Benjamin Sawe,
Dar es Salaam
Msajili wa Vyama vya siasa nchini Bwana John Tendwa amesema ataviwekea pingamizi Vyama vya siasa na wagombea wa Ubunge na Urais kwa Tume ya Uchaguzi kutoshiriki kampeni ikiwa vitachelewesha kujaza hati ya kiapo cha matumizi ya fedha wakati wa kampeni.
Bwana Tendwa alisema Chama au mgombea binafsi anatakiwa kujaza fomu za kiapo cha matumizi ya fedha wakati wa uchaguzi kwa kipindi cha siku saba baada ya tarehe ya kupitishwa na kukidhi vigezo vya Tume ya Uchaguzi.
Bwana Tendwa alisema chama kinatakiwa kuelezea kina kiasi gani cha fedha za matumizi wakati wa kampeni na kitatumia kiasi gani na kinategemea kupata kiasi gani kwa kujaza fomu maalumu ya kiapo cha matumizi ya fedha za kampeni za uchaguzi mkuu.
Aidha Msajili alisema hata mgombea wa nafasi ya ubunge anatakiwa pia kujaza fomu maalumu za hati ya kiapo kwa kipindi kisichozidi siku saba baada ya tarehe ya kupitishwa na Tume kwa kuelezea kiasi alichonacho ikiwa ni pomoja na kiasi atakachotumia na kiasi gani anachotegemea kupata kutoka kwa wafadhili.
Bwana Tendwa aliongezea kuwa baada ya uchaguzi wagombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Vyama kwa Ujumla watatakiwa kuelezea kwa kujaza fomu ya hati ya kiapo kuthibitisha kiasi gani walichotumia wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na kutaja chanzo cha pesa walizotumia wakati wa kampeni.
Alisema wagombea wa nafasi ya Ubunge watatakiwa kutoa risiti kwa Msajili wa Vyama vya siasa baada ya kampeni za uchaguzi ikiwa ni uthibitisho wa matumizi ya pesa walizojaza wakati wa kiapo cha kwanza.
Bwana Tendwa alisema kwa upande wa Vyama vitatakiwa kutoa uthibitisho wa risiti kwa msajili wa vyama vya siasa baada ya siku 180 na kuelezea kuwa sababu kuu ni vyama vinawagombea wengi.
Alifafanua kuwa Chama au mgombea wa nafasi ya Ubunge atazidisha bajeti aliyoapa katika hati ya kwanza kabla ya Uchaguzi kwa asilimia 15 anatakiwa kuitolea maelezo na ikiwa atazidisha zaidi ya asilimia 15 atatachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kulipa faini ambayo hakuitaja.
Wakati huo huo Bwana Tendwa alisema Ofisi yake imejipanga vya kutosha na imefungua matawi katika mikoa mbalimba ikiwa ni pamoja na Mbeya,Mwanza,Dar na Zanzibar
Bwana Tendwa alisema lengo kubwa la Sheria hiyo ni kudhibiti tatizo la rushwa wakati wa shughuli za kampeni za uchaguzi mkuu

Mnavionea vyama vidogo. Nyie ni tembo kukanyaga majani bila huruma. Mnataka nchi muile tu nyie wenyeew kiulaini watu wengine wasipite kabisa. Nyie wanyimeni watu tu haki zao kila siku kwa kujidai kuweka vikwazo hivi na vile mwishowe watu watachoka kuteseka na ndio hapo itakua Burundi sijui hayo mahela yenu mutayalia wapi watu wakianza kukatana vichwa.
ReplyDelete