinga tena kama ingekuwa serikali ina watu wenye akili kitu kama hiki Planing Engeneer anatakiwa kuwajibika kwa hili.
ReplyDeleteWapi tatizo, serikali yetu kama akitokea kiongozi akawaambia ukweli basi huyo atakuwa adui yao,
suala la trafiki kulala au wamesahau njia au sijui hawakai vichochoroni hilo halina maana kwa kuwa tunatakiwa kuondoa tatizo sio kufunika
Nyie watanzania mnosema watunga sheria mnoa mmewaona wapi? Wanaotakiwa kutunga sheria ni bunge bunge lenyewe miaka yote mitano wanajadili kuhusu ufisadi au kupitisha bajeti.Lini uliona wabunge wakijadili kuhusu kutunga sheria. Sheria ya uchaguzi wala haijatungwa na bunge.Tanzania tunawabunge wlioishia darasa la saba na wengine wengi darasa la 12 hawana upeo wowote kuhusu sheria yeyote ile na hao wenye upeo kidogo wako busy kusinzia bungeni unafikiri kuna sheria itatungwa hapo? Acheni kujidanganya jamani.
ReplyDeletehii inasababishwa na yule traffic flani anaitwa sjui afande nani huko, akikaa pale taa za stanbic asubui anaita watu wa barabara ya Ali Hassan mwinyi tu anasema wanaotokea barabara ya Mwananyamala hawaendi makazini wanakwenda feri kununua samaki kwa hiyo hawana haraka, ila ana wanawake zake wakimpigia simu nipo kilimaaani hapa makaburini anaivuta foleni na anamwambia ukipita nipungie mkono akipita tu yule mtu wake anasimamisha tena. so madereva hawana budi kufanya hivyo coz hakuna usawa hapo mdau ulielewe hilo.
ReplyDeleteJamani, sio kama ni masuala ya third world country, ni kwamba hiyo njia hua inasahaulika saana hasa wakati wa asubuhi, kuna trafic mmoja hua yupo pele kwa jina ni Samweli sio siri hua anatutesa wakazi wa njia ile, halafu eti hua anaongea kwa kejeli kua gari za mwananyala hubeba watu wanao enda feli tu kununua samaki, hua hawana hara. kwakweli kitu ambacho sio sahihi, hata kama ni kweli wanafuta samaki ndo ajira yao sio lazima kila mtu akae offini. Huyo akikutana na wananchi wenye hasira kali watamfanya kitu mbya kama alichofanyiwa alivyokua mataa ya pale ubungo.
ReplyDeleteMkereketwa