Yale ya Uwanja mpya wa Taifa yamejirudia tena Mchikichini jirani na Kiwanda cha Bia.Tarehe 6 Aug 2010, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, alizindua rasmi mradi wa maji safi uliotolewa kwa hisani ya TBL kwa Wakazi wanaozunguka eneo hilo.TBL iliwataka wakazi kutunza huduma hiyo.Chini ya Wiki 2, huduma hii imeharibiwa na kuachwa katika hali mbaya.Mabomba yote yemeibwa na eneo lote limeachwa katika hali ya uchafu uliokithiri.
Ni lini tutakuwa wastaarabu na kutunza miundo mbinu inayotufaidisha?
Mdau Mchikichini.





Inatia Uchungu sana kuona hali kama hii, tatizo kubwa ni kwamba usikurupuke tu kwenda kufanya kitu kabala hujajiuliza utakitunza namna gani? Elimu kwa umma ni muhimu sana. Waulize wananchi kwanza huo mradi je wapo tayari kuutunza? Sasa naona hao jamaa walioweka maji kazi bado haijaisha kwani utekelezaji ulikuwa ni wa kizembe. Naona na wenyewe walikuwa wamekunywa bia wakaamka tu nakwenda kuweka maji as long tunamafundi na pesa hakuna tataizo.Yani hawa waswahili wakishapata oder kutoka kwa hao makaburu kawekeni bomba ina maan nyie hamjui jumui zenu na tabia zao. Lengo lilikuwa zuri lakini think tank hakuna. Waulize KILL water walifanikiwa namna gani kueneza maji mkoa wa kilimanjaro?
ReplyDeleteKunguru hafugiki bwana ..
ReplyDeleteHii inasikitisha sana,naukumbuka vizuri sana huu uzinduzi,ilikuwa juzi kati tu,haya yatakuwa ni matokeo ya biashara ya vyuma chakavu.KWELI,ALIYETUROGA ALISHAKUFA.
ReplyDeletekitu kinachotukosesha mambo mengi ni nidhamu, watanzania hawana nidhamu hata kidogo na kama huna nidhani hata maendeleo yako nayo yatakuwa finyu......uwanja wa taifa umefunguliwa tu mara baada ya muda mchache watu wakaanza kunya kwenye masinki ya kuoshea mikono sasa ustaarabu gani huo?....
ReplyDeleteSave water..drink beer!"
ReplyDeletehii ni aibu sana jamani, hivi ni kwa nini serikali isipige marufuku biashara ya vyuma chakavu? manake wanaiba hadi mageti ya watu wanapeleka huko viwandani, na serikali inajua ila imeuchuna tu! mkuu wa mkoa dar unafanya nini kuzuia upuuzi huu??
ReplyDeleteBila Bia Hakuna Uhai
ReplyDeletePole sana TBL
USTAARABU UTAKUJA SERIKALI IKIACHA KUIBIA WATU WAKE. JAMANI HII NI WAKE UP CALL!! KUWA NCHI KWISHNEY, LABDA KUWE NA CHANGES. . . .
ReplyDeleteAISEE....HUWEZI KUAMINI, SASA MNATAKA MSAIDIWE VIPI????, KAZI KULALAMIKA TU OOHO MAFISADI MAFISADI, SASA KAMA MNAWEKEWA HUDUMA MUHIMU KAMA HII YA MAJI, HALAFU MNAKUJA KUIBA MABOMBA...HUO SI UCHIZI HUO JAMANI???...MNAFANYA WATU WAKATE TAMAA KUWASAIDIA NA WANAISHIA KUJISAIDIA WENYEWE....BADI SIAMINI...WIKI MBILI TU...DUH
ReplyDeletejinsi nilivyo na shida ya maji huku ninakoishi! Daaaah....! imenigusa kweli!
ReplyDeleteDamn!
ReplyDeleteNyie shangaeni, Tembeleeni mabweni ya UDOM vyooni hasa Mabweni ya Education na baadhi ya vyoo vya madarasani muone kama mtakuta mabomba, na hiki ndo chuo kipya kabisa na kizuri kwa majengo.
ReplyDeleteMi nasema tusipobadilisha sheria za nchi yetu zikawa kama za china, hatutaendelea kamwe.
Inatia uchungu sana, hata wasomi ni waharibifu, utakuta na bustani zilizomwagiliwa vizuri mtu anakatisha, wakati mwingine kupitia dirishani/
Bongo Discipline Hakuna, Tembelea Rwanda upate habari yake, Displine ya kufa mtu, hata gari chafu halikanyagi jiji la kigali.
Barabarani trafiki hakagui lesseni akiwa karibu yako, anaichukua na kwenda mbali ili usimshawishi.
Mi naona JK akishapita, avae miwani ya mbao displine iwe kwa kwenda mbele.
Ni utamadubi wetu sie waafrika na hususan watanzania, katika kufanya uharibifu hata kama tutapata hasa sisi wenyewe. Uwanja wa taifa watu wameiba vioo vya kunyia, na hakuna kitu kinachoendelezwa hapa.
ReplyDeleteAcha tuudumishe utamaduni huo huo watu watucheke huku wanazidi kutupa msaada na kututangazia.. aibu kama hii na bado hatutajirekebisha.. uvivu, udokozi, utegezi, uharibifu, na kutaka missada na pesa BURE ndio tumekumbatia...
baada ya mikaka mia moja bado tutakuwa na hali hii hii.. eti watu wanatoka nje wanatusaidia.. hebu tizameni nchi nyenzetu zinavyopiga hatua..
tatizo ni watanzania tu, nchi hii haindelei kwa sababu watanzania sisi ni watu wa ajabu, haitajiki elimu kwa utumiaji wa mradi wa maji kwani kila mahali kuna shida angalau ya maji safi,na hilo eneo huwa lina shida ya maji, nahisi wale vijana wanaouza maji ndio wameharibu maana biashara yao ilikufa kiaina.
ReplyDeletePoleni TBL hawa ndio watanzania bwana.
Mnashangaa nini wabongo wenzangu? Mlivyosema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake mlikua hamjui madhara yake? Hakuna wa kulaumu ila nafsi zetu ndizo za kulaumiwa kwani kila mtu katika nchi hii anajiona mjanja na mjuaji kisa eti bongo.Kila mtu hapo alipo ajitazame anavyofanya uhalifu wa aina hiyo hiyo (matumizi mabaya ya mali za umma,muda,pesa,wizi, nk)
ReplyDeleteHUKO NI KUTO STAARABIKA KWETU WENYEWE NA KUKOSA ELIMU YA KUTOSHA MAANA TABIA HIZI KTK JIJI LA DAR ZIMEKUWA NI KERO KUBWA SANA KWA SASA NA SHANGAA VIONGOZI WANAZIFUMBIA MACHO TU KAMA VILE HAWAONI,HAPA DAWA NI KUPIGA MARUFUKU UUZWAJI WA VYUMA CHAKAVU KOTE NCHINI KAMA WALIVYO FANYA MKOANI MOROGORO SASA HILI LIWE NI LA NCHI NZIMA PIA MADUKA YA VIFAA VILIVYOTUMIKA PIA YANGEPIGWA MARUFUKU NAFIKILI HUU UPUMBAVU UNGETOKOMEA MARA MOJA COZ HATA HUKU MTAANI MIFUNIKO YA CHEMBA ZA MAJI TAKA PIA NA ILE YA BALABALRANI WANAIIBA SANA HAWA WATU WANAKERA SANA NA TUNAWAONA WANAPITA MTAANI WAKITANGAZA WANANUNUA VITU CHAKAVU WAKIWA NA MIKOKOTENI WAKIKUSANYA HIVYO VITU INAUMA SANA INAUMA SANA NA NIAIBU KWA WAGENI JAMANI WATANZANIA NI WAPITUNAENDA????????
ReplyDeleteHapa tatizo si la wananchi. Tatizo ni la nchi imekua ya ufisadi sana na watu wamekua magreed mno. Kila mtu anataka kila kitu atumie peke yake au na familia yake.
ReplyDeleteImani na upendo umeisha kwa watu ndio maana kila wanachoona kinawafaa wanachukua bila kujali wengine wataathirika vipi. Wanajua wasipochukua wao watachukua wengine tu.
Huyu aliyechukua hizo bomba ana tofauti gani na mtu anayekula hela za watoto yatima, hela za watu walioathirika, hela za kujengea shule za wanafunzi na kuwaacha wakae chini, tofauti gani na mla rushwa ambaye hajali utalishaje wanao? Hawana tofauti yeyote, tofauti yao ni aina ya uchukuzi huo lakini the end result is the same...
Tunahitaji kuchange toka kwa viongozi wa juu mpaka chini. Wote mnajua ukiwa na familia hata kama ulivyokua kijana ulikua brazaman kila mtu mtaani anajua jina lako lakini ukiwa mkubwa na kupata familia unajikuta unabadili tabia yako ili wanao waone mfano mzuri. Unakua a good role model kwa watoto wako lakini viongozi wetu wengi ambao ni kama wao bado ni brazamen. Utundu huu bado hawajauacha hivyo watoto wanaiga, tumlaumu nani?
Tangu lini kitu cha bure kina mwenyewe?
ReplyDeleteTBL acheni show off kwa watu wasio hitaji huduma yeni, mungepeleka vijijini mngeshukuriwa zaidi.
Ni aibu kubwa na inatia uchungu sana. This is a disgrace to civilised Tanzanians who care about their society. Kweli discipline na accountability ZERO kabisa ......Jamani when will things change?????? TUMECHOKA NA LEGELEGE...kama watu hawawezi kuishi mjini warudi shamba ...washamba wakubwa!!!!!!
ReplyDeleteVita ya marekani na washirika wake nchini Afghastan siyo kuzuia ugaidi tu ni kuzuia madhara ya madawa ya kulevya kwenye nchi zao, USA,M UK na nchi nyingi kwenye bara ya ulaya na marekani walengwa wa madaya ni matagiri hawa wakibwiya hatafanyakazi tena kwahiyo serikali haitapata kodi tena, lakini Tanzania walengwa wa madawa ni madereva wa daladala na wapiga debe wao hawa kama hawana hela wanaenda kuiba bomba la maji hili ni tatizo, haya labda yangepungua kama marehemu Amina Chifupa angepewa ushirikiano wa kutosha, lakini jeshi la polisi orodha mliyopewa ilifanyakazi?sasa Lukuvi omba hiyo orodha kwa Said Mwema tatizo la vibaka na wizi wa mabomba utakwisha. Hii inaonyesha serikali ya ccm imelala au inajua nani waingizaji madawa au wanachangia hata kampeini hilo ndilo tatizo la kuchanganya siasa na biashara ni lazima hela chafu zitatumika katika kuchagua viongozi na return yake huna sauti nao.
ReplyDeleteMdau Uk.
China watu kama hawa wananyongwa tu hakuna lolote jengine.. na ndio maana wameendelea.. kwetu sisi kwanza tunaomba, baada ya hapo tukipewa msaada tunaharibu, ikisha bila ya kuona haya tunaomba zaidi.. tushakua hatuna aibu na watu wanatucheka tuuu - tumekaa tukicheza ngoma tuu - wenzetu washafika mwezini washarudi..
ReplyDelete