It’s day 37 on M-Net’s Big Brother All Stars ---and the housemates and the barnmates have been given their latest task --- creating their very own radio station!Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Code, Sheila and Uti


Huyu jamaa Uti BABA yake kafa, badala ya kwenda kumzika bado yuko kwenye hilo jumba tu ana show love.Jamani kuna watu kweli mambo ya kidunia yamewameza. Na yale maneno kwamba watu wa nchi nanino ambayo huyu jamaa katoka wanasaka pesa kwa udi na uvumba ndio nimedhihirisha kwa huyu. BABA yako kafa wewe bado tu unang'amg'ania show. Kwa maana hiyo hata mke au mtoto wako anaweza akafa na wewe ukaendelea kutafuta pesa. Yaani baada ya kutokwenda kwenye msiba wa baba yake kwa sasa kila anachofanya mimi namuona mnafiki tu. Mara ajifanye mtu wa dini, mara mpole, lakini hakuna kitu, ni unafiki tu.Na si ajabu aka.....na huyo Sheila. Jamani si kama namsagia lakini amenikera sana! Na hao Big Brother inabidi wawe na rule kwamba mtu ukifiwa na wazazi uruhusiwe kwenda kuzika na kurudi. La sivyo hiyo show yao itakuwa kama NYUMBA YA KISHETANI...!!
ReplyDeletemdau wa kwanza usilaumu sana , inaweekana hawajamwambia, sidhani kama angejua asingetoka humo ndani fasta, maana hao si hawatakiwi wajue nini kinachoendelea duniani ni mumo kwa mumo
ReplyDeletemi naona kuna kila sababu ya Big Brother mwenyewe au hao wanaija kumfagilia sana huyo Uti ili end of the day awe mshindi labda kwa kuwa kamptoteza baba yake akishinda iwe kama pole yake.lkn kwa ukweli kabisa hain etertain chochote ni boring plus. halafu na sisi watanzania hatupigi kura wala kutuma msg kuonyesha support kwa mshiriki wetu, well labda kwa sababu wenye ving'amuzi ni wachache au kuna sababu nyingine sijui lakini kwa kweli katika house mates wote Mwisho yuko real na wala ha act, watanzania tumuonyeshe support basi.
ReplyDeleteBig Brother walimpa fursa kama angetaka angepewa siku nne aende kwao na kurudi ili aendelee na mchezo na lakini alichagua kubaki mjengoni kusaka mkwanja.
ReplyDeleteWe anonymous wa kwanza inaonekana hata show yenyewe hauifuatilii, Big brother alimpa option ya kwenda kuzika na kurudi kwa hiyo anasubiria siku ya mazishi ifike ili aende na kurudi. Navilevile kabla hata hajafariki kunasiku Uti alikuwa anasema babayake ni mgonjwa sana na yeye Uti alikuwa anataka asishiriki kwenye show kwasababu baba yake alikuwa mgonjwa ila babayake akampa ruhusa ya kushiriki. kwahiyo itakuwa ni haina tija kama uti akiamua kujitoa kwenye show ambayo babayake alimruhusu kushiriki wakati wa uhai wake ilihali amepewa option ya kwenda kumzika na kurudi.
ReplyDeleteMchangiaji wa kwanza, hata mimi nilishangaa na kustuka sana kuona kuwa Uti ameamua kubaki katika jumba la BBA baada ya kufiwa na baba yake mzazi!!!!!!! huyu lazima awe ana roho ngumu sana na moyo wa mawe!!! Vinginevyo itakuwaje mtu uanze kuimba na kufanya utani na kupapasana na wanawake siku mbili tu baada ya mzazi kufa? Wa-TZ, tujichunge sana tusije tukapoteza utu wetu kwa ajili ya pesa. Tutafute pesa na kufanya kazi kwa bidii lakini tusifike kiasi cha kuwa na nyoyo za mawe kama Uti au wale wafuasi wa shetani wenye kuua ndugu zetu maalbino kwa imani za giza.
ReplyDeleteNi kweli kabisa...huwezi kufiwa na mzazi wako aliyekuzaa na kukulea halafu ukaendelea tu na business as usual. Huyu uti labda anahitaji msaada wa tiba ya akili.
ReplyDeletebaba yake kumruhusu kushiriki kabla hajafa si hoja sababu alifikiri Uti akishinda atakuwa mzima wale hela wote. Kwa yeye kupewa option ya kutoka na kukataa ina maana ana usongo na hizo hela. Angetoka ndio angekua kajitoa. Lawama kwa Big brother ni kutowaruhusu kutoka na kurudi kama wana dharura
ReplyDeleteme ata sielewi!!wala sifatilii huu uhuni wa waziwazi.watu wanalalana kama vyura?
ReplyDeleteNakubaliana na anon aliyesema hapa juu kuwa labda Uti anahitaji kumuona psychiatrist. Huwezi kufiwa na mzazi wako kisha baada ya masaa 12 uanze kucheka na kufanya masihara. Ama kweli wahenga walisema duniani kuna mambo. Walioshangaa ya Nabii Musa/Moses sasa wanayaona ya Firauni. (there'll always be something to amaze you). Vedasto M.
ReplyDelete