Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia Simba anayepita karibu na magari yao wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kujionea wanyama na mambo mbali mbali yalipo katika hifadhi hiyo.
Baadhi ya warembo wanoshiriki mashindano ya Kumsaka Vodacom Miss Tanzania wakicheza ngoma ya Kimasai wakati walipokaribishwa katika Boma la wafugaji hao lililopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakitoka katika nyumba za Tembe za wafugaji wa jamii ya Kimasai waishio katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakinunua shanga za kimasai kutoka kwa wauzaji waliopo katika Boma lililopo katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hongera kwa waandaaji.warembo wanaenjoy ni kambi nzuri wengi hawatasahau.

    ReplyDelete
  2. Kuleni bata tu watoto. Angalau kwa watakaoshindwa mtakua mmetesa kidogo!

    ReplyDelete
  3. Bado sijaona mrembo apo!

    ReplyDelete
  4. Huyu mwingine anatumia simu kwenye stage kama hii muhimu!

    ReplyDelete
  5. Ww anon wa Tue Aug 24, 05:07:00 PM uayesema, "Bado sijaona mrembo apo!" hebu tuoneshe demu wako basi.

    ReplyDelete
  6. Mbona huonyeshi mchakato of miss universe hahahhah au kwavile hatukufika kokote hahahhahah

    ReplyDelete
  7. Michuzi, acha kubana mitundiko mingine kuhusu hizo nywele feki na matarajio ya Miss Universe; au endapo hao warembo walikaribishwa vyakula vya wazawa hapo Ngorongoro!

    Kama hukuipokea hiyo mitundiko, basi niko radhi kukuletea tena!

    ReplyDelete
  8. Sijaelewa hizo namba porini huko za nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...