Mkurugenzi wa Lino Interanational Agency, Waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Hashim Lundenga akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasicahana Maasai ya Mkoani Arusha jana wakati warembo wa Vodacom Miss Tanzania walipoitembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa wameshikilia vyandarua kabla ya kugawa vyandarua kwa baadhi ya wakazi wa mto wa Mbu mkoani Manyara jana. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutuio vya Utalii na kuhamasisha Utalii wa ndani ya nchini.Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimkabidhi chandarua Maria Charles, mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara wakati warembo hao walipoambatana na Balozi wa Kampeni ya Malaria Haikubaliki Mwasiti Almas (hayupo pichani). Warembo wa Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Henry Tzamburakis (kulia) akimkabidhi vyandarua Mganga wa Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara Frank Sanga jana ambapo Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 waliopo katika ziara ya kutembelea Vivutio vya Utalii Kanda ya Kaskazini. Katikati ni Balozi wa Malaria Haikubaliki nchini, Mwasiti Almasi.
Balozi wa Kampeni ya Malaria Haikubaliki ambaye pia ni mwanamuziki Mwasiti Almas pamoja na baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimkabidhi chandarua , mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara. Warembo wa Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Paulina Lowasa dada wa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowasa, akiwapa mkono wa kuwatakia heri Warembo wa Vodacom Miss Tanzania alipokutana nao Wilayani Monduli mkoni Arusha na kuwapa zawadi ya vikoi vya kimaasai warembo wote 30. Warembo hao wanatembelea Kanda ya Kaskazini kuangalia vivutio vya Utalii nchini.
Washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa UWT Wilayani Monduli pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania baada ya akina mama hao kuwapa zawadi ya vikoi vya kimasai na kuwatakia kila la heri katika mashindano hayo yatakayo fikia Kilele Septemba 11 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hakuna miss hapo. Wote wapo Shortee- (wafupi), avu wabaya. Bora ya house girl wangu...

    ReplyDelete
  2. watoto bado mnakula bata tu. mjini mnarudi lini?

    ReplyDelete
  3. Hawa na wale waliowavalisha hawa "warembo" wote wajinga. Kuwapeleka vijijini ni jeans zimewabana ni ujinga tu. Au ndio "usasa?" (modernity). Tanzania kuna makabila zaidi ya 120; lazima hawa "warembo" wavae hivi vi-jeans kwenda vijijini? Nawaheshimu sana Wamasai kwa kuwa wanajivunia mila, desturi na utamaduni wao. SI kama hawa.....

    ReplyDelete
  4. Hao ma misi Kila mwaka ni ktembelea mbuka za SErengeti, Arusha, yaani maeneo ya kaskazini mwa nchi yetu tu why, kwa nini hawafiki KIGOMA mbuga ya wanyama Gombe kama swala ni kutembelea mbuga za wanyama?

    Bwana LUNDENGA mwaka kesho tuone wakienda kigoma kutembelea hata kituo cha living stone na mbuga ya wanyama ya GOMBE.

    ReplyDelete
  5. Hiyo pich aya tano toka juu hapo. Mgonjwa huyo ni miss kuliko ma miss. Yaani mgonjwa utazania ni wakuadvertise tangazo fulani. Wote na mtoto wake they are just lovely...

    ReplyDelete
  6. Wakati wenzetu hawalali wanafanya utafiti wa kisayansi, sisi tupo tu mara Miss Kindoni mara miss chuo, mara miss manzese... You can take this to the bank..hata vitukuu vyetu havitaona maendeleo ya maana...

    While I fully support beauty and comes with it, I am a bit sceptical with how we are handling this issue

    ReplyDelete
  7. Mdau wa 07:40:00 PM, Nakubaliana 100% na wewe. Tanzania watu wamekuwa mafukara kabisa katika utamaduni na maskini katika ubunifu. Ndiyo maana wamekuwa malimbukeni wa mashindano ya "warembo" ambapo wasichana wanapitishwa kuonyeshwa jukwaani kama vile ng'ombe katika maonyesho ya kilimo! Mara miss kusini, miss gongo la mboto, miss vyuo, miss utumbo gani sijui, n.k. Hakuna ubunifu wowote!!! Kama alivyosema mdau hapa juu, maskini ya Mungu hawa wakishavaa vi-jeans uchwara vyao na vi-tee shirts basi wanajiona eti wamefika kwenye "usasa". Modernity italetwa na kusoma, kufanya kazi kwa maarifa na bidii na kufikiri na kutenda na SIYO na ulimbukeni kama huu au watu kuvaa tai Dar majira ya joto na kufa kiofisa. Tuamkeni. It's not too late.

    ReplyDelete
  8. Ha ha ha!!!!??? Lundenga unawapeleka hao watu wako kwa wanafunzi wa kike wawaambukize nini? Wapeleke kwa wanye tabia kama zao sio watoto wanaosoma, utawaaribu pia.

    Nakushukuru sana dada Lowassa kuwavalisha, maana vivazi vyao vilikuwa vinatisha na hayo ni maeneo ya kiheshima (kijadi)inabidi wavae kiadabu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...