
Viongozi wa CUF wakishanglia baada ya kurejesha
fomu za Profesa Lipumba kugombea urais wa Tanzania bara

Sehemu ya umati wa wana CUF wakisindikiza wagombea wao

Mgombea urais wa CHADEMA Dk Wilbroad Slaa akitoka kurejesha fomu

Wana CHADEMA wakiseherehekea kuruejesha fomu mgombea wao

JK akiwashukuru wanachama wa CCM waliojitokeza kumpongeza kwa hatua ya kurejesha fomu katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi leo na pia kukubaliwa kama Mgombea halali wa CCM katika uchaguzi ujao.

Mgombea Mwenza wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Dkt Mohamed Gharib Bilal akiwashukuru wanachama wa CCM na wapenzi waliofika leo katika viwanja vya Ofisi Ndogo ya CCM jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwapongeza kwa kukubaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania kuwa wagombea kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi ujao.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba (kushoto) akiteta na Mwenyekiti wa CCM, Dkt Jakaya Kikwete leo nje ya Ofisi Ndogo za CCM jijini Dar es salaam mara baada kurejea kutoka Tume ya Uchaguzi alipokuwa amerudisha Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao.

Msanii Ummy Wenceslaus (Dokii) akitumbuiza leo mchana jijini Dar es salaam mbele ya baadhi ya wanachama waliofika katika Ofisi Ndogo za CCM kuwalaki wagombea wao mara baada ya Rais Kikwete na Mgombea Mweza Dkt Bilal kurejea kutoka Tume ya Uchaguzi ambapo alikuwa wamerudisha fomu za kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwasikiliza wagombea wao wakati walipokuwa wakihutubia maelfu wa wanachama wao katika ofisi ndogo ya chama CCM Lumumba.
(Picha na Tiganya Vincent-Dar es salaam)
Hata ubane kuweka picha za Dr.Silaha kurejesha fomu tunamchagua yeye, Michuzi acha kuwa biased kiasi hicho,umejaza mipicha ya ccm tu.
ReplyDeleteWeka na za Dr.Silaha a.k.a Mabunduki
we mshamba nani atamchagua slaa,labda wewe na familia yako,fungueni blog yenu basi mumuweke huko,mara mia lipumba kuliko huyo slaa.anyway rais ni jk,
ReplyDeleteNilidhani mgombe urais wa zanzibar ni Dr. Sheni na Dr. Bilal ni mgombea mwenza au nimeelewa vibaya. Hebu fafanua maana tofauti hapo ni kubwa mnooo!!
ReplyDeleteMdau AB, Canada
Tukananeni mnavyoweza ila Padri Slaa atashika nafasi ya 3 tu sina haja ya kusema wa kwanza atakuwa nani.
ReplyDeleteKaka Michuzi naona unadhihirisha U-YANGA wako!!!
ReplyDeleteUnasahau michuzi anafanyia gazeti la serikali?? Wanapewa instructions za kum cover zaidi mgombea wa CCM, otherwise atapoteza kazi. Akina Slaa hata kwenye magazeti wanawekwa kwenye kurasa za ndani tena picha ndogo na jk anawekwa front page picha kubwa!!!!!! Hii ndio media yetu bwana.No fair play in practice ila theoretically!!!!!!
ReplyDeleteHEKO Fri Aug 20, 01:17:00 AM KWA MSIMAMO WAKO WA UDINI ILA TU ULICHOKOSEA NI KUWASEMEA WATU WENGINE WENYE AKILI NZURI KUWA HAWATAMCHAGUA SLAA.
ReplyDeleteCCM wanajaribu kujenga hoja kwamba Slaa asichaguliwe kwasababu ya udini. Ukweli ni kwamba JK na Lipumba hawawezi hata kumfunga viatu Dr. Slaa. Yaani kawazidi kiakili na utu. Afadhali hata ungesema Lipumba awe raisi sio huyo mkwere anaeharibu nchi. Haya michuzi nibanie upate faida maana uCCM umekukithiri.
ReplyDeleteHaijalishi CCM siku zenu zinahesabika!!!!!Silaah atatetemesha uchaguzi huu tunajua hata kama akishinda mtaiba kura lakini i can bet miaka 20 ijayo Raisi sio wa CCM.CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!mi nawapotezea CCM uchaguzi huu mpaka washangae kuanzia udiwani.They are the reason behind all the sufferings we have here
ReplyDeleteNchi hii hatujafikia demokrasia ya kumpa mpinzani kuongoza dora, regardless matokeo ya kura. Ndio maana CCM wanafanya wanavyotaka wakijua wanaweza kudhibiti matokeo ya kura. Mifano inafahamika
ReplyDeleteKitu kimoja kinachosahaulika hapa ni kwamba wapiga kura wengi wapo vijijini, na sina uhakika ni wangapi huko wanaomfahamu Dr. Slaa au CHADEMA yake. Kosa kubwa la vyama vya upinzani ni kujikita mijini na kusahamu kuweka mitandao na kujitambulisha vijijini. Baba wa Taifa alikuwa na akili sana kuanzisha mabalozi wa nyumba kumi kumi enzi zile.
ReplyDeleteVyama vya CUF, CHADEMA, NCCR Mageuzi na UDP vimekuwapo kwa muda sasa lakini vingine havina hata ofisi wilayani. Kwa mwendo huu itachukua muda mrefu sana kushinda ngazi za kitaifa.
Ni kweli Dr. Slaa ameleta msisimko tena katika kambi ya upinzani lakini utabakia hivyo tu - msisimko!
UCHAGUZI WA BONGO UNABORE SANA KWA SABABU HAKUNA LOLOTE JIPYA ZAIDI YA USHABIKI KAMA WA SIMBA NA YANGA. LABDA VIZAZI VIJAVYO NDIYO KUTAKUWA NA JIPYA.
ReplyDeleteMABADILIKO YANAANZA NA KURA YAKO. TUNAWEZA.... KAMA UNAKIPENDA CHAMA CHA MAPINDUZI KAMA ALIVYOKIPENDA MWALIMU NYERERE, BASI, KURA YAKO MPE MPINZANI MWAKA HUU... KAMA NYERERE ALIVYOTETEA VYAMA VINGI KWA LENGO LA KUIMARISHA CCM.
ReplyDelete1. IMARISHA CCM, CHAGUA UPINZANI.
2. IMARISHA DEMOKRASIA NA UTENDAJI WA BUNGE, ONGEZA WAPINZANI BUNGENI
USIFANYE AJIZI, THUBUTU ULETE MABADILIKO CHANYA.
Hakuna lolote la maana huko kwenye Upinzani, yaani ni aina au njia nyingine ya ulaji tu.
ReplyDeleteKinachonishangaza mke wa Dr Slaa amehamia Chadema hivi karibuni tena mwezi huu huu wa August baada ya kushindwa kwenye kura za maoni za wabunge huko Hanang, yaani alishindwa na Dr. Mary Nagu. Tena hapo hata baada ya mumewe kuwa mgombea wa urais kupitia Chadema. Kama kweli hiki chama ni cha maana kwanini huyu mama alikuwa Diwani wa CCM huko Basuto miaka yote hiyo? Hakuoona uzuri wa Chadema? Au kuna nini ndani mwake? Je kama Dr Slaa asingegombea urais huyu mama angeendelea kubaki CCM au kama angeshinda kura za maoni huko Hanang angebaki CCM au angeenda Chadema?
HII PEKE YAKE INAONYESHA KUWA HATA HUYO DR SLAA ANAANGALIA MASLAHI YA FAMILIA YAKE KWANZA, MSIMPAMBE MTU SIFA ZA UTAKATIFU WAKATI HANA. KAMA CCM NI MAFISADI BASI HATA MKEWE DR SLAA ALIKUWA KWENYE HILO KUNDI MPAKA MWEZI HUU ALIVYOTOKA.
Na nyie wenye kugubikwa na mawazo mgando kuwa wanasiasa ndio watawaondolea umasikini wenu badala ya kuondoa umasikini wao mmeliwa huku mnajiona!
KWA COMMENT NILIZOZIONA KWENYE MAONI YA ZITTO KABWE KUTOKA KWA WANACHAMA WA CHADEMA, SINA HAJA YA KUCHAGUA CHAMA CHENYE KUBAGIANA WENYEWE KWA WENYEWE HUMO NDANI.
ReplyDeleteCHAMA CHENYE WANACHAMA WANAOONA KUWA UPINZANI NI UADUI WA KUKATANA MAPANGA! UADUI WA KUTOSALIMIANA WALA KUPEANA MAJI, NA UADUI WA KUTOONGEA NA WANACHAMA WA VYAMA VINGINE NA UKIONGEA AU KUSHIRIKIANA NAO UTAITWA MSALITI.
CHAMA AMBACHO WAO WENYEWE WANACHAMA WANAOWAONA VIONGOZI WAO WA JUU KAMA ZITO KABWE ANA KIBURI JE HUYO DR SLAA AKISHINDA ATAUNDA SERIKALI NA KINA NANI KAMA SIO HAO HAO WENYE VIBURI?
IKIWA NYINYI WENYEWE HUMO NDANI HAMUAMINIANI NANI ATAWAAMINI HUKU NJE?
ni ndoto ya mchana kwa Dr. Slaa kuwa Rais Tanzania, masikini wee mmemchuuza mwenzenu Ubunge kakosa, jimbo la Karatu litakwenda kwa Dr Wilbord Slaa Rorry na badala ya kuongeza wabunge wa upinzani bungeni ndio mmepunguza na huyo ndio mwisho wa kisiasa wa Dr. Slaa maana atakuwa hana msisimko tena kama alivyokuwa Mwenyekiti wake Mbowe!