Kaka Michuzi,
Nimekutana na hii hali mitaa ya kibaha, vyandarua vya JK vinalinda vifaranga dhidi ya mwewe badala ya kulinda mbu dhidi ya watoto. Kweli Mwewe hakubaliki sio mbu tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi nimeipenda hii ni kali ya mwaka, Ni vizuri watu wakapata elimu muafaka kwa hivi vitu na pia serikali itafute namna ya kutokomeza hawa mbu maana mikoa ya pwani na joto linavyokuwa kali kulala na net nikitendawili kingine.

    ReplyDelete
  2. hehehehehe hii kali,tutafika kweli.mmh

    ReplyDelete
  3. mh!
    kulinda mbu dhidi ya watoto???

    ReplyDelete
  4. Amaaakweli, hiya ndio mambo ya kupigiwa mfano. Gharama za utengeneza wa hivyo vyandarua ni ya hali ya juu ambayo kama isingekuwa hivyo hiyo pesa ingetumika kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo. Ingekuwa ni uwezo wangu na mamlaka yangu, mtu aliyefanya kitendo hicho angefunguliwa mashitaka sawa na yale ya kuhujumu uchumi ili iwe fundisho. Ifike mahali Watanzania tujionee huruma. Kisingetumika kuzuilia vifaranga visiliwe na Mwewe, chandarua hicho kingekuwa kimeokoa maisha ya Mtanzania mahali pengine.

    Mdau, Jacob

    ReplyDelete
  5. kweli mchawi aliyeturoga watanzania alisha kufa

    ReplyDelete
  6. MCHANA KINATUMIKA KUKINGA VIFARANGA DHIDI YA KUNGURU NA USIKU VINATUMIKA KUKINGA BINADAMU DHIDI YA UMBU.

    ReplyDelete
  7. HAYA NDIO MADHARA YA UMASIKINI

    ReplyDelete
  8. MKAPA ALISEMA KAZI YAKE YA URAIS ILIKUWA NGUMU SANA KWANI ALIKUWA NA KAZI YA KUFUNDISHA WATU KUTUMIA VYOO TENA VYA SHIMO.

    ReplyDelete
  9. Du, wabongo ni noma ! yaani msaada wa "watu wa marekani" umeishia hapo ?

    ReplyDelete
  10. Lazima mkono uende kinywani kwanza

    ReplyDelete
  11. bila chakula kuna haja ya kuleta vyandurua. na huyo mbu atanyonya nini. eti vyandurua vya jk...stupid!

    ReplyDelete
  12. Hakika watanzania wabunifu. Tehe teheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  13. Ndiyo mtu anayo haki ya kutumia mali yake kadari anayoona inafaa! Angalizo kidogo: Vynadaru hivi si vya JK; ni mali ya Rais Mstaafu G. Bush wa Amerika. Alitupatia Wadanganyika baada ya kukubali kupitia kwa Rais wetu kuwa hatutabadilisha mikataba ya Barrick na kampuni zingine za Migodi: Vyandarua ni karibu Millioni moja hivi za Amerika! Lakini kama tungebadilisha Mkatabab na kuweka Clause ya "windfall Tax", hivyo basi wangekuwa wanalipa kwa sasa kwenye kiwango cha US$1,924.00 badala ya zamani ya ounce kwa US$ 270.00. Hii ilikuwa fainda kwa watu wa amerika ambao wamewekeza kwenye Kampuni ya Canda ya Migodi hiyo na pia familia na maradiki wa Bush. Alikaa Dar siku tatu na kumweka sawa Rais wetu Mrisho Abdalah Kikwete! Kweli sasa wacha na kuku wafaidi, maana kwa kupokea msaada huo tulionyesh wazi kuwa sisi watangaynika Ubongo wetu ni sawa na Kifaranga cha KUKU!

    ReplyDelete
  14. vyandaruwa vinalinda kuku dhidi ya mbu hujapata mantiki weye.

    ReplyDelete
  15. Very creative.

    Mchana mwewe hakubaliki Na usiku maralia haikubaliki/ mbu hakubaliki ukizingatia mbu waenezao maralia ni wale wanaomng'ata binadamu usiku wa manane.

    Hata hivyo utafiti ulifanyika ni wangapi wanaovitaka hivyo vyandarua na kujua wangapi wanavyo vya ziada.

    Na je ubora wa vyadarua vya msaada ni sawa na vya kununua Dukani?

    Huenda ndoa maana wameamua kukingia vifaranga.

    ReplyDelete
  16. Anonym. wa 08.10 PM umenena.

    ReplyDelete
  17. mdau 8:10 sio MARALIA ni MALARIA loohhh! aibu!

    ReplyDelete
  18. akili mali,Vifaranga vikikuwa hatauza na atanunua vyandarua vya kutosha...ila kwasasa acha kuku wawe geti kali...

    note: WALIOGAIWA VYANDARUA SI WALE WENYE SHIDA NAVYO..ULITEGEMEA NINI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...