Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi,Ramadhan Khijjah akioyesha kwa wadau mbalimbali chapisho linaloelezea jinsi ya kupata taarifa kwa njia ya tovuti zinatoa ufafanuzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Misaada ( Aid Management Platform System) inayotolewa na wahisani mbalimbali kwa Tanzania. Mfumo huo utawawezesha wadau mbalimbali kupata taarifa sahihi ya misaada yote inayotolewa na wahisani kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Misaada ( Aid Management Platform System) inayotolewa na wahisani mbalimbali kwa Tanzania. Mfumo huo utawawezesha wadau mbalimbali kupata taarifa sahihi ya misaada yote inayotolewa na wahisani kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania,jijini Dar es Salaam leo.

mfumo sio? badala ya kutangaza mkakati wa kwakamata wale wanaokwamisha maendeleo yetu unatangaza mfumo wa kupata habari! Kwani tofauti na sasa ni ipi kwa sababu hata leo nikihitaji information nitapewa vitabu tena vime balance vizuri kabisa.
ReplyDeletePathetic
Hii ni kali ya mwaka!!! sasa omba omba amekuwa more organized kiasi ametengeneza chombo kitakacho ratibu kinachopatikana kwenye bakuli... nchii hii bwana. Badala yakusimamia raslimali zetu (BANDARI TATU, MADINI, RAILWAYS, AGRICULTURE, FISHING ETC) ilikuongeza pato la nchi, lakini sasa tuko bize kuratibu misaada. hebu na bunge lianze mara mora tunaikosa misemo yaoo kama hii
ReplyDelete1. tumekwishaanza mazungumzo na wafadhili....
2. endapo mfadhili akipatikana...
3. mradi umechelewa kwa kuwa wafadhili wamechelewa kuachia fungu
4. tunawashukuru wafadhili kwa misaada.
5 Wafadhili wame suspend misaada kwa sababu ufisadi...
Lakini yote hayo watanzania tumekaalia uchumi. Katibu mkuu achakupoteza muda wa walipa kodi fanya kazi kuongeza pato la taifa kwa uzalishaji sio hiyo ya omba omba.
....at mature age (as a country) we are still aid dependent, 40% of the budget!!??
ReplyDeleteMtoto/mtu akifikisha miaka kama hiyo hajatembea huwezi ukasema ni mchanga, bali ni crippled, incapacitated. Hivyo apelekwe kwenye maabara/theater (kama inawezekana) awekewe miguu ya plastic.
Tuko bize na platform au mikakati ya misaada!! Tuone aibu!!
Inachekesha tunaspend money kutengeneza kitabu na tovuti ya kuangalia mabakuli yamepita mtaa upi na upi.
ReplyDeletemabakuli yamekua mengi kiasi kwamba tunahitaji controlling cabinet....
kweli huyu mtoto sijui alikua ni wa mwisho hataki kutembea kabisa...
RIP Tanzania
ReplyDeleteHaya yanatokea baada ya wazungu kugoma kutoa misaada ndiyo mnaana wanakuja na danganya toto,tunahitaji viongozi wabunifu siyo siyo utapeli wa tics na mashirika mengine, tunaweza kujiendesha wenyewe mfano bandari ipanuliwe na kuamishiwa Bagamoya, ilipo sas na kituo cha polisi cha kati iwe ni sea front ambayo itavuta watalii wengi sana, bandari ya mtwara itumike kwa mizigo ya zambia na zimbabwe hata mikoa ya kusini, reli iendelee na kuwe na mpago mahususi wa kuwa na meli zaidi kama mv umoja kusafirisha mizigo ya uganda,haya yakafanyika hatuna haja ya kusukumwa na wazungu.
ReplyDeleteMdau kutoka Bukoba.
Yaani inatia kinyaa!Mnachowaza masikini ni kutembeza mabakuli tu!
ReplyDeletekaka naona hii blog imekuwa ya ccm
ReplyDeleteyamejaa mambo ya chama hicho tu au nawe umetishwa kama yaliotokea uchaguzi wa yanga