Wanasiasa 10 walipata ajali mbaya alitokea mkulima mmoja alichimba shimo na kuwazika, Polisi walikuja na kuanza kumhoji;

Polisi:Uliona ajali?
Mkulima:Hapana, nilikuta imeshatokea na maiti zimezagaa.
Polisi:Zipo wapi maiti?
Mkulima:Nimezizika.
Polisi:Una uhakika wote wamekufa?
Mkulima:Kuna wengine walikuwa wanalalamika kwamba hawajafa lakini si unajua wanasiasa walivyo waongo! mimi nikajua tu wanadanganya nikawazika wote...

Na Mdau LS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. teh teh teh thats so funny.
    Ippy

    ReplyDelete
  2. jamani sasa wanasiasa wanalo kwa hari hii na jinsi wanavyoongozana kurudisha fomu ndio tutawazika wooote na itkuwa bora couse wanakela sana

    ReplyDelete
  3. Ni ucheshi wenye kufikirisha. Lakini pengine angeachia japo wanasiasa wachache kwani wanasiasa wote si waongo.

    Toleo la Kiingereza la ucheshi huu linapatikana hapa:

    http://matondo.blogspot.com/2010/03/kisa-cha-mkulima-mzee-aliyechoshwa-na.html

    ReplyDelete
  4. NOT FUNNY!

    ReplyDelete
  5. Nafikiri mkulima yuko sahihi na hasa tukitumia uzoefu wetu sisi waafrika, wanasiasa wetu ni waongo kupindukia na ndio maana hata wapiga kula aaah!! samahani wapiga kura wanajitokeza kwa uchache vipindi vya uchaguzi

    ReplyDelete
  6. hahaha humo mgosi makamba asinge kosekana!

    ReplyDelete
  7. BILA SHAKA WOTE WALIKUWA WA CCM, HILO HALINA UBISHII

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...