Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh.Mohammed Babu akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ndege mpya ya Precision Air aina ya ART 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abiria 48 katika uwanja wa J.K. Nyerere International Air Port ambayo itafanya safari zake kati ya Dar - Bukoba - Dar, ndege hiyo ambayo iliruka leo kutoka Dar kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake hizo za Dar - Bukoba -Dar mapema mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CitiBank,Jamal Hussein , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji wa Precision Air,Allan Sharra na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk


Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo,Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu CitiBank na mwisho kushoto ni Lucy Malu Meneja Mkazi Kenya Airways.

ndege mpya ya Precision Air ATR 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abilia 48 itakayofanya safari zake kati ya Dar na Bukoba ikitua katika uwanja wa J.K.Nyerere.
baadhi wa Marubani wa Precisiano Air wakiwa katika uzinduzi huo leo.

(Picha na Full Shangwe Blog)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Absolutely fantastic.... Unatoka London moja kwa moja mpaka Bukoba...Asante saana wajasirimali wa Precision Air.

    ReplyDelete
  2. jamani bado tunakata mapanga tu ndege gani hiyo tafadhali

    ReplyDelete
  3. HII NIABU YA KUSIKITISHA, YAANI SHIRIKA BINAFSI KILA SIKU LINASHUSKA KITU KIPYA, ATCL YA SERIKALI IPO ICU. WATANZANIA TUMEROGWA NA ALIYETULOGA KAFA. MPENI DR. SLAA NCHI.

    ReplyDelete
  4. Michuzi
    Huyo dada wa kushoto kabisa nimeona cha ndani,amenikuna kweli......hauna contact yake????

    chaos

    ReplyDelete
  5. http://www.youtube.com/watch?v=Jh2jQcnWcQo&feature=player_embedded
    the future Kigamboni

    ReplyDelete
  6. @ Annony wa Tue Aug 31, 08:18:00 AM: Hivi unadhani wanaomiliki Precision Air ni akina nani? nyuma ya pazia wako hao wanene wa nchi hii.. na huenda hata viongozi wa ATCL wamo..hivi kweli uandhani hapo watakuwa na hamasa kuiendeleza ATCL? wanaiua ATCL kwa makusudi ili wao waendelee kufaidika na biashara.

    ReplyDelete
  7. Tehe teh teh!

    Safi sana Michuzi. Picha nzuri zinavutia.

    Huyo Anony wa hapo juu anaeomba kontakts mbona anaingilia kazi za watu?

    ReplyDelete
  8. We michuzi ndege gani mpya ina makataupepo ya nje?
    Hii technolojia ya mwaka 47 ndo waafrika tunaambiwa mpya!
    Ndege ya hivyo sipandi ng'o! Hata kama kwenda moshi ni elf ishirini!!

    ReplyDelete
  9. @anonymous 08:06:00 AM, Ndege za mapanga zina ubora zaidi kwasababu zina stahimili mazingira mangumu ya airport zetu za ndani. Ndio maana ndeze nyingi za Kijeshi especially za wenzetu Wamarekani, Warusi, na Waingereza ndegezao za mizigo vitani ni zenye mapanga. Zina uwezo wa kustahimili, vumbi, rough ranways, vile viel siyo rahisi kwa ndege kuingia kwenye engine kutokana mapanga yake. Kwa hivyo basi, hawa jamaa wa Precision, wana jua wanacho fanya.

    ReplyDelete
  10. Watu badala waangalie ndege mpya ipo kiwanjani,wanaangalia mipaja ya pilot.

    Mzee wa pajaaaaaz + titiiiiiiz upo?mbona cku hizi kimya au ndo mambo ya mfungo upo kimya!

    ReplyDelete
  11. Hata watengenezaji wa ndege wenyewe wanatumia za mapanga kata!

    Achana na kulilia vya usasa! Tengeneza vya kwako!

    ReplyDelete
  12. Nilikuwa naogopa vile vidogo vya kubeba abiria 15. Nilikuwa nimeisha zoea kupanda Meli mpaka Mwanza then Mwza to Dar ama DAR to Mwza,then Meli. Sasa naona safari yangu ya Dec itakuwa bomba. Waambie basi wafanye Entebbe to BUKOBA. Make muda mwingine napiga za USA to ENTEBBE, then Bukoba.

    Mdau POPOTE

    ReplyDelete
  13. Mdau hapo juu inaonesha nyinyi ni wale wale akina wanshomile...kwa majisifu mliyonayo?
    Mdau Mbije A,B-mweusi kaa nyinyi lakini mimi mtu wa mbeya

    ReplyDelete
  14. afadhali wameleta hii kubwa kidogo maana mateso ya vile vi-foka sijui videge viduchu kama popo vinapepea ziwani kama kishada bwana!!mtu unasafiri unapiga kelele na BP juu

    precision angalau wanasaidia

    ReplyDelete
  15. toto la kike,safi saaana
    nimekupenda kinyama
    &$#^^5*(( kabisa lol...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...